ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 6, 2013

BOTSWANA YAAHIDI KUFANYA KAZI NA IBF/AFRICA


Rais Ngowi akihutubia katika mkutano na waandishi wa  habari katika ukumbi wa BNSC
Serikali ya Botswana imeahidi kushirikiana na Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika program yake ya “Utalii wa Michezo” na kuifanya nchi hiyo kuwa moja ya mataifa yanayong’ara kwenye medani ya masumbwi katika bara la Afrika. Ahadi hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Michezo la Botswana bwana Persy Raditladi alipofanya mazungumzo na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi katika ofisi za BNSC leo.
Rais Ngowi akiwa amesimama na Mkurugenzi
Mtendaji wa BNSC bwana Persy 
 Raditladi

Rais Ngowi yuko nchini Botswana kuutangaza mkanda wa ubingwa wa ngumi wa kimataifa ambao utashindaniwa tarehe 5 July nchini Namibia kati ya  bondia  wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia kutoka Namibia Immanuel Naidjala. Wawili hao walitoka sare katika mpambano wa kukata na shoka wa kugombania mkanda huo tarehe 20 Machi mwaka huu katika jiji la Windhoek, nchini Namibia.

Serikali ya Botswana imeahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa programu ya “Utalii wa Micheazo ya IBF” inanufaisha nchi hii yenye vivutio kadhaa vya kitalii likiwamo bonde la maarufu la “Okavango Delta”

Katika mazungumzo yao Rais Ngowi alieleza jinsi IBF inavyozinufaisha nchi ambazo zimeingia katika programu hii na namna mabondia wanaotoka katika nchi hizi wanavyonufaika na viwango vya kimataifa vya IBF. Ngowi aliielezea Botswana kama nchi yenye neema ya vipaji vya mabondia wazuri wa ridhaa na kuwashauri kuwa waweke mikakati ya mabondia wa ridhaa wanavyoweza kujiunga na ngumni za kulipwa ili waweze kufaika na vipaji vyao.

Nchi ya Botswana ni moja kati ya nchi zenye mabondia wazuri katika ngumi za ridhaa lakini kumekuweko na pengo la kuwaendeleza wanapofikia kustaafu na kutokuwa na uwazi wa namna ya kujiunga na ngumi za kulipwa. Ujio wa Rais wa IBF Afrika nchini Botswana umefanyika wakati nchi hii inapokabiliwa na sintofahamu juu ya kuwaendeleza mabondia wake wanapostaafu ngumi za ridhaa.

Mazungumzo ya Rais Ngowi na serikali ya Botswana yalitanguliwa na mkutano wa waandishi wa habari pamoja na wadau kadhaa wa ngumi za kulipwa uliofanyika katika ukumbi wa BNSC jijini Gaborone Botswana leo. Katika mkutano huo Rasi Ngowi aliuonyesha mkanda wa IBF wa kimataifa katika uzito wa bantam utakaoshindaniwa kati ya bondia wa Botswana Lesley Sekotswe na bondia kutoka Namibia Immanuel Naidjala tarehe 5 July mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.

Rais Ngowi aliwahakikishia wadau wa ngumi wa Botswana kuwa IBF itafanya kila liwezalo kuhakikisha kuwa Botswana imejenga msingi mzuri wa ngumi za kulipwa na kutumia vipaji vilivyonavyo katika ngumi za ridhaa. Rais Ngowi aliondoka leo kwenda nchini Afrika ya Kusini ambako atakutana na wadau wa ngumi na kutangaza mapambano kadhaa ya IBF yanayotarajiwa kufanyika nchini humo kuanzia mwezi ujao! 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.