ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 12, 2013

MSAADA WAKO UNAHITAJIKA ILIKUWEZA KUOKOA UHAI WA MTOTO SIMON MLOPE


Hivi ndivyo hali ya mtoto Simon Mlope ilivo kwa sasa.

Angalia Video ya  mtoto Simoni Mlope akiwa na Mama yake. 

Mtoto Simon Mlope akiwa na mama yake ambaye anaitwa Amina Ally.

Simon Mlope akijaribu kutembea kwa shida
Taarifa na Demasho news.
 Mtoto simon Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la mahenge katika manispaa ya songea mkoani Ruvuma amelazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa darasa kwanza  kutokana na mototo huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo .
Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake. Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya .

 Mtoto simon Mlope alikubwa na ugonjwa  moyo  tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa  moyo wake una tundu hali ambayo inasababisha  kuvuta pumzi kwa shida.
Mama wa mototo  simon mlope anayeitwa AMINA ALLY  anawaomba watanzania kumsaidia mtoto  wake fedha za matibabu Baada ya kuambiwa na madaktari kuwa simon anatakiwa kwenda nchini  india kutibiwa,baada ya kupata rufaa kutoka muhimbili mwaka 2006  huku familia yake ikiwa haina uwezo kabisa.

Majirani wa familia ya simon nao wanasema kuwa mototo simon anahitaji msaada wa haraka kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania wamsaidie.
Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo  anayejulikana kwa jina la SIMON MLOPE  ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.
Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia  SIMONI MLOPE  atumie simu namba  0752732290

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.