ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 1, 2013

WAZIRI MKUU KESHO KUFUNGUA SHEREHE ZA BULABO 2013 MAANDALIZI YAKAMILIKA ASILIMIA 99.9

Tamasha la Bulabo huusisha ushindani wa ngoma za asili za watu wa kabila la wasukuma, na katika ushindani  waganga na wachawi huusishwa ili kupata ushindi, na hii ndiyo kamati ya ufundi, unaambiwa kwamba jamaa hawa wamejipaka dawa ambazo hawapaswi kuoga wiki nzima ya tamasha la Bulabo yaani mpaka litakapomalizika na wana masharti hawatakiwi kuzungumza na mtu mwingine zaidi ya watu wao tu!! (kwao ni tabasamu na minuno)

Mara baada ya kuwasili leo kwenyehimaya ya hii ya makumbusho ya Bujora walipaka dawa zao na kuelekea moja kwa moja uwanja wa tukio na kufanya mambo yao ya kamati wakizindika dawa zao pande zote za uwanja kisha wakarejea hapa eneo la matayarisho na kuwa kama sehemu ya watizamaji huku wakiwa kimyaaaa. 


Chekshia Kideo....upate uhondo wa pasha pasha za maandalizi kuelekea Bulabo.

Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo ili wasili Kisesa na kudhuru maeneo yote kwaajili ya kuhakiki na kufanya ukaguzi mahususi kwaajili ya ugeni wa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda ambaye ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi tarehe 2 juni 2013.

Mteni wa watu wa kabila la Wachaga ajulikanaye kwa jina la Mtemi Mariale (wa pili kutoka kulia) ambaye ni mwenyekiti wa watemi wote nchini naye ni mualikwa kwenye tamasha hili la tamaduni za watu wa kabila la wasukuma.

Katika viwanja hivi nakutana na Shangazi yangu ambaye naye ni Mtemi wa koo za eneo la Shinyanga.

Watoto ni sehemu ya tamasha la Bulabo hivyo walijumuika hapa mapema, unaowaona pichani ni viongozi wa watoto wao wakijinoa zaidi katika kukariri yanayopaswa kuzungumzwa shereheni kwani wataandamana wakirusha maua na kupaza sauti zao kwa kauli moja kwenye paredi. 

Ngoma ya Wigashe ikijinoa.

Hapa palikuwa patamu.

Mwnyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Paul Bomani akiwapungia mikono wadau wa ngoma za jadi mara baada ya kuwasili kituo cha Bujora.


Diwani wa kata ya Kisesa Mh. Clement akimkaribisha Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Paul Bomani ambaye pia ni mlezi wa jumba la makumbusho la Bujora ili kupata kuzungumza na watemi waliokusanyika hapa ukumbini.

Mwenyekiti wa Kampuni ya bia ya Serengeti Paul Bomani ambaye pia ni mlezi wa jumba la makumbusho lya watu wa kabila la Wasukuma yaani  Bujora akizungumza na watemi waliohudhuria kikao cha maandalizi jioni ya leo.

Mwaka huu 2013 Bulabo imechukuwa sura mpya, kwani idadi ya watu wengi inatajwa kuahidi kuhudhuria wakiwemo viongozi na makampuni mbalimbali, vikumndi mbalimbali vya ngoma asili vimejiandikisha kushiriki mashindano kikubwa zaidi ni ugeni wa Mh. waziri Mkuu.  

Pichani Mwenyekiti akisalimiana nakijana wake' mara baada ya kikao cha maandalizi kukamilika usiku wa leo hapa Bujora Kisesa mkoani Mwanza,  Watemi kutoka Moshi, Tabora na sehemu mbalimbali hapa nchini wamehudhuria kupata ujuzi na kujenga umoja. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.