ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 24, 2012

SAUT WAHITIMU HII LEO












Picha zote na Alan Kisoi.

Friday, November 23, 2012

RAIS WA ZAMANI WA UFARANSA AFIKISHWA MAHAKAMANI


Na Sabina Chrispine Nabigambo

Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amefikishwa mahakani na kusomewa mashtaka ya matumizi ya fedha zisizo halali katika kampeni za kuwania urais wa nchi hiyo mwaka 2007


Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy,
Sarkozy
Sarkozy ambaye amepoteza kinga ya kushtakiwa baada ya kuondoka madarakani mwezi mei na kiti chake kurithiwa na rais wa sasa Francois Hollande anakabiliwa na mashtaka dhidi ya matumizi ya fedha zisizo halali katika kampeni zake za urais wa mwaka 2007.

Sarkozy amefikishwa mahakamani akituhumiwa kupokea jumla ya euro laki moja na elfu hamsini 150,000 toka kwa mwanamke tajiri Liliane Bettencourt na kuzitumia katika kampeni zake.

Sambamba na hayo Sarkozy pia alikiuka sheria ya uchaguzi ya nchi hiyo ambayo kikomo cha matumizi ni euro 4600 pekee.

Rais huyo wa zamani aliwasili sambamba na mwanasheria wake Jean-Michel Gentil huku vyombo vya usalama vikiimarisha ulinzi.

Sarkozy amekanusha kuhusika na rushwa ya aina yoyote ile, hata hivyo kama atakutwa na mashtaka atakabiliwa na adhabu kama ilivyokuwa kwa Rais aliyemtangulia Jacques Chirac ambaye alihukumiwa kifungo alipotoka madarakani mwaka 2007 baada ya kukutwa na hatia ya kutokuwa mwaminifu na ubadhirifu.

Thursday, November 22, 2012

MKUU WA MKOA WA MWANZA AWAKABIDHI BENDERA YA TANZANIA KILIMANJARO STARS USIKU HUU

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo (R) akimkabidhi bendera ya Taifa Nahodha wa timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars Juma Kaseja kwenye hafla fupi iliyofanyika usiku huu ndani ya Hotel Lakairo jijini Mwanza tayari kwa safari kuelekea nchini Uganda michuano ya Chalenji inakayoanza kutimua vumbi 24 nov 2012 nchini humo, huku ikiwakosa wachezaji wake, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, Hata hivyo licha ya wachezaji hao kutowasili hadi jana, viongozi wa timu hiyo wanaamini kuwa wataungana na wachezaji hao. Katikati anaonekana kocha mkuu wa timu hiyo  Kim Poulsen.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akiwaasa wachezaji wa timu ya taifa Tanzania Bara Kilimanjaro Stars, ambapo kubwa zaidi kutoka kwake amewasisitiza  wachezaji hao kuweka fikra zote kwenye kila mchezo kwa dakika 90 pamoja na nidhamu ndani na nje ya uwanja.


Kilimanjaro Stars, inayonolewa na kocha wake Kim Poulsen, iliweka kambi jijini Mwanza kwa siku kadhaa, kabla ya kesho alfajiri kuondoka Mwanza na kuunganisha ndege katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Licha ya kocha mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen kuahidi mazuri kwa watanzania pia amesema kuwa morari itaongezeka kwenye timu yake iwapo Watanzania watajitokeza kwa wingi kuisapoti timu yao ya Taifa, katika michezo yake yote na kustaajabisha wenyeji kwa ubunifu namna ya ushangiliaji.


Meza kuu...


 Meya wa jiji la Mwanza (Nyamagana) Stanslaus Mabula (R) akiteta na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Henry Matata (L) kwenye hafla fupi iliyofanyika usiku huu ndani ya Hotel Lakairo jijini Mwanza tayari kwa safari kuelekea nchini Uganda michuano ya Chalenji inakayoanza kutimua vumbi 24 nov 2012 mjini Kampala.


