ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, August 29, 2013

BAADA YA KUMALIZA KIFUNGO KWANEEMA FM YA JIJINI MWANZA YAREJEA HEWANI

Kituo cha Radio ya Injili Kwaneema Fm cha jijini Mwanza  ambacho mapema mwaka huu kilifungiwa na kuamriwa na serikali ya Tanzania kupitia TCRA  kusitisha urushaji wa matangazo yake kwa muda wa miezi 6, kutokana kutuhumiwa kuhusika na uchochezi wa kidini hususani katika suala tata la uchinjaji wa kitoweo cha nyama hatimaye muda wa kifungo hicho umemalizika na kituo hicho tayari kimeanza kurusha matangazo yake kwa mara nyingine tena.

Kwaneema Fm inarejea hewani ikiwa bado mmiliki wa kituo hicho Askofu Bishop Mpemba anasakwa na jeshi la polisi Mwanza na huku akiwa hajulikani wapi alipo.

Bishop huyo anakabiliwa na mashtaka ya kujibu  kwa kuchapisha DVD inayoitwa 'INUKA CHINJA ULE' inayotajwa kuwa na uchochezi wa kidini ndani yake.

Radio Kwaneema Fm 98.20 Mhz ya jijini Mwanza imeanza kusikika hewani kuanzia jana Jumatano August 28/2013 majira ya saa 11alfajiri chini ya masharti waliyopewa na TCRA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.