ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 29, 2013

STORY...


MWANDISHI: NEEMA JOSEPH

Ukweli utabaki palepale  kwamba afya bora ni muhimu  kwa binadamu kuliko kitu  kingine chochote hapa duniani. Siku zote binadamu anapo ishi duniani kila kukicha anategemea  awe mzima ndipo atakapoendelea na  shuguli zake kwa sababu mtu hawezi kupanga mipango ya kesho kama mwilini  kwake  kuna maradhi.

Ilikuwa ni jioni   ambapo nilipiga  kambi  katika nyumba ya  Cosmas   Bonifance, mzee  ambaye   anaishi  na wake wawili  na kwa  wakati  huo alikuwa  kwa bi  mkubwa  akiwa  ameenda  kiumtembelea na kumpelekea matumzi .

hapo  ndipo  mzee  huyo alipoanza mazungumzo name kwa kuniambia  ushiriki wake  kikamilifu  katika  huduma  ya  ushiriki wa  uzazi  wa afya   kwa  familia  yake  yenye  wake wawili, kwa ujumla  mzee Cosmas amekiri   kushiriki  kikamilifu  kwenye  huduma ya  uzazi wa afya  baada  ya  kupata  elimu  na kuhudhuria  semina  mbalimbali tofauti  na hapo  awali.
Kwa sasa  anakwenda  kliniki  na mkeo  na kushiriki  hatua  zote  za  tangu  mwenza wake  anapoanza  kuhudhuria  kliniki  hadi  anapojifungua  ikiwa na pamoja na kupima  vipimo  vinavyohitajika wakati mama  akiwa mjamzito.

“Kabla  ya  kupewa  elimu  ya ushiriki  wa huduma  ya uzazi   ya   afya    mke  wangu  hakuthubutu  kuniambia  juu  ya  ushiriki  wangu  wakati wa ujauzito wake  na hata  mila  na desturi za kabila  letu  la wasukuma  hazikuruhusu  mwanaume  kushirikishwa  kwenye  afya  ya  uzazi” alisema   bwana  Cosmas.

Kwa hivi  sasa bwana  Cosmas  anaishi na wake zake wawili   na amekuwa akishiriki vyema  katika huduma ya  afya  ya uzazi  kwa wote  licha ya mke wake  mkubwa   aliyemtaja  kwa jina la  luncy  Magesa kutokuwa na  mtoto  kutokana  na kila anaposhika  mimba, mimba uharibika lakini  yeye amekuwa mshiriki wa karibu  katika  kufahamu  chanzo cha  tatizo  hilo.

 Sheria ya masuala ya uzazi na ushiriki wa   mwanaume  inasisitiza   mwanaume  kushiriki katika    huduma  ya  afya  ya   uzazi  kikamlifu  lakini wanaume  wengi   hawaijui  sheria  hiyo  hali  inayosababisha  ugumu wa kuwaomba waajiri wao  ruksa  ya  kumsindikiza  mke/wake  kliniki  na   baadhi yao wanaoijua wansingizia  kuwa wananyimwa  ruksa  na waajiri wao kuwasindikiza wake zao.

Lengo  la  tano  la millennia  linasisitiza  kupunguza  vifo  vya  kinamama wajawazito  kwa  robo  tatu  ya   vifo  kati ya mwaka 1990  hadi  2015  sanjali  na  lengo  la  sita  la kukinga  maambukizi  ya virusi  vya  ukimwi, malaria  na magonjwa  mengineyo.
Sera  ya  afya   ya Tanzania  ya  mwaka 2003  iliyosainiwa na waziri wa afya  wakati  hulo Anna  Magreth  Abdallah  moja  ya  lengo  lake kati  ya  malengo  tisa  ni kupunguza  maradhi  kwa  wakina mama wajawazito  na watoto  na kuongeza  umri wa kuishi.

Takwimu za  shirika la chakula duniani (FAO) zinaonyesha kuwa  wanawake huzalisha asilimia 60 na 80 ya chakula chote katika nchi zinazoendelea.wanawake  wanatoa mchango mkubwa  kama wazalishaji wakuu wa chakula katika ngazi za familia hatua ambayo imeanza kutambuliwa na kudhaminiwa na vikao mbalimbali kitaifa na kimataifa.

Serikali kushirikiana na vyama visivyo vya kiserikali(NGOS) imefanya kazi  ya kuondoa vipengele vinavyo bagua sheria zinazotumika ambazo hazitoi haki  na uhuru wa wanawake ,Aidha, serikali imepitisha sheria kadha katika kutoa upendeleo  kwa mwanamke mfano”sexual offences special provision Act of 1998, land law Act of 1999, na village land Act1999.

Sheria ya kwanza itawalinda  wanawake, wasichana na watoto kutokana na kunyanyaswa  kijinsia na  kutendewa  matendo mabaya .katika maeneo mbali mbali, mathalani mkoa wa Arusha, familia nyingi uimara wake umewezeshwa  na wanawake, ambao  ndio walezi  na wenye kutafuta kipato kwaajili ya kutunza familia.

Ushiriki  wa  wanaume katika swala zima la  afya ya uzazi mkoa  wa  mwanza umeongezeka kwa  asilimia 24 kwa mwaka  2011 haya yamebainishwa na katibu mkuu wa  mkoa  hospitali ya seketure mwanza Bw,  Danni  temba.

Mara nyingi  wanawake  wamekuwa wahanga wa  tabia , mila,  na  desturi  zenye  athari  katika  afya  ya  uzazi  kama ukeketaji  kwa  wanawake, kudhalilishwa  kingono ,   unyanyasaji wa kijinsia, ukahaba,  kulazimishwa   kuolewa   a u  kuoa  mapema  na  utumiaji  wa  madawa  ya  kulevya.

Wanaume  waache  kuwanyanyapaa   wenza    wao,   ubepari,   mila,  na  desturi walizo nazo waziiache, afya ya mama mjamzito ni muhimu kuliko kitu kingine chochote  duniani, hinyo  wanaume wadhubutu   kwani     nia,  uwezo  na  nguvu  wanazo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.