Mkuu wa wilaya ya ilemela Bi. Amina Masenza (L) akiteta jambo na Katibu tawala wa Mkoa wa Mwanza (RAS) Bi. Doroth Mwanyika, kwenye hafla fupi iliyofanyika usiku huu ndani ya Hotel Lakairo jijini Mwanza tayari kwa safari kuelekea nchini Uganda michuano ya Chalenji inakayoanza kutimua vumbi 24 nov 2012 mjini Kampala.


Afisa habari wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mr. Kuni Atley (R) akiwa na kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars,  Kim Poulsen (L).


M-blogishaji maarufu wa The big top ten Muhksin Mambo (R) akiwa na kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars,  Kim Poulsen (L).


CEO wa Blogu hii Albert G. Sengo (R) akiwa na kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars,  Kim Poulsen (L).


Kila la kheri Kilimanjaro Stars. 

TANZANIA YASIFIWA KWA KUONGEZA UFANISI KATIKA BANDARI ZAKE

Mwakilishi wa Tanzania Phares Magesa akiwasilisha mada inayohusu mfumo mpya wa eSWS katika mkutano huo.

Ndugu Magesana washiriki wengine wakifuatilia majadiliano


Ndugu magesa akibadilishana mawazo na mshiriki wa mkutano huo kutoka Wizara ya viwanda na Biashara ndugu Manumbu.
Katika mkutano ulioandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshugulikia Uchumi Afrika (UNECA) uliokuwa unafanyika Moroni, Comoro 20-21 Novemba, 2012, Mkutano wenye lengo la kuendeleza biashara bila kutumia karatasi "Advancing Paperless Trade in Eastern Africa".

Tanzania ilisifiwa na wasemaji wengi wa mkutano huo kutokana na juhudi za kuimarisha miundombinu ya usafirishaji na kuongeza ufanisi katika bandari zake.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi wa serikali na wataalamu wa masuala ya usafirishaji na Teknolojia ya habari na mawasiliano(Tehama) kutoka nchi zote za Afrika Mashariki, Kati, Kusini na visiwa vyote vya bahari ya hindi.

Mmoja wa wachangiaji mada katika mkutano huo ndugu Hamidou M'Homa ambaye ni Rais wa Chama Cha watumiaji wa huduma Comoro, alisema kwa kipindi cha karibuni ameona ufanisi umeongezeka katika bandari za Tanzania na akatoa pongezi nyingi kwa jitihada zinazofanywa na serikali na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika kuboresha huduma.

Msemaji wa Tanzania katika mkutano huo Ndugu Phares Magesa alipokea salamu hizo za pongezi na kuelezea jitihada mbali mbali zinazofanywa na TPA na Serikali katika kuboresha huduma katika badari zetu. Moja ya jitihada hizo kwa upande wa Teknolojia ni kuanza matumizi ya mifumo ya kisasa ya kuhudumia mizigo na meli ambapo sasa watumiaji wa huduma za meli na mizigo wanaweza wakafanya kazi kutokea maofisini kwao badala wote kwena bandarini hivyo kupunguza msongamano bandarini na kurahisisha utuoaji huduma.

Jitihada nyingine ni Mamlaka kwa kushirikiana na wadau wote wa bandari kuamua kuharakisha ununuzi na ufungaji wa mfumo wa kisasa wa kutoa huduma zote za kibiashara ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini , mfumo huu unaitwa Tanzania Electronic Single Window System(eSWS), ndugu Magesa aliulezea kwa kirefu mfumo huu na jinsi utakavyorahisisha huduma za kibandari na kiforodha. Mfumo huu unatarajiwa kupunguza muda wa kukaa mizigo bandarini na kufikia siku 5 au chini ya hapo. 
Kwa sasa bandari zote chini ya jangwa la sahara ukiacha Durban ya Afrika Kusini, zinatumia zaidi ya siku 10 na zingine hadi 20. Hivyo basi kwa kuweka mfumo huu pamoja na jitihada nyingine za kuboresha miundombinu ya usafirishaji na utoaji huduma, Tanzania itafikia malengo yake katika miaka michache ijayo ya kufanya bandari ya Dar es Salaam kuwa moja ya bandari bora duniani na hii itachochea kukua kwa uchumi wa Tanzania na kuongeza mapato ya Serikali.

