ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 23, 2013

KUNDI LA SANAA LA THE GREAT ZONE ENTERTAINMENT LATEMBELEA TBL MWANZA

Kundi la Great Zone lililosheheni vipaji mbalimbali katika picha ya pamoja na Afisa Bia Ubora Kwenye soko wa Kampuni ya TBL Mwanza Mr. kamambi ambaye aliwatembeza kiwandani hapo kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Hapa ni ndani ya eneo la uzalishaji ambapo kundi la sanaa la The Great Zone Entertainment lilipata fursa ya kutembelea kujionea yaliyomo na yanayojiri. 

Dirisha la kuelekea eneo jingine la chemba ya uzalishaji ndani ya kampuni ya Bia TBL Mwanza.

Haya ndiyo yanayosomeka toka dirishani hapo panapo chunguliwa.

Afisa Bia Ubora Kwenye soko wa Kampuni ya TBL Mwanza Mr. kamambi akitoa maelekezo juu ya shughuli nzima ya uzalishaji kiwandani hapo kwa wasanii wa kundi la The Great zone Entertainment.

Viambatanisho elekezi vilivyo muhimu kwa ajili ya uzalishaji bora na makini viko kwenye eneo la ufungaji bia.

Umakini unazingatiwa  kuanzia ndani ya kiwanda hivyo ufungaji si wa vizibo pekee bali hata upachikaji lebo makini unapewa kipaumbele. 

Afisa Bia Ubora Kwenye soko wa Kampuni ya TBL Mwanza Mr. kamambi akitoa maelekezo katika seksheni ya ugongaji vizibo.

Sasa bia imekamilika na inapakiwa kwenye gari kuelekea kwenye soko.

Wasanii walipata fursa pia kutembelea ghala ya kuhifadhi bia zilizo kamilika kuelekea sokoni.

Wasanii wa The Great Zone wakipata flash eneo la ghala kabla ya kwenda kupata vinywaji na chakula walichoandaliwa..

Wadau wa TBL Mwanza wakiburudika mara baada ya kazi ndani ya bar iliyoko ndani ya kiwanda hicho eneo la Bwiru wilayani Ilemela.

Picha na kinywaji vya TBL.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.