ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 5, 2013

BHARTI AIRTEL YASAIDIA KUONDOA UMASKINI KUPITIA MRADI WA MILLENIUM VILLAGE

Meneja huduma kwa jamii wa Airtel Hawa Bayumi akiongea wafanyakazi wa afya wa mradi wa millenium village wakati akikabithi simcards 240 zitakazowasaidia wafanya kazi hao kuwasiliana kwa bei nafuu na kutoa huduma kwa wakazi wa Mbola Tabora.akishuhudia ni Mkurugenzi wa mradi huo Dr Gerso Nyadzi na wafanyakazi wengine wa mradi huo

Meneja Huduma za Jamii wa Aitel Tanzanaia- Hawa Bayumi akikabidhi SIM card 240 za mtandao huo kwa Meneja Mkuu wa Mradi wa Millenium Village ulioko Mkoani Tabora- Dr Gerson Nyadzi. Mradi huu unalenga katika kuboresha huduma za afya na elimu vijijini kupitia technolojia ya mawasiliano. Kulia ni afisa mauzo wa Airtel kanda ya ziwa Charles Elisante, na Meneja wa Airtel money kanda ya ziwa Violet Gyumi. Hafla ya makabidhiano ilifanyika mkoani Tabora

Bharti Airtel yasaidia kuondoa umaskini  kupitia mradi wa Millenium Village

*         Mradi huo kutoa  elimu kwa wafanyakazi wa afya kwa kupitia huduma za mawasiliano

*         Yawawezesha wafanyakazi 240 kuwasiliana kwa gharama nafuu za pekee.

*         Airtel unasaidiana na  mradi huu wa millennium village katika nchi 6 za Afrika



Dar es Salaam Juni 04 2013: Kampuni ya Bharti ("Airtel") inayoongoza kwa kutoa huduma za mawasiliano inayoendesha shughuli zake katika ndani ya nchi 20 barani Afrika na Asia, leo imethihirisha thamira yake ya kufikia malengo ya Millenium kwa kushirikiana na kampuni ya Erickson katika mradi maalum ujulikanao kama Millenum village inayoendeshwa katika nchi 6 za Afrika ikiweko Tanzania.

Mradi huo umeundwa na taasisi ya Earth Institute kwa dhamira ya kutimiza baadhi ya malengo ya Milenia kwa kuelekeza ufumbuzi wa kiubunifu zaidi katika maeneo ya vijijini huku ikishirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni ya simu za mkononi Airtel barani Afrika Airtel imesaidia mradi wa millennium village katika mkoa wa Tabora kwa kutoa huduma za mawasiliano zitakazowawezesha watu kupata elimu kuhusu maswala ya afya kwa urahisi. Airtel imetoa namba ya dharura itakayopigwa bila kutozwa gharama yoyote na kuwawezesha watoa huduma za afya  na wagonjwa kuwasiliana kiurahisi zaidi.

Mradi wa millennium Vilage unasaidiwa na Airtel katika nchi 6 ambazo Airtel inafanya biashara zake. Nchini Tanzania mradi wa millinium village umeanzishwa katika eneo la Mbola mkoani Tabora na kusambaa katika maeneo mengi na kufikia  zaidi ya vijiji 20 vilivyopo katika eneo lenye mita za mraba 700msq likiwa na wakazi 30,0000 waishio katika wilaya ya Uyui Tabora.

Mpaka sasa mradi huu umekuwa na mafanikio makubwa, zaidi ya watu 500,000 katika nchi 11 zilizoko kusini mwa jagwa la sahara Afrika wamefaidika ambapo hadi kufikia mwisho wa mwaka 2011 asiliimia 90 ya vijiji vilikuwa vimesha unganishwa na mtandao wa simu Vile vile ndani ya mradi huu kuna kipengele cha Connect to Learn, chenye ushirikiano baina ya  Earth Institute Chuo kikuu cha Columbia , Ericsson and Bharti Airtel Africa, ulioanzishwa  katika shule zilizopo ndani ya mradi wa millennium village  na kuwafikia walimu na wanafunzi zaidi ya 5,000 katika nchi za Ghana, Tanzania, Uganda  na Kenya.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Airtel Tanzania Bwana Sunil Colaso alisema" Airtel  ina dhamira ya kugusa maisha ya watu si tu kwa kutoa huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu lakini pia kuwazifikia jamii  za  chini zenye uhitaji wa technologia katika kuendeleza na kukuza maisha yao, ambayo ndio lengo lililotufanya kushirikiana na Earth Institute pamoja na  Erickson kusaidia mradi huu wa millennium village.

Ushirikiano huu unatupelekea kufikia malengo ya mradi wa millennium village ya kushughulikia changamoto za umasikini katika maeneo mengi ikiwemo Kilimo, elimu, afya, miundo mbinu, usawa katika jinsia na kukua kwa  Biashara. Tunafurahi kuwa sehemu ya mabadiliko na tunaahidi kuisaidia jamii nchini Tanzania.

Akiongea wakati wa halfa ya kupanua mradi wa millennium village katika kijiji cha Mbola mkoani Tabora, Meneja Huduma Jamii wa Airtel bi Hawa Bayumi alisema" tunafurahi kuendelea kutimiza dhamira yetu ya kutoa huduma za mawasiliano zenye gharama nafuu katika  vijiji mbalimbali Tanzania .

leo tunaonyesha kwa vitendo dhamira yetu na  kuwapatia wafanyakazi 240 huduma za mawasiliano ili kuuendesha  mradi huu wa millennium village kirahisi.  Airtel pia imetoa namba ya dharura ambayo itaboresha upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo huduma za dharura na elimu ya afya katika kijiji cha Mbola"

"Huduma ya mawasiliano tuliyoitoa kwa wafanyakazi 240 ni pamoja na kupigiana simu kwa gharama nafuu zaidi (CUG), ujumbe mfupi wa bure pamoja na huduma ya internet ilikuwezesha mawasiliano kati yao na jamii" aliongeza Bayumi

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha huduma kwa jamii katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa jangwa la Sahara Bi Margaret Kositany, alisema" ni imani yetu kwamba kwa kuboresha mawasiliano kutawezesha kuleta ufanisi katika huduma zetu za afya na kufanya mawasiliano ya karibu kati ya wauguzi na wagonjwa kuwa ya rahisi, kutoa elimu kwa jamii  kupita mitandao  na kuongeza uelewa wa elimu kwa njia ya mtandao kwa watoto wa shule."


Mbali na  mradi wa  Millennium Villages , Airtel Tanzania iko mstari wa mbele katika kusaidia shule za secondari nchini kwa kuwapati nyenzo za kufundishia ikiwemo vitabu. Tangu kuanzishwa kwa  mradi wa  'Airtel Shule Yetu'  zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na kupata vitabu kutoka Airtel.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.