ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 16, 2013

MKIMBIAJI MKENYA ASIMULIA HOFU MILIPUKO BOSTON


Korir alishinda mbio za Boston Marathon mwaka 2012.


Mshindi wa mbio za mwaka 2012 za Boston Marathon, Wesley Korir, aliyemaliza wa tano mwaka huu, ameambia BBC kuhusu hofu yake pindi aliposikia milipuko miwili iliyotokea Boston Marekani.
Milipuko hiyo ilitokea karibu na msitari wa mwisho wa kumalizia mbio hizo na kuwajeruhi takriban watu 140 takriban saa mbili baada ya mshindi kumaliza mbio hizo.

Alikuwa akisherehekea ushindi wa mkenya Rita Jeptoo katika mbio za wanawake.''Ikiwa shambulio hilo lingetokea saa mbili kabla ya mbio kumalizika labda ningekuwa miongoni mwa waliojeruhiwa,'' alisema bwana Korir.
"furaha yetu ni kuwa tulikuwa tayari tumeondoka katika eneo hilo,'' Korir aliambia BBC.
Bi Jeptoo anatoka katika eneo bunge la Cherangany, ambalo bwana Korir ni mbunge wake baada ya kushinda katika uchaguzi uliofanyika mwezi jana.
Licha ya milipuko hiyo pamoja na jukumu lake la kisiasa, Korir amesema kuwa ataendelea kushindana katika mbio za marathon hata ikiwa Boston itaandaa mbio zengine mwaka ujao.
Rais Barack Obama emesema wahusika lazima
watasakwa na kuchukuliwa hatua kali
.

Korir alisema kuwa aliogopa sana aliposikia kuhusu habari ya milipuko.
Alisema kuwa punde tu baada ya kusikia habari hiyo aliwapigia simu wakwe zake kuwajulia hali kwani walikuwa wamemtembelea pamoja na kocha wake.
Balozi wa Kenya nchini Marekani amesema kuwa hana taarifa zozote kuhusu wakenya waliojeruhiwa kwenye mashambulizi hayo.
Raia wawili wa Afrika Kusini walitibiwa baada ya kupata majeraha
Lelisa Desisa, wa Ethiopia alishinda mbio za wanaume mbele ya mshindani wake Micah Kogo.
Mbio hizo mwaka huu zilikuwa na wanariadha 23,000 na zilitazamwa na mamia ya mashabiki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.