ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 28, 2012

YA WAZIRI MAIGE 'SHANGAA .... USISHANGAE'

Mjengo wenyewe.

Kipi hatari waliojenga mahekalu bila kukopa au walionunua kwa kukopa?
Usishangae asilimia kumi ya watu wanamiliki asilimia themanini ya uchumi wa dunia while the rest wanagombania makapi. Wakati kuna mtu ana struggle kwa mshahara wa laki mbili kuna mtu ananunua shati dola elfu moja na yuko Tanzania hii.

Kilo moja ya pamba ni shilingi mia tatu na hiyo kilo inaweza kutengeneza shati tano ambazo zikirudi Tz huuzwa kwa shilingi elfu hamsini mpaka laki nne kutegemeana na brands. Wakati wa Nyerere watu walitupa magunia ya hela lakini was it worth it?

Kama hizo hela wangeambiwa wajenge viwanda Tanzania hapa leo hii tungekuwa na akina Diallo wengi na ajira kibao kwa nchi na export kubwa. Kenya ya mabepari wakati huo wakiitwa manyang'au leo hii wanaweza kufinance budget yao kwa asilimia tisini na tano.

Sisi tuko wapi? Why Kenya? kwa sababu walijenga uwezo kwa wawekezaji wa ndani wakati sisi hata wale wasukuma waliohangaika au wachaga waliosota tuliwaweka rumande eti wahujumu na kutaifisha mali zao.

Leo hii nyumba za NHC wanakaa akina Pateli kwa kodi ya bure waswahili wako hoi huko mbagala and elsewhere.

Katika kupiga vita rushwa tuwe makini tusijikute tunasombwa na kimbunga cha mawazo hasi kwamba kila mtanzania anayepata basi kauza unga au kaiba au ni freemasons.
Hiyo ni hatari.

Copy & paste Kutoka kwa
fikra za mdau Rmg...2000

TUNDU LISSU ASIMAMIA MZIGO WAKE 'MWENYEWE' HADI USHINDI

Mbunge wa jimbo la Singida mashariki CHADEMA),Tundu Lissu,muda mfupi baada ya mahakama kuu kutupilia mbali maombi yaliyotolewa na Shaban Selema na Pascal Halu wa CCM,kupinga matokeo yaliyompa ushindi wa ubunge. Akitoa hukumu hiyo jana, Jaji Mosses Mzuna wa Makahama Kuu Kanda ya Moshi alisema ushahidi uliotolea na upande wa walalamikaji, umeshindwa kuthibitisha kuwa, walalamikiwa walivunja au kiuka sheria, taratibu na kanuni za uchaguzi na kusababisha uchaguzi huo kutokuwa huru na wa haki, hoja zote 11 zilizoletwa na walalamikaji, zimeonyesha ushahidi wa kuhisi,kusikia na kushuku, ambao hauna uhalisia wa mambo.


Wakili Msomo mleta maombi ya Wana CCM Godfrey Wasonga akitafakari kwa hisia kali muda mfupi kabla ya kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ubunge Tundu Lissu hayajatangazwa.


Tundu Lissu akifutwa machozi wakati wakitoka nje ya mahakama baada ya mahakama kuu kutangaza kuwa ushindi wake huo, ni halali.


Baadhi wa watu waliohudhuria kusikiliza kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi Tundu kuwa mbunge muda mfupi baada ya maamuzi hayo kutolewa ambapo kwa upande wa wao, walisema kuwa mahakama zinapaswa kuhakikisha kuwa hazibariki hoja ambazo zina mwelekeo wa kuwanyima haki wananchi viongozi wanaowataka.

Friday, April 27, 2012

MCHEZO WA AND 1 NA MWANZA ALL STARS WASHINDIKANA KISA BOGI (MVUA)

Kukosekana kwa viwanja vya ndani vimeligharimu jiji la Mwanza kukosa burudani ya Kimataifa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa mchezo wa basketbal waliofurika katika dimba la CCM Kirumba hii leo mara baada ya mvua kubwa kunyesha hali iliyopelekea hali ya uwanja kuwa tete.
Mwanza All Stars

Maiko Maluwe ni Kaimu katibu mkuu shirikisho la mpira wa kikapu Tanzania ambaye ameambatana na timu ya And 1 jijini Mwanza naye anaeleza sababu za katisho la mchezo huo... .

Huku mashabiki wa basketbal wa jiji hilo la miamba wakiwa na kiu ya kushuhudia maufundi ya wachezaji wa Mwanza All stars na wale wakali kutoka nchini marekani And 1, ilikuwa ni majira ya kumi mvua kubwa ilinyesha kwa muda mrefu hata kusababisha eneo la uwanja kuwa si salama kwa wachezaji.
Ground kabla ya bogi kushuka...
Wacheza mahiri wa timu ya mpira wa kikapu And 1 wakipasha misuli moto kabla ya mpambano.
Wachezaji wa And 1 wakijadiliana hatma ya mchezo wao mara baada ya hali ya hewa kuzingua dizaini.

