ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 10, 2013

TCRA YAAMURU CHANEL YA STAR TV IREJEE MARA MOJA KATIKA VING'AMUZI VYA STAR TIMES

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Prof. John Nkoma akitoa maamuzi kuhusu kujitoa kwa Star TV kwenye Star Times. 

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) leo imekiagiza kituo cha Star Tv kurejesha  mara moja mawasiliano yake kwenye king'amuzi cha Star Times  leo juni 10 kabla ya saa 10 jioni. BOFYA PLAY SIKILIZA 
 

Aidha Star Times na Star TV wameelezwa kuwa wote wamevunja sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta ya 2010 na Kanuni zake na kutakuwa na kujitetea tarehe 17 Juni 2013.
 

Agizo la kurudishwa kwa Chaneli ya Star TV linatakiwa kutekelezwa ili kuhakikisha kuwa wananchi hawanyimwi haki ya kupata habari kwa vituo vitano vya bure vilivyoainishwa.
 

Vile vile wote wametakiwa kufuata Sheria inapotokea kutokuafikiana badala ya kutoa maamuzi bila kumshirikisha Mdhibiti (TCRA)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.