ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 13, 2012

RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAKANISA YALIYOHARIBIWA KATIKA VURUGU ZA WAISLAMU MBAGALA, ATOA POLE KWA WAUMINI, AWAHAKIKISHIA MKONO WA SHERIA KUWANASA WOTE WALIOHUSIKA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia uharibifu mkubwa ulkiofanywa katika kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Mchungaji Alkwin Mbawi uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye magari yaliyokuwa yameegeshwa ndani ya kanisa la Pentekoste la Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Bw. M Mkosimonga  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Ni  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hili.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa baadhi ya waumini wa  Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam kufuatia uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu

Ni  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hili.

Ni  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hili.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akioneshwa na Katibu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam Bw. M Mkosimonga  uharibifu mkubwa uliofanywa kwenye kanisa hilo huko  Mbagala jijini Dar es salaam wakati wa vurugu za Waislamu Ijumaa iliyopita kufuatia habari kuwa kuna mtoto amekojolea Msahafu
 PICHA ZOTE NA M. MICHUZI.

MKUU WA MKOA WAMWANZA AFUNGUKA ZAIDI JUU YA KIFO CHA KAMANDA WA POLISI MWANZA





Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa mwanza EVARIST NDIKILO amesema kuwa uchunguzi dhidi ya mauaji ya KAMANDA BARLOW tayari umeanza na kwamba polisi inamshikilia mwalimu DOROTHY MOSES ambaye alikuwa akipelekwa nyumbani  na kamanda huyo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza LIBERATUS BARLOW ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi usiku wa kuamkia jumamosi oktoba 13 mwaka huu katika eneo la kitangiri manispaa ya ilemela mkoani Mwanza.


Hili ndilo geti ambalo kifo cha Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza RPC Liberatus Barlow kilitokea usiku wa kuamkia leo wakati mwalimu Dorcas Moses alipokuwa akirudishwa nyumbani kupitia lifti ya Kamanda Barlow.


Taarifa ya Mkuu wa Mkoa inasema kuwa Kamanda Barlow alikuwa akitokea kwenye kikao cha Harusi ya ndugu yake aitwaye Sembeli Maleto kilichokuwa kikifanyika katika Hoteli ya Florida na kisha akampa lifti mwanamke aitwaye Dorcas Moses ambaye ni mwalimu ya  msingi Nyamagana maeneo ya barabara ya kona ya Bwiru kuelekea Kitangili.

Walipofika getini kwa Dorcas walijitokeza watu wawili waliokuwa wamevaa makoti ya Polisi Jamii, mama Dorcas akamwuliza Kamanda kama anawafahamu watu hao, naye bila shaka akasema kuwa hao ni vijana wa ulinzi jamii wako doria.

Sekunde chache baadaye vijana hao wakaongezeka na kuwa sita wakaanza kuzozana huku kamanda huyo akiwauliza kwani hamnijui mimi ni nani, wakiendelea kumtilia ngumu kutomfahamu na watu hao wakizidi kulizingira gari lake marehemu, kamanda Barlow akajaribu kuchukuwa radio call kuwasiliana na askari wake. 

Jamaa hao hawakumruhusu kamanda afanye mawasiliano kwani papo hapo walimfyatulia risasi kichwani iliyopelekea kifo chake.  

 Mwili wa marehemu LIBERATUS BARLOW umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Bugando kusubiri taratibu za mazishi.


PRIMETIMES PROMOTIONS WAWAPONGEZA WADHAMINI SERENGETI FIESTA 2012

Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa shukurani kwa Wadhamini wakuu waliofanikisha Serengeti Fiesta 2012 kufanyika na kumalizika kwa amani kwa mikoa takribani 12 nchini Tanzania ile hali tamasha hilo likiacha alama ya maendeleo na chembe za changamoto ya ukuzaji uchumi kwa wananchi wa mikoa iliyo kuwa kwenye ratiba. 

Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki bora kwa wadhamini wa mafuta vyombo vya barabarani GAPCO walioshiriki vyema Tamasha la Serengeti Fiesta 2012. 

Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akitoa Cheti cha Ushiriki Bora kwa wadhamini wakuu Kampuni ya bia SBL kupitia kinywaji mahsusi Tamasha la Serengeti Fiesta 2012, Serengeti Premium Lager walioshiriki vyema kufanikisha mpango mzima mwanzo mwisho. 

Kisha zikafuata shukurani za dhati kutoka kwa Mdhamini mkuu zilizotolewa na Mkurugenzi wa Masoko bia ya Serengeti Ephaim Mafuru.

Msanii mahiri mwenye mbwembwe za kila aina Juma Nature akimwimbia Mtangazaji wa kipindi cha Jahazi Wasiwasi Mwabulambo 'aaaah ... naye alicheza siutani' 

Top in Dar, You can call him TID naye alipata fursa kutoa shukurani zake katika usiku huo maalum wa marafiki kukutana ndani ya Escape Two.

Kwa upande wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Shettah amesema kuwa ujio wa tamasha hilo mwaka huu 2012 umetumika kuijenga sanaa yake sambamba na kumweka karibu na mashabiki wake ana uhakika kupata mialiko mingi ya kutosha kwani amekwisha jitangaza vya kutosha naye amejipanga kufanya show levo za kimataifa. 