Nachukua nafasi hii kuwaomba wadau wote sasa watoe ushirikiano mzuri ili mifumo hii iweze kuleta tija na kutoa mrejesho chanya ili kuboresha huduma kwa faida ya nchi yetu na wananchi wote kwa jumla .

Phares Magesa.

NAMTAMBULISHA LADY ZHENA…..AWAPA SOMO WANAMUZIKI WA KIKE!!

Wapo wanamuziki wachache wa kike wanaopiga muziki wa kizazi kipya, kwa sasa, lakini kadri siku zinavyokwenda, wanaendelea kuibuka wanamuziki kadhaa wa kike ambao kwa hakika wanajitahidi kuziteka nyoyo za wapenzi wa muziki wa kizazi Kipya.

Mmoja wa wanamuziki hao ambaye ameamua kufunguka na kueleza ya moyoni mara baada ya kuingia rasmi katika tasnia hii ya muziki wa kizazi Kipya ni manamuziki Lady Zhena.

Lady Zhena anaeleza kinagaubaga kuwa ni vyema wanamuziki wa kike nchini kutambua kuwa wanapaswa kuwa na moyo wa uvumilivu nakutokata tamaa mapema kwani hakuna maendeleo ya ghafla na ya haraka.

Wanamuziki wa Kike wanapaswa kutilia maanani mazoezi na kujifunza mbini za muziki zitakazo wawezesha kutunga na kuimba kwa sauti tamu kama wanavyofanya wenzao wanong'ara hapa Afrika.

Anasema Inafaa pia kwa wanamuziki wetu wa kike Kuithamini kazi hiyo kwa kuiona kuwa sawa na zingine, tena isiyopaswa kuchezewa.

Isiwe tu wanapotoka stejini, basi wanajiona na kazi ndiyo imekwisha. Ni vyema pia kwa wanamuziki wa kike kujiheshimu wakati wote.

 Iwapo watajiheshimu wawapo kwenye muziki, ni rahisi pia kwao kuheshimika kwa mashabiki.

Lady Zhena amefunguka na kusema kuwa maendeleo ya wanamuziki wa kike na kung'ara kwao kimuziki kutaamsha hamasa kwa wanawake wengi wenye vipaji kujitokeza badala ya ilivyo hivi sasa ambapo wengi wanasita kwa kuiona fani hiyo ni ya kihuni.






Mwisho Lady Zhena, anaomba
Suport kwa watanzania waipokee kazi yake mpya na kuomba baraka za Watanzaniakuipokea kazi yake mpya na kuomba baraka zao, kwani bila wao yeye si mali kitu.

Single yake mpya aliyoitoa hivi karibuni katika Audio na Video amemshirikisha B-Baros imeanza kufanya vizuri kwenye radio na televisheni nyingi hapa nchini ikienda kwa jina 'Niliteleza' chini ya usimamizi wa Brabe Entertainment.




TUENDELEE KUMSAIDIA ANASTAZIA

*Pichani anaonekana Augustine Mgendi, akimkabidhi Mama wa binti anayeumwa Anastazia kiasi cha shilingi 10,000 fedha iliyotolewa na mama Abduweli wa Bandari ya Dar es Salaam, baada ya kukabidhi fedha hizo mama huyo alishukuru na kusema kuwa itasaidia kupiga Xray kwani hakuwa na kiasi cha shilingi 10,000 kupiga  X ray.

