ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 11, 2013

AMSHA AMSHA YA KUELEKEA PASAKA ILIVYOKUWA JANA KATIKA ENEO LA BUHONGWA

Ni Amshaamsha ya pasaka, na hii  ni safari ya kuziandaa kwaya mbalimbali za jijini Mwanza kuelekea sikuu ya Pasaka ambapo COSU Entertainment wanataraji kuzindua studio za kurekodi muziki sambamba na video hapa ilikuwa katika eneo la viwanja vya michezo Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza.


Kwaya zinajinoa vilivyo kwa style kalikali viwanjani hapa sambamba na kuongeza ubunifu.


Shughuli imenoga kwa kwaya kuvalia sare zao maridadi tena za kupendeza, tukio limekuwa kama mashindano vile ya kwaya, kumbe laa hasha... ni maandalizi tu! kuelekea tarehe 31/03/2013 sikukuu ya Pasaka ambapo Enock Jonas anayetamba na wimbo 'ZUNGUKA' sambamba na Neema Mwaipopo anayetamba na wimbo wa 'RAHA JIPE MWENYEWE'  na waimbaji wengine toka mikoa mbalimbali hapa nchini watashuka CCM kirumba kuwasha moto wa injili kwa njia ya uimbaji.


Nao watu hawakukubali kupitwa na Amsha amsha hii ya kuelekea tarehe 31/03/2013 sikukuu ya Pasaka.
Nyang'omango


Macho kwenye Amsha amsha ya Pasaka.


Vikundi mbalimbali na ustaarabu wao.


Waimbaji wa moja ya kwaya wenyeji hapa Buhongwa.


Sound 'cheki' 


Pozi.... 


Akinamama na watoto wao wakiyawajibisha macho.


Kwa uhuru na amani viwanjani hapa.


Hapo vipi?




Vijana wa Mungu kazini....


Muacheni Mungu aitwe Mungu haya ni maandalizi tu katika 'Amsha amsha ya Pasaka', shughuli kamili itakayokuwa na kishindo kikuu ni siku ya tarehe 31/03/2013 CCM Kirumba kwa kiingilio cha shilingi 2000/= tu!


Burudani imenoga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.