ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 1, 2013

ROYAL OVEN WAGUSWA NA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MWANZA

Uongozi wa kampuni ya Royal Trinity ambao wanamiiki kampuni ya Royal Oven ambao ni waokaji wa mikate jijini Mwanza wakiingia katika lango kuu la kituo cha watoto waishio katika mazingira magumu cha Upendo Daima kilichopo Lumala jijini Mwanza, kwaajili ya kutoa mchango wao wa chakula mara baada ya kuguswa na maisha waishio watoto wa kituo hicho.


Mkurugenzi wa Royal Oven ya jijini Mwanza Mwanabure Mberea akikabidhi madaftari kwaajili ya watoto hao waishio katika mazingira magumu cha Upendo Daima kilichopo Lumala jijini Mwanza, ambapo sambamba na kampuni hiyo kutoa vifaa vya elimu pia kampuni hiyo ilitoa mchango wa chakula ikiwa ni mara baada ya kuguswa na maisha waishio watoto wa kituo hicho.


Mkurugenzi wa Royal Oven ya jijini Mwanza Mwanabure Mberea akimkabidhi mikate na vitafunwa vingine mtoto Isack Lucas kwa niaba ya watoto wote wa kituo cha Upendo Daima kilichopo Lumala wilayani Ilemela jijini Mwanza.

Kampuni yauokaji mikate ya Royal Oven iliyopo barabara ya Posta ikitizamana na New Mwanza Hotel pia ilikabidhi vyakula vingine kama Mchele, Unga na Mafuta.
Ekzaud Kiwali akiongea na watoto wa kituo cha Upendo Daima kilichopo Lumala wilayani Ilemela jijini Mwanza. Msikilize Bofya Play..


Uongozi wa juu wa kampuni ya Royal Oven pia walipata fursa ya kutembezwa idara mbalimbali za maeneo ya nyumba waishio watoto hao kama sehemu ya ukaguzi kuona changamoto zilizopo. 


Mratibu mkuu wa kituo cha Upendo Daima Benson Nyasebwa akiongoza ujio wa wakurugenzi wa Kampuni ya Uokaji Mikate ya Royal oven kuingia kwenye darasa la kituo hicho kama sehemu ya ukaguzi kujionea changamoto zilizopo kituoni hapo.


Mratibu mkuu wa kituo cha Upendo Daima Benson Nyasebwa akitoa ufafanuzi kwa Wakurugenzi wa Kampuni ya Uokaji Mikate ya Royal Oven mara baada ya kuingia kwenye darasa la kituo hicho kama sehemu ya ukaguzi kujionea changamoto zilizopo kituoni hapo


Hii ni  moja kati ya sehemu mbili zilizopo kituoni hapa kwa ajili ya kulia chakula ikitumika pia kama maktaba ya kujisomea kituo cha Upendo Daima


Mkurugenzi wa Royal Oven ya jijini Mwanza Mwanabure Mberea akifurahia matandiko ya watoto wa kituo cha Upendo Daima, kituo ambacho kinaongozwa kwa misingi ya kumjua Mungu (chekshia matandiko)


Mratibu mkuu wa kituo cha Upendo Daima Benson Nyasebwa (wapili kutoka kulia) akitoa ufafanuzi kwa Wakurugenzi wa Royal Trinity mara baada ya kuingia kwenye moja ya vyumba vya kulala watoto waishio katika mazingira magumu kilichopo Lumala jijini Mwanza, kutoka kushoto ni Mwanabure Mberea, Leonard Shayo na Ekzaud Kiwali ambao wote ni Wakurugenzi kampuni ya Royal Trinity.

Msikilize Bofya Play..


Royal Oven pia ilipata picha ya pamoja na watoto hao na walezi wao.
Mkurugenzi wa Royal Trinity Bw. Leonard Shayo akipata pix na  madaktari  wetu wa kesho. Msikilize Bofya Play..


Hisia zinaanzia lango la chumba cha kulala.


Royal Trinity wameamua kutoa msaada kwa kituo hicho ikiwa ili kuungana na makampuni mengine na watanzania wanaoguswa, walio mstari wa mbele kusaidia kuwezesha vituo vya watoto waishio mazingira magumu kuwa na tabasamu, na pia wakiunga mkono kauli za wadau wengine wanaoamini kuwa watoto hawa ni wetu sote.


Meneja wa Royal Trinity ambao ni wamiliki wa kampuni ya uokaji mikate ya Royal Oven, Bi. Carolyne Mhando akifunga lango la kituo cha Upendo Daima ikiwa ni ishara ya kuondoka eneo hilo la kituo na makaribisho ya karibu tena.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.