ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 16, 2013

MICHEZO MWANZA YAPATA MWARUBAINI



Mkuu wa Mkoa wa mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo akisikiliza kwa makini Michango ya Wajumbe wa Kamati ya Michezo Mkoa walipokutana kujadili maendeleo.

Meneja wa TRA Mkoa wa Mwanza (kushoto) pamoja na Bw. Kizito Bahati Afisa Michezo wilaya ya Ilemela aliyemwakilisha Mkurugenzi wa wilaya hiyo wakiwa kwenye kikao hicho kilichofanyika ukumbi wa mikutano ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha soka mkoa wa Mwanza MZFA Bw. Jackson Songora ambaye ni mmoja kati ya wajumbe wa kamati hiyo akichangia hoja iliyowasilishwa mezani. 

Wajumbe wakitafakari kwa makini huku wakiainisha kwenye karatasi zao maoni yao namna ya kuinua michezo mkoa wa Mwanza.

 · Zachangwa Mil. 6 Papo kwa Papo

Na. Atley Kuni -Afisa Habari Mkoa wa Mwanza.

Kamati ya Michezo Iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,  imeazimia kuhakikisha inainua suala zima la Michezo katika Mkoa huo.
Wakitoa mawazo katika kikao kilicho itishwa na Mkuu wa Mkoa huo  walisema tatizo kubwa ambalo lipo katika Masuala ya Michezo ni pamoja na nidhamu ndogo ya michango kwa Viongozi wanao chaguliwa,

Walisema kukwama kwa michezo katika Mkoa nia tatizo la watu wanaochaguliwa kutokuwa na dhamira ya dhati katika kuendeleza michezo Mkoani hapa.

Akizungumza katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo amesema, "kwakweli tufike mahali tumalize tatizo hili lakukwamisha suala la michezo katika Mkoa huu". Alisema haipendezi watu kugeuza uongozi kama sehemu ya Miradi yao badala yake tufanye kazi ambayo itakuwa na maslahi kwa wanamwanza wote.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Mwanza bwana Hamisi Maulid alisema tatizo lililopo ni Umbwe la uongozi usio zingati maadili ya uongozi hivyo Umefika wakati sasa kamati kama hii inayo undwa kusimamia kwa dhati na ikiwezekana viongozi wanaochaguliwa wawe ni wale tu wenye dhamira ya dhati katika kuinua Michezo katika Mkoa huu, akitolea mfano alisema huko yeye alipotoka waliunnda kamati kama hiyo na usimamizi wa fedha ukaimarishwa tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Hata hivyo kamati hiyo ilitoka na Maazimio Manane yakwenda kuyafanyia kazi, Maazimio yaliofikiwa ni pamoja, kila halmashauri ya Wilaya kuchangia, Mil.10, Uchaguzi wa vilabu ambao bado haujafanyika ufanyike ikiwezekana hata kwakulazimishwa, Kamati ya Michezo ya Mkoa kuwa Mhimili Mkuu wa kusimamia masuala ya michezo, kufungua akaunti kwaajili ya kuhifadhi pesa itakayokuwa inapatikana, kutunga sheria ndogondogo kwaajili kukusanya sehemu ya kodi ya leseni kwaajili yakuendeleza michezo mkoani humo, Aidha kila mjumbe wa kamati hiyo amehimizwa kuwa chachu ya mabadiliko yakuhakikisha suala la Michezo katika Mkoa huo linarejea kama enzi za zamani.

Katika hatua nyingine kamati hiyo Imewachagua Bibi Doroth Mwanyika kuwa Mwenyeki wa Kamati hiyo, huku bwana Peter Ngongoseke akichaguliwa kuwa Makamu wa Mwenyekiti, huku nafasi ya Mtunza fedha ikienda kwa bwana Peter Shewio ambaye ni mfanya kazi wa Mamlaka ya Mapato nchini TRA.

Kabla ya kikao hicho kumalizika wajumbe hao walikusanya kiasi cha Tshs 6,000,000 kwaajili yakuanziasha mfuko huo na wadau wengine waka ahidi kuendelea kuchangia mfuko huo.

 Kamati ya Michezo ya Mkoa wa Mwanza inaundwa na Mkuu wa Mkoa Mwenyewe kama Mlezi, Bibi Dorothy Mwanyika Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza Mwenyekiti, Peter Ngongoseke Makamu wa Mwenyekiti,  wajumbe ni Ernest Mangu, Christopher Gachuma,Altaf Hilani, Nuru Suleiman, Jeremiah Lusana wajumbe, wengine ni Leonard Kadashi Mjumbe, L. Japhet,Wilson Kabwe,Zuberi Mbyana Jackson Songora, Gisiruri Mwihechi, Baraka Ezekiel, Njile Lili, Samwel Nyala wote wajumbe, taarifa hiyo Imeongeza kuwa wajumbe wengine ni James William, Lameck Airo, Joseph Kahungwa, Lazaro Ngweleja, na Hamis Salehe wote wajumbe.

Kwa mujibu wa historia Mkoa wa Mwanza uliwahi kuwika katika Michezo katika vipindi tofauti kati ya miaka ya sabibi na Themanini, lakini pia Mwanza ndio Mkoa pekee wenye chuo kikubwa kabisa cha Michezo cha Malya.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.