ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 4, 2013

MWANZA YAMPOTEZA MMOJA KATI YA WANAHABARI WAKE.

Tasnia ya habari jijini Mwanza imempoteza mmoja kati ya wanachama wake ni marehemu Winnifrida H. Kabambo (Hellen) aliyefariki dunia mnamo tarehe 2 mwezi januari 2013,  amezikwa leo kwenye makaburi Lumala yaliyoko wilayani Ilemela jijini Mwanza, marehemu alikuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Radio Living Water Fm Mwanza.

Mwili wa marehemu ukiwasili eneo la makaburi ya Lumala.

Mwili wa marehemu Hellen Kabambo ukishushwa kwenye nyumba yake ya milele.

Ni baadhi ya waandishi wa habari Mwanza wakisaini kwenye daftari la rambirambi kutoka kushoto ni Jackline, na Rose Jackob.

Mwenyekiti wa Mwanza Press Club (MPC) Deus Bugahirwa akiweka mchanga kwenye kaburi la marehemu Hellen Kabambo aliyezikwaleo kwenye makaburi Nyasaka yaliyoko wilayani Ilemela Mwanza, marehemu alikuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Living Water Fm Mwanza.

Jeneza lenye mwili wa marehemu Hellen Kabambo likiwa kwenye nyumba yake ya milele tayari kwa kufukiwa mavumbini.

Mkurugenzi wa Chuo cha Victoria Institute Of Tourism and Hotel Management Bw. Geleta. (mwenye suti nyeusi katikati)  akishiriki zoezi la kufukiaudongo kwenye kaburi la aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo aliyezikwa leo jioni kwenye makaburi ya Lumala jijini Mwanza.

Mama wa marehemu akiwa ameambatana na watoto wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo Hellen Kabambo wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu.

Baba wakubwa wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu.


Waandishi wa habari wkiwakilisha vyombo mbalimbali vya habari wakiweka shada la maua kwenye kaburi la marehemu Hellen Kabambo wa Living Water Fm, kutoka kushoto ni Jacline (Mwananchi), Rose Jackob na Fabian Fanuel (Living Water Fm & Blogger wa F Plus) 

Ndugu wa marehemu, mama wa marehemu pamoja na watoto wa marehemu walijumuika pamoja kuwasha mishumaa katika tukio la kuhitimisha hatua ya kuupumzisha mwili wa aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo Winnifrida H. Kabambo.

Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye hali ya majonzi makaburini kumsindikiza aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha radio Living Water Fm marehemu Hellen Kabambo aliyezikwa leo jioni kwenye makaburi ya Lumala. 






Na mwanga wa milele na umwangazie.

Kutoka kulia ni Liberata Mashimba, Amina Mashimba, Pendo Martin na bibi Elizabeth Masabo.

MPC Team.

MPC Team.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.