Mwana FA kwa upande wake amesema hii ni miaka yake ya kusherehekea mafanikio kwa sanaa yake kushika hatamu akimshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumtunuku karama ya ubunifu wa mashairi, nyimbo za kueleweka pamoja na umiliki bora wa jukwaa na hadhira.

Tajiri wa Sauti aka Rich Mavoko na shukurani zake ndani ya Part Maalum la Shukurani lililoandaliwa na Primetimes Promotion kuwapongeza wadhamini wa Serengeti Fiesta 2012 nakufanyika Club Escape Two jijini Dar es salaam.

Hip hop thing'

Mchekeshaji maarufu nchini Tanzania toka kundi la Vuvuzela Entertainment,  Bukuku (katikati) akiwa na wadau.

The Crew.

Watu waliunyuka.....

Wawo....

Men....

Ni Dr. Isaack, Fid Q na mie.

Ze Crew...

Shine....
  
Producer wa Clouds Tv Mr. Mebb.

Dj Mayanga on the one and two.

Fun moment ni Madee, Chege, Morgan na Wasiwasi.
Good.

Wanyama....

Inshort kila kitu kili shine usiku wa jana...
Shukurani kwa Primetimes Promotion kwa kutukutanisha,
Serengeti Premium Lager, GAPCO, PEPSI na Precission Air kwa udhamini.

BONDIA THOMAS MASHALI NA MEDY SEBYALA WA UGANDA WAPIMA UZITO KWA AJILI YA MPAMBANO WAO KESHO JUMAPILI

Bondia THOMAS MASHALI kushoto akitunishiana misuri na MEDY SEBYALA wa UGANDA baada ya kupima uzito Dar es salaam leo kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika siku ya kumbukumbu ya baba wa Taifa katika pambano la Ubingwa wa Africa mashariki litakalofanyi ukumbi wa Friends corner hotel siku ya jumapili 14/10/2012a katika anaeshudia katikati ni Rais wa TPBC Onesmo Ngowi ambaye ndie msimamizi mkuu wa mpambano huo 


Bondia Jonas Segu akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia mpambano huo wa mabondia chipkizi umefuta isia za watu wengi kwa upande wa wapenzi wa mchezo wa masumbwi nchini.


Bondia Jonas Segu kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunishiana misuri baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika kesho.

Bondia MEDY SEBYALA wa UGANDA akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na THOMAS MASHALI litakalofanyika kesho katika ukumbi wa Friends corner hotel pambano la Ubingwa wa Africa masharikipicha na pambano la Ubingwa wa Africa mashariki picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

BREAKING NEWS YA USIKU HUU: KAMANDA WA POLISI MWANZA AUAWA

Marehemu Kamanda Liberetus Barlow (kulia) enzi za uhai wake akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza. 

Ilikuwa ni majira ya saa  8 usiku huu napata taarifa ambazo hatimaye zinathibitishwa kutoka kwa waugwana kuwa  Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Liberatus Barlow amefariki dunia kwa kupigwa risasi usiku huu maeneo ya hotel Tai 5, Kitangili jijini Mwanza .


Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alifariki kabla ya kufikishwa katika hospitali ya Bugando ambapo inadaiwa alivamiwa na watu takribani wanne waliokuwa wamevalia mavazi ya polisi jamii ndipo aliposimamishwa na baada ya kusimama watu hao walimmiminia risasi kufuani na kusababisha  kifo chake

Imeelezwa kwamba Marehemu Kamanda Liberatus Barlow alikuwa akitoka kwenye harusi na alikuwa na mtu mmoja
  kwenye gari aliyekuwa akimsindikiza mtu huyo ambaye ni mwanamke yeye hakudhurika na chochote katika tukio hilo.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.Eng. Evarist Ndikilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza ameshathibitisha kutokea kwa tukio hilo la kifo cha kamanda Liberatus Barlow.

Aidha taarifa zaidi kuhusu tukio hilo tutaendelea kuwajuza kwa kadri tutakavyozipata hapa


Friday, October 12, 2012

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MAJI MH ENG DK BINILITH MAHENGE WILAYA ZA MUSOMA NA BUTIAMA



Naibu waziri wa Maji Mh Dk Binilith Mahenge akiwa pamoja na DC Musoma Jackison Msome na mkurugenzi wa MUWASA Gines Kaduei

Sehemu ya mitambo ya maji

Naibu waziri wa Maji Mh Dk Binilith Mahenge akipewa maelezo na ufafanuzi juu ya mradi huo na mkurugenzi wa MUWASA Gines Kaduei
Chanzo cha maji cha Muwasa katika ziwa victoria ambacho kinahitajika kuhamishwa kwa gharama ya bilioni 41 kwaajili ya kuwezesha mji wa Musoma kupata maji ya uhakika

Sehemu ya mji wa Butiama

Viongozi wa wilaya ya Butiama wakiwa na naibu waziri wa maji wa kwanza kushoto ni Magina Magesa m/kiti wa halmashauri ya Musoma

Msafara.
Chanzo cha maji cha mradi wa Mugango,Kiabakari hadi Butiama

Maelezo kwa kina yalifanyika hapa.
 Bango la wafanyakazi wa maji Mugango/Butiama ambao wanaidai serikali miezi 26 hadi miaka mitatu


Sehemu ya mji wa Butiama

Naibu waziri wa maji akiangalia Bwawa la Kiarano