ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 28, 2013

BIG RIGHT YAWEKA MIKAKATI YA UBINGWA


Big Right YAWEKA MIKAKATI YA UBINGWA

Kampuni  changa ya Bigright Promotion inaanzisha mkakati wa kuwapiganisha mabondia  kwa ajili ya kugombania mikanda au kutetea mikanda yao isipotee.
Ibrahim kamwe kiongozi wa kampuni hiyo alisema ” Tutaanzia kwa kuandaa ubingwa wa mapambano ya uzito mdogo kabisa yaani light fly weight,baadae tunawaandalia fly weight na super fly  ,bantam …. .. ..mpaka heavy weight.
Hiyo itawasaidia mabondia kupata mapambano ya mara kwa mara na kuwapatia kipato kidogo kwa ajira walioichagua inayoambatana na utambulishaji wa kimataifa kwa nchi yetu, kwani mchezo wa ngumi ni mchezo  mmojawapo unaoutangaza na kuipeperusha vema bendera ya nchi yetu kimataifa.
Bila ya watanzania wengi kulifahamu hilo, hivyo kukosa usaidizi mzuri toka serikalini na taasisi binafsi tofauti na baadhi ya nchi za wenzetu zinazopenda na kuithamini michezo, Nchi nyingi zinatangazika  kupitia michezo hadi sisi tunazifahamu na kuzitembelea  au kuwa na shauku ya kutaka kuzitembelea, wakati uwezo huo wa kufanya vizuri  tunao lakini hatusaidiwi kujinyanyua wala kuwa na sehemu ya kueleweka kwamba hii ni kwa ajili ya ngumi (ulingo wa kisasa na ukumbi wa uhakika), na wakati wadau wa mchezo huu tunanung`unika na kuhaha kutafuta wadhamini  nasi tujikwamue tokakatika hali tuliyonayo, kuna wengine wasio wastaarabu watataka kuchukua nafasi hii kufanya ubadhilifu dhidi ya wanaosaidia-hii sio njema  na inadumaza michezo.
Kwa mfano mashindano yaliyo andaliwa na bigright tarehe 7 april mwananyamala hayana udhamini wala ufadhili wowote hivyo yanaendeshwa katika hali ya ugumu ili vijana nao wapate kucheza kuliko kufanya mazoezi ya muda mrefu bila mashindano hivyo kuwasababisha baadhi ya mabondia kukata tamaa na kuacha ngumi au kijiingiza katika vitendo vya ukabaji jambo ambalo sio jema na laweza kuepukika kwa kuwaandalia mashindano kama haya.
Ili azma yetu ya kuyafanya michezo iendelee yatubidi tushirikiane kwa kushawishi wafadhili, wadhamini au wapenda mchezo wenye uwezo watuwezeshe japo kidogo walichonacho ili nasi tuongeze nguvu ya kupigania michezo isidorole,  mipango ikienda kama tulivyopanga tunategemea kila mwezi kuwashindanisha kugombania ubingwa na kila mwezi wa 12 kunakuwa na ligi ya mabingwa na kumzawadia mshindi  kitu ambacho atakuwa anakikumbuka katika maisha yake.
Hivyo  kwa alie tayari na mwenye mapenzi na maendeleo ya michezo tunaomba mchango wako uwe wa vifaa kama gloves, bandages, ballguard, headguard, gumshield, chakula ,nauli, ulingo na mengineyo mengi tu sijayaorodhesha,msitutenge na uwezo wetu mdogo tusaidiane
 
IBRAHIM ABBAS KAMWE
+255 713501991 ,+255 784501991 , +255 767501991

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.