ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 1, 2013

WAZIRI WA UCHUKUZI DR.HARSON MWAKYEMBE AMALIZA MZOZO WA KIVUKO CHA SAMMAR III AGIZA KIENDELEE KUTOA HUDUMA ENEO LILILOPO AFUTA AGIZO LA PTA.

Hali ilivyokuwa hii leo mara baada ya kivuko hicho kurejea kazini.
 WAZIRI wa Uchukuzi Dkt..Harrison Mwakyembe ameagiza kivuko cha Mv.Sammar III kiendelee kutoa huduma ya usafiri  ndani ya  eneo la Bandari ya Mwanza Kaskazini linalomilikiwa na Mamlaka ya Bandari nchini PTA.


Agizo hilo la Waziri Mwakyembe limefuta uamuzi wa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari PTA nchini na kumaliza utata wa jambo hilo uliokuwa umezua sitofahamu na hata kutofautiana na agizo la Kamati ya Ulinzi na Usalama la Mkoa wa Mwanza la kukiruhusu Kivuko cha Sammar III kuendelea kutoa huduma katika eneo hilo la Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini Jijini Mwanza.

 Hatua hiyo inafuatia agizo la barua iliyotolewa kutoka kwa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari (PTA) waliyomwandikia na kumkabidhi Mwekezaji na Mkurugenzi wa Kivuko cha MV.Sammar III  Salum Ally yenye kumbukumbu  NaMN/2/3/04 ya Januari 29 mwaka huu iliyosainiwa na Kaimu Mkuu wa Bandari (PTA) Mwanza Richard Msechu,ambapo ilieleza kwamba agizo hilo limetoka na Wizara ya Uchukuzi.

Agizo hilo lilionekana kupingana na lile la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza lililoridhia Kivuko hicho cha MV.Sammar III kuendelee kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na magari kati ya Mwanza na Kamanga Wilayani Sengerema ndani ya eneo la Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini baada ya tamko la awali la Naibu Waziri wa Uchukuzi Dr.Charles Tizeba alilolitoa Desemba 9 mwaka 2012 la kutaka Mamlaka hiyo imuondoe eneo hilo na kumhamishia sehemu nyingine.
Mbunge mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Fortunatus Masha (UDP)
 Baada ya taarifa za kuruhusiwa kuendelea na shughuli za kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na magari, mamia ya wananchi na baadhi ya abiria wanaotumia kivuko cha Sammar III wakiongozwa na Mbunge mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Fortunatus Masha (UDP) alisema kwamba uamuzi huo ni bubusara na ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wengine katika kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia masilahi ya umma.


Aidha alipongeza uamuzi wa Waziri Dr. Mwakyembe umeonyesha kuwa ni mungwana na mtu anayejali sana na hata pengine kuondoa kero za wananchi na kuwajali zaidi badala ya kuangalia masilahi binafisi kama ilivyo kwa viongozi wengine ambao husababisha hata wananchi kuwachukia na kuilaumu serikali yao iliyopo madarakani.


Wananchi wa Jiji la Mwanza na Kamanga Wilaya ya Sengerema leo asubuhi wamedhuru eneo la kamanga wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti ya kuwapongeza Waziri Dkt.Mwakyembe, Mkuu wa Mkoa Injinia Ndikilo na Kamati yake na Mbunge wa Jimbo la Sengerema William Ngeleja kwa kusimamia na kuondosha kero hiyo kwa kukiruhusu Kivuko cha Sammar III  kuendelea kutoa huduma ya usafiri. 


Mwenyekiti akizungumza kushukuru sakata hilo kumalizika...
Mama Ester ambaye ni mfanyabiashara ya chakula eneo hilo aliwakilisha akina mama kuzungumzia kumalizika kwa sakata hilo.. 
Akina mamalishe nashughuli zao za kipato eneo la Kamanga upande wa Sengerema leo wameendelea na shughuli zao kama kawaida mara baada ya kusitisha zoezi hilo kwa muda wa siku kadhaa wakati kivuko hicho kikiwa kwenye katazo.

 Wananchi wa Kamanga Wilaya ya Sengerema na bango lao.

Mkurugenzi wa Kivuko cha Sammar III, Salum Ally

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kivuko cha Sammar III, Salum Ally alisema kwamba anaupokea uamuzi huo wa Waziri kwa mikono miwili, kwa vile ni uamuzi ambao umezingatia kero na adha ambayo wangelipata wananchi lakini pia naye kama mwekezaji kwakuwa alitumia gharama kubwa kuwekeza ikiwemo miundombinu ya eneo la kivuko pande zote mbili Mwanza na Kamanga.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.