ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 22, 2013

HATIMAYE MWANARIADHA MLEMAVU ANAYETUHUMUWA KWA MAUAJI YA MPENZI WAKE NCHINI AFRIKA YA KUSINI AACHIWA KWA DHAMANA


Jaji nchini Afrika Kusini hii leo wametoa dhamana mwanariadha mlemavu Oscar Pistorius, anayetuhumiwa kwa mauaji ya mchumba wake. 
Mwanariadha huyo alikanusha kosa la mauaji akisema kuwa alimpiga risasi Reeva Steenkamp akidhania kuwa alikuwa jambazi.
Pistorius amesema kuwa hakuua 
mchumba wake kwa maksudi. 
Pamoja na kwamba upande wa mashtaka awali ulikuwa na hofu kuwa huenda Pistorius angekosa kufika mahakamani kwa siku ya leo, Pistorius amejitokeza leo na hatimaye kuachiliwa kwa dhamana.Upande wa utetezi ulisema kuwa ushahidi huo wenye utata na uliotolewa na mmoja wa polisi umeweza kuhujumu upande wa mashtaka.
Mara baada ya kupewa dhamana Pistorius anatarajiwa kurejea katika mazoezi wiki ijayo.
Kocha wake aliyasema hayo alipowasili mahakamani kwa siku ya nne ya kusikiliza kesi ya dhamana dhidi ya Pistorius.
Mnamo Alhamisi polisi walimbadilisha jasusi aliyekuwa anachunguza kesi hiyo na kuweka polisi mwingine baada ya taarifa kujitokeza kuwa polisi huyo mwenyewe alikuwa anakabiliwa na kesi ya jaribio la mauaji.
Carl ambaye ni kaka wa Oscar pistorius akikumbatiana na
 baba yake mzazi mara baada ya maamuzi ya dhamana kwa 
mdogo wake. (Reuters)
Jasusi mkuu wa Afrika Kusini Luteni, Vineshkumar Moonoo, ndiye anachunguza kesi hiyo sasa.
Viongozi wa mashtaka wanasema kuwa Pistorius alifyatua risasi nne katika bafu yake iliyokuwa imefungwa huku marehemu Steenkamp akiwa ndani. Aligongwa kichwani , kwenye paja na mkononi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.