Jana Augustin Mgendi alituma habari na Picha za Anastazia binti anayesumbuliwa na uvimbe wa Mguu wa kushoto ambapo amekosa fedha za kupata angalau matibabu ya awali, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru wale wote walioonyesha kuguswa na habari hii na mpaka sasa kuna wengine wametuma na wemetoa ahadi ya kutoa fedha za kumsaidia Anastazia.

Mpaka sasa Mama Abduweli wa Mamlaka ya banadari Dar es Salaama mwenye namba 0713 689656 ametuma kiasi cha shilingi 10,000 huku dada Edna John kutoka Uingereza aliyesoma Blog ya Michuzi amesema atatuma fedha za kumsaidia Anastazia kwenye akaunti.

Hivyo basi watanzania tuendelee kumsaidia Annastazia ili aweze kurudi katika hali yake ya kawaida aungane na ndugu zake katika ujenzi wa familia yake,kama unamchango wowote unaweza kupitishia katika akaunti 022201093996 NBC au katika simu namba 0756 035 825

ASHANTI NOMA YATEMBEZA BAKORA KUMI KWA MORO UNITED



TIMU ya Ashanti United jana iliivurumisha bila huruma Moro United mabao 10-1 kwenye mchezo wa ligi daraja la kwanza uliochezwa uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulionekana dhahiri kuwa wa upande mmoja kutokana na wachezaji mahiri wa Moro United kutokuwepo, Ashanti walikwenda mapumziko wakiwa wanaongoza mabao 5-1.

Lambele Jerome 


Moro ambayo mlinda mlango wake alikuwa bonge la mtu alikuwa akijigararagaza kila wakati kwa madai akaumia.

Mabao ya Ashanti yalifungwa na  Lambele Jerome alifunga mabao sita dakika ya 35, 52, 71, 76, 81 na 89, Shabani Hatibu alifunga matatu dakika ya nane, 11 na 37, na Raju Mahmoud dakika ya 16.

Bao la Moro United lilifungwa kwa njia ya penalti  na Twahir Kiparamoto dakika ya 21.

Kwenye uwanja wa Mabatini mkoani Pwani Green Warriors na Polisi Dar es Salaam zilitoka sare ya kufungana bao 2-2.

Mabao ya Green Worriors yalifungwa na Said Asaa dakika ya 80  Edward Kheri dakika ya 89. 


 ZAIDI TEMBELEA http://pallangyor.blogspot.com/

MASAHIHISHO YA TAREHE ILIYOTOLEWA PICHA YA ONESMO NGOWI NA DAVID MIGEKE!


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
NOVEMBA 22, 2012
Masahihisho ya picha iliyotolewa na gazeti la Uhuru wakati bondia Onesmo Ngowi na David Migeke wakitia sahihi mkataba baina yao wa kupigana pambano lililofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar-Es-Salaam ni mwaka 1983 na sio 1987.

Onesmo Ngowi alimdunda David Migeke kwa KO raundi ya 2 (pili) katika mpambano ulioandaliwa na kampuni ya Safari Sound Promotions ya jijini Dar-Es-Salaam ambayo ilikuwa inamiliki bendi ya musiki ya Orchestra Safari Sound chini ya mfanyabiashara maarufu bwana Hugo Kisima wa jijiniDar-Es-Salaam.

Wafadhili wakuu wa mpambano huo walikuwa Tanzania Bottlers (Coca Cola), Tanzania Distilleries (Konyagi), Kamin Industries na Chibuku.

Baada ya mpambano huo ambao ulikuwa moja ya mapambano mengi ya ushindi kwa Onesmo Ngowi alipata nafasi ya kugombea mkanda mpya wa Afrika Mashariki na Kati jijini Nairobi Kenya akichuana na bondia wa Kenya aliyekuwa anapigana ngumi nchini Japan Modest Napunyi Odour, June 1983. Mpambano huo ndio ulioanzisha ngumi za kulipwa nchini Kenya na Uganda.

