ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 2, 2013

WATU 61 WAFARIKI DUNIA NCHINI IVORY COAST SERIKALI YAANZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO

Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouatarra, akitoka hospitalini ambako amewatembelea baadhi ya wale waliojeruhiwa na kusema kuwa kutakuwa na uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ambacho alikitaja kuwa mkasa wa kitaifa.

Wakati huo huo serikali ya Ivory Coast imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya zaidi ya watu sitini kuuwawa na wengine wengi kujeruhiwa kwa kukanyagwa wakati wa onyesho la fataki kuukaribisha mwaka mpya katika mji mkuu wa Abidjan.
Hali ndani ya hospitali wakati rais wa Ivory Coast, Alassane Ouatarra, alipokwenda kutembelea baadhi ya wale waliojeruhiwa na kusema kuwa kutakuwa na uchunguzi kuhusiana na kisa hicho ambacho alikitaja kuwa mkasa wa kitaifa

Maafisa wanasema wengi wa waathiriwa waliokufa ni vijana na kuna ripoti za kutatanisha kuhusu kilichosababisha maafa hayo karibu na uwanja wa michezo uliopo mjini Abidjan.

Baadhi ya wale walioshuhudia kisa hicho wanasema watu waliingiwa na wasiwasi baada ya vijana waliokuwa wamejihami kwa visu kuanza kuiba simu za mkononi huku wengine wakisema ni utepetevu wa maafisa wa usalama katika kuthibiti umati.
Viatu na nguo vimezagaa eneo lote la uwanja. 

Afisa usalama wa nchini humo akiwa nje ya eneo la uwanja wa mpira palipotokea msongamano uliosababisha mauaji hayo pembeni nguo na viatu vikiwa vimezagaa. 

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. These are fundamentally brief term loans that do deliver you
    meet your fiscal matters inside a preferred precise time period.

    Taking into consideration time limitations these loans are particularly
    made above an obligation free platform. As such, these are kept entirely
    totally free from credential checksums. Challenges
    such as defaults, arrears, bankruptcy, CCJs and even IVAs are not viewed as
    here. Additional, there are also no collaterals related with these loans.
    There is minimal paper operate needed on the part of borrower.
    There are also no hidden or added documentation or faxing expected here.
    Applying for these loans is also especially hassle-free.
    Consumers merely require filling an on line form and as soon as this
    gets approved cash is received inside 24 hours time frame.
    These loans are typically provided beneath handy terms and situations.
    The common simple applicant criteria right here is
    that they should certainly be a UK resident and of 18 years of age.
    Here is my weblog - http://www.arizonalocals.com/index.php?do=/profile-12798/info/

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.