ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 6, 2013

MALKIA WA TAARAB HADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE

Jafari Ally enzi za uhai wake akiwa na mkewe Malkia wa Mipasho nchini Tanzania, Khadija Omar Kopa wakifuatilia onesho la Mshauzi Classic ndani ya Mango Garden. 

Habari zilizoufiki mtandao huu hivi punde zinasema kuwa Kijana mtanashati aliyekuwa Mume wa Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa, aliyefahamika kwa jina la Jafari Ally, amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa akitibia kile kilichoelezwa alikuwa akisumbuliwa na kifua. 

Jafari na Khadija Kopa, walifunga ndoa mwaka 2008.
 Wakati kifo hicho kinatokea mke wake hakuwepo jijini Dar, kwani alikuwa safarini Rukwa alikokwenda na kundi zima la TOT kwa ajili ya kusherehesha Sherehe za Siku ya Mazingira Duniani zilizofanyika Kitaifa mkoani humo, ambapo leo anatarajia kuwasili jijini. 

Ratiba kamili ya msiba huo bado hadi sasa haijafahamika lakini inadhaniwa huenda msiba huo ukawa  maeneo ya Chalinze au Lugoba ambako ni nyumbani kwa wazazi wa Marehemu.
CHANZO: FATHER KIDEVU

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.