Ngowi alihamia Nairobi, Kenya Septemba 1983 na kuondoka mwaka mmoja baadaye Decemba 1984 na kuhamia barani Ulaya katika nchi ya Ugiriki ambako alicheza ngumi chini ya Kampuni ya bingwa wa mieleka Ulaya George Tromaras (Tromaras Sports Arena) na kustaafu mwaka 1988 akiwa ameshamia nchini Denmark!

Imetumwa na:
Onesmo Ngowi

IN EVERLASTING MEMORY



5th January 1937 – 22nd November 2006


Our beloved father, it seems like 22nd November 2006 was just like yesterday but it’s already six years since you depart from us to join our father in heaven.

We do not need a special day to bring you to our minds. The days we do not think of you are very hard to find. Each morning when we awake we know that you are gone. And no one knows the heartache as we try to carry on. Our hearts still ache with sadness and secret tears still flow. What it meant to lose you no one will ever know.

Our thoughts are always with you, your place no one can fill. In life we loved you dearly; in death we love you still. There will always to be heartache, and often a silent tear. But always a precious memory of the days when you were here.

If tears would make a staircase, and heartaches make a lane, we’d walk the path to heaven and bring you home again. We hold you close within our hearts; and there you will remain,
To walk with us throughout our lives until we meet again. Our family chain is broken now, and nothing seems the same, but as God calls us one by one, the chain will link again.

Missing you always and remembered by your Wife Vera, Children: Victor, Susan, Alex, Prosper, Francis, Colletha, Patrick, Kutina-Neema, Venancia and Suzi Mdogo. In laws: Sadock, Agapinus, Goodluck, Charles, Janet, Esther, Joyce and Neema. Grandchildren: Prince, CrispinI, Alex, Brian, Brenda, Sadock Jr, Vera, Hans, Kutina, Davis, CrispinII, Alma, Tax Jr, CrispinIII, Kenen JJ, David, Tonga, Trinity and Talia.
May the almighty God rest your soul in eternal peace, Amen.

Wednesday, November 21, 2012

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA ACHANGIA MATIBABU KWA MMOJA WA MACHINGA ALIYEJERUHIWA KWENYE VURUGU ZA HIVI KARIBUNI


MEYA wa Jiji la Mwanza Stanislaus Mabula, amemtembelea na kumjulia hali majeruhi Chacha Ryoba (29) mkazi wa mtaa wa Pamba Jijini Mwanza aliyepigwa risasi na kulazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando akipatiwa matibabu baada ya kutokea vurugu kati ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) na askari mgambo wa Jiji la Mwanza katika eneo la stendi ya zamani ya Tanganyika mwishoni mwa juma lililopita Wilayani Nyamagana Jijini hapa.

Hatua hiyo ya kumtembelea majeruhi huyo imekuja mara baada ya kijana huyo kuwa mhanga wa vurugu hizo.

Wa kwanza kulia ni mzee Ryoba (baba mzazi wa kijana Chacha), akisikiliza kauli ya Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula (shati jekundu) kwa kijana wake Chacha.  Pichani anaonekana pia  Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo jimbo la Nyamagana diwani wa kata ya Igoma Chagulani (shati la pinki).
Mstahiki Meya ameweza kumchangia gharama za matibabu kiasi cha shilingi laki mbili na nusu (250,000/=)  kijana Chacha ili kuwezesha kufanyiwa upasuaji katika mkono wake wa kulia  kuondolewa vipande vya mabaki ya risasi baada ya kujeruhiwa katika vurugu hizo ambapo mtu mmoja alikufa papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa akiwemo kijana huyo



Msikilize kijana Chacha Ryoba akisimulia kulichotokea vilevile na shukurani zake kwa Meya na rafiki zake. Bofya play.... 
Pia msafara wa Mstahiki meya ulimtembelea Bw. Juvenile Matagili (kushoto) ambaye ni mratibu wa Chama cha Umoja wa Wavuvi mkoani Mwanza (TAFU) ambaye anapatiwa matibabua ya mifupa kwenye hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Mazungumzo kabla ya kuondoka hospitalini.

