ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 6, 2013

FORUM SYD YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KONGAMANO JIJINI MWANZA

Meneja wa nchi wa shirika la Kiswidi Forum Syd bwana Godfrey Wawa akizungumza wakati wa ufunguzi kwenye mkutano  wa akinamama uliofanyika leo Monarch Hotel jijini Mwanza ukiwa na lengo la kujadili changamoto wanazokutana nazo akina mama katika harakati za maisha ya kila siku vilevile kutambua umuhimu wa wanawake katika maendeleo ya jamii.

Afisa habari wa Forum Syd Tanzania Bi. Emma Mashauri akitoa maelezo juu ya  mikakati iliyowekwa kufanikisha maadhimisho hayo.

Forum Syd imekuwa ikifanya kazi nchini Tanzania tangu mwaka 1982 ikilenga katika kuchochea maendeleo endelevu, haki na kuzingatiwa kwa sheria, pamoja na kupunguza umasikini.

Kongamano hili limekuja likihusisha na akina baba pia kwa nia ya kutoa elimu ikiwa ni safari kuelekea siku ya Maadhimisho ya akinamama duniani tarehe 8/03/2013

Mkufunzi kutoka Chuo Cha SAUT akiwasilisha mada kwa wanakongamano ilizipate kujadiliwa kwa kina ikiwa ni pamoja na kutolewa ufafanuzi na maamuzi.

Wadau mbalimbali kutoka ndani ya jamii na mashirika ya huduma za kutetea haki na kuzuia ukatili kama vile shirika la kijamii la KIVULINI, wamehudhuria kongamano hili la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke duniani lililofanyika Monarch Hotel Mwanza.

Kwa utulivu na umakini akinamama wakisikiliza yanayojiri ndani ya kongamano hili la Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke duniani lililofanyika ukumbi mkubwa wa mikutano Monarch Hotel jijini Mwanza.

Sehemu ya wahudhuriaji.

Shirika la Forum Syd lilipata ufadhili kutoka Sida-Tanzania kutekeleza mradi wa Uwajibikaji Jamii nchini Tanzania,mradi ukilenga vijiji na kata za wilaya za karagwe, Magu na Ukerewe ukiwana lengo la kusaidia na kuimarisha jitihada za wadau wa maendeleo kwa kuwajengea uwezo kwa njia ya mafunzo mbalimbali.

Umakini zaidi kusanyikoni.

Burudani nayo ilipata nafasi.

Kula burudani ya Kadogoli ambayo ilitumbuiza. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.