ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 28, 2013

LOWASSA MGENI RASMI JUMAPILI HII KATIKA PASAKA GOSPEL FESTIVAL JIJINI MWANZA

Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa akiwa na Meneja wa COSU Entertainment Albert G. Sengo. 
Waziri Mkuu Mstaafu ambaye ni Mbunge wa jimbo la Monduli Mh. Edward Lowassa amethibitisha kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha kubwa la muziki wa Injili lijulikanalo kama Pasaka Gospel Festival litakalo fanyika pasaka hii tarehe 31 march 2013, na kujumuisha waimbaji mbalimbali kutoka mikoa tofauti hapa nchini ikiwa ni pamoja na kwaya zaidi ya 15 za jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa COSU Entertainment Phabian Fanuel (kushoto) akifafanua jambo ndani ya studio za Afya Radio kuhusu tamasha la Pasaka Gospel Festival litakalofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza tarehe 31/march 2013 ambapo mgeni rasmi anatazamiwa kuwa Waziri  Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli Mh. Edward Lowassa.  Kulia ni mtangazaji wa Xtra Vaganza Mr. Credit.

Si wageni hao tu bali atakuwepo pia Meya wa jiji la Mwanza Mh. Stanslaus Mabula na wengine wengi waalikwa, hivyo wakazi wa Mwanza watashuhudia burudani ililoandaliwa kwa ubunifu wa hali ya juu ikishirikisha waimbaji wakubwa kama Enock Jonas (ZUNGUKA), na Neema Mwaipopo (RAHA JIPE MWENYEWE).

Wengine ni Nesta Sanga (JIANDAENI), Danni Safari, John Shahban, Jeska Julius, Isaya Msangi (SHETANI IMEKULA KWAKO), Danny Sanga kutoka Iringa, Tumaini Mbembela  kutoka Mbeya na mkoa wa Arusha utawakilishwa na Neema Munisi.

Kwaya za mkoa wa Mwanza ni nyingi za kutosha Anglican Vijana kwaya, EAGT City Centre kiufupi kwa zote zitaweka kambi kwenye shughuli yetu ya Uzinduzi Pasaka hii.

Jumatatu ya pasaka tutakuwa Geita uwanja wa CCM Katoro
Kiingilio kwa maeneo yote kitakuwa ni shilingi. 2000/= tu
Hivyo tunawakaribisha wote kwenye uzinduzi huo.

Mkurugenzi wa COSU Entertainment Phabian Fanuel amesema kuwa hii imekuwa ni bahati ya kipekee kuweza kuweza kufikia hatua hii na ugeni huo mzito kwani maandalizi yote yamekwisha kamilika kwa asilimia 97 jambo la kumshukuru Mungu.


Kulia ni mtangazaji wa Xtra Vaganza Mr. Credit na kushoto anaonekana Dj. Sande.
Njooni tuzunguke kwani wema wa Mungu umetuzunguka. 


Ili ufanikiwe tizama na sikiliza wimbo huu 'UFANIKIWE'

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.