KUTOA NI MOYO TUMSAIDIE MTANZANIA MWENZETU


Anaitwa Anastazia Dulianus miaka 18, ni mwenyeji wa Wilaya ya Serengenti mkoani Mara, amefika jana Hospital ya Mkoa lakini mpaka sasa hajapata huduma yoyote .

Mzazi wake wanatafuta fedha za kwenda kupima nyama ya Mguu wake KCMC Moshi, binti huyu anahitaji msaada wa kifedha hivyo atakayeguswa na mateso haya ayapatayo binti huyu afike wodi namba 4 Hospital ya Mkoa wa Mara
                                    
                            Au fanya mawasiliano kwa namba  0756 035 825
Katika kumsaidia Dada Anastazia tumia akaunti namba 022201093996 NBC
  Kutoa ni Moyo, tumsaidie Mtanzania mwenzetu

  Kutoa ni Moyo, tumsaidie Mtanzania mwenzetu

TAIFA STARS KUONDOKA KESHO KUELEKEA CECAFA UGANDA, MASHABIKI MWANZA WAJIPANGA KWENDA KUTIA HAMASA.

 Kocha Kim Poulsen amekiri kuwa Stars kuweka kambi yake jijini Mwanza hakika lilikuwa ni wazo sahihi kwani hamasa imeongeza  kwa wachezaji wake na hata walimu nao wanaahidi kuhakikisha wanacheza kufa na kupona kwenye michuano hiyo kwa nia ya kuiletea sifa nchi ya Tanzania. Haya yamejiri kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa kikosi chetu kinachoelekea Kampala nchini Uganda hapo kesho.


Mwakilishi wa Vilabu Mkoa wa Mwanza kwenye Mkutano Mkuu wa TFF Taifa Bw. John Kadutu (pichani mwenye miwani) licha ya kusema kuwa MZFA imejipanga kuhakikisha mpira Mkoa wa Mwanza unakua kwa kasi na kuzalisha wachezaji wengine kwa maslahi ya Timu za Taifa na vilabu mbalimbali pia alikuwa na nyongeza hii kwa mashabiki kuelekea nchini Uganda kushuhudia michuano ya CECAFA



Wachezaji a timu ya Taifa Tanzania bara pamoja na viongozi wakijadiliana na mastori kwenye hafla ya kuwaaga wachezaji wa kikosi kinachoelekea Kampala nchini Uganda hapo kesho..


Baadhi ya wachezaji wa Kilimanjaro Stars na viongozi wa soka Mwanza.


Hewa safi ya Hoteli Tilapia....na kuchati kwa chati....


Refreshment  kandokando ya ziwa Victoria


Fun 


Old is good..


Yes we are...


Bariz za hapa na pale....


Picha ya pamoja kati ya Kilimanjaro Stars na viongozi wa soka mkoa wa Mwanza MZFA

WAKATI huo huo chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA) kimewataka mashabiki wanaohitaji kwenda kuishangilia na kuipa hamasa timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars inayoshiriki michuano ya CECAFA Challenge Cup 2012 inayotaraji kuanza jumamosi ya Novemba 24 mwaka huu Jijini Kampala nchini Uganda kujitokeza kwa wingi na kuonana na uongozi wa MZFA kwaajili ya taratibu za safari.

Kwa mujibu wa Katibu wa MZFA Bw.Nasbu Mabourk amesema kuwa  maandalizi ya taratibu za kupeleka washabiki nchini Uganda kuishangilia Kilimanjaro stars katika kila mechi itakazocheza zimekwisha kamilika na kuahidi kutoa gharama halisi ya kwenda nchini humo siku ya ijumaa, ikiwa ni pamoja na ile ya hati ndogo ya kusafilia toka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Mwanza  zitakazoratibiwa na MZFA kwa ajili ya kuwarahisishia mashabiki na kuwaondolea usumbufu.