ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 16, 2013

JIJI LA MWANZA KUSAINI UPYA HATI YA URAFIKI NA JIJI LA HUSBERG


 Ujumbe wa watu watano ukiongozwa na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula hivi karibuni ulifanya ziara katika jiji rafiki na Mwanza la Augsburg nchini Ujerumani.

Ziara hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa baada ya jiji hilo rafiki na jiji la Mwanza kusaidia vifaa vya utendaji kazi pamoja na mitambo ya kuboresha miundombinu kwa ajili ya shughuli za usafi wa jiji la Mwanza.
Katika ziara hiyo jiji hilo la Augsburg ambalo ndani ya kipindi cha mwezi wa April litakwenda kuadhimisha miaka yake 50 tangu lilipotunukiwa hadhi ya kuwa jiji, liliweza kuahidi ujumbe wa jiji la Mwanza, kuendeleza mahusiano kwa kusaini upya hati ya urafiki wa majiji siku ya kilele cha maadhimisho hayo mwezi April 2013.

Pamoja na kusaini hati mpya jiji hilo rafiki liliweza kutoa msaada kwa jiji la Mwanza wa magari mawili ya kisasa ya uzoaji taka pamoja na kompyuta 500,  kwa ajili ya kuboresha maktaba ya jiji na shule za Sekondari za jiji la Mwanza.

Jiji la Husberg limeahidi kugharamikia safari ya wajumbe watakao kwenda kuhudhuria sherehe hizo za kutimiza miaka 50,  ikiwemo shughuli ya kusaini mkataba mpya wa Urafiki, lakini pia jiji hilo litaendelea kusaidia jiji la Mwanza linalokuwa kwa kasi kimaendeleo ili kuboresha sekta mbalimbali za Afya, Miundombinu, Teknolojia,  Elimu  na Mawasiliano.

Wengine walikuwemo kwenye ziara hiyo ni pamoja na Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Bw. Wilson Kabwe, Afisa Uhusiano wa jiji la Mwanza Bw. Joseph Mlinzi pamoja na Mweka hazina wa jiji la Mwanza Bw. Paulo Ntinika na Afisa mmoja wa Kitengo cha Tampere.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.