"Yo men the rain is coming..."

Adam Mchovu na Reuben Ndege aka Ncha Kali (R) wakionyeshana maufundi.

Baba Joniii akipata flash na Blogu.

Wacheza wa And 1 wakishow love na mashabiki wao wa jiji la Mwanza.
Kiu haikuwa kwa mashabiki pekee bali pia kwa wachezaji wa nyumbani (Mwanza All Stars na hapa team captain Vicent Shinda anafunguka...

Yes we...

Mwanza All Stars katika mwonekano wa pili.

Mwanza All Stars na mashabiki wao wa nyumbani vizazi vijavyo katika game la kikapu, kiukweli Mwanza kama ni wachezaji wapo tatizo hakuna viwanja vya kutosha vilivyo rafiki kwa mchezo husika nikimaanisha visivyo tegemea mabadiliko ya hali ya hewa .

WAZIRI NAGU AFUNGUA KONGAMANO LA MAKATIBU MUHTASI LILILOFANA VILIVYO JIJINI MWANZA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu ameeleza kushangazwa kwake na hali mbaya ya umasikini unaowakumba Watanzania, huku taifa lao likiwa imejaa rasilimali nyingi zisizo na kifani.

Amesema, Tanzania ni nchi tajiri sana wa rasilimali, lakini wananchi wake bado wanakabiliwa na tatizo la umasikini, jambo ambalo amesema upo umuhimu zaidi wa uwezeshwaji wa wananchi, ili kuondoa tatizo hilo la umasikini katika ngazi ya kaya, mkoa hadi taifa.

Dk Nagu ameyasema hayo leo jijini Mwanza wakati akifungua Kongamano la siku mbili linaloratibiwa na TAPSEA lililo kutanisha Makatibu Muhtasi takribani 1500 wa mikoa mbalimbali nchini katika Hoteli ya Kimataifa ya Malaika iliyoko nje kidogo ya jiji la Mwanza.

Pi amewataka makatibu muhtasi nchini kupitia fursa na nguvu waliyonayo kuanzisha Sacos ili kujikwamua kutoka katika hali duni za maisha licha ya watumishi hao kuwa na changamoto kubwa ya viwango vidogo vya mishahara.

Hata hivyo, alikwenda mbali zaidi na kuwaonya Watanzania kwamba, wasibweteke na hali waliyo nayo sasa, bali wachangamkie fursa zilizopo nchini za uwekezaji, ili wasije wakabaki watazamaji tu katika sekta hiyo muhimu na mkombozi mkubwa wa umasikini.

Katika hatua nyingine, mkuu wa mkoa wa Mwanza Erenest Ndikiro amewashukuru wadau wote wa TAPSEA kwa kuichagua Mwanza kuwa sehemu ya kufanyia Kongamano hilo huku akiamini kuwa kupitia ugeni huo basi ni fursa tosha kwa mkoa kuzitangaza zaidi raslimali za utalii zilizopo kanda ya ziwa.

Huu ndiyo ukumbi ulio lihusu Kongamano.

Mc wa Kongamano Efraim Kibonde ilikuwa ni zaidi ya 'Jahazi'.

Mwenyekiti wa TAPSEA akihutubia.

Zawadi hiyoo kwa mlezi mweshimiwa Waziri Nagu.
Kuna kitu cha ziada juu ya uonekano mahali hapa.

Nilipendezwa sana na mavazi rasmi ya vitenge yaliyotumika kwenye kusanyiko hili.

Mblogishaji maarufu nchini Otman Michuzi wa 'Mtaa kwa mtaa' naye nikamnasa katika flash  na hapa akiniringishia kitu cha 7D.

KESHO TUKUTANE HAPA CCM KIRUMBA

Ni Hapa game litachezwa.
Ground nzima.
Kwa engo.
Kati.
Goli.

Thursday, April 26, 2012

BARUA YA SHUKURANI KWA WANA MWANZAKWANZA TOKA KWA MAMA WA MAREHEMU MSANII WA HIP HOP

Nibarua ya shukurani kwa wana Mwanzakwanza wote na wadau wote wanaojibidiisha kufanikisha maendeleo ya jiji la Mwanza, iliyopokelewa na Mwenyekiti wa Mwanzakwanza Philbert Kabago toka kwa mama mzazi wa msanii wa kizazi kipya Mwanza marehemu Mo Chella, aliyeuawa kwa kuchomwa kisu ubavuni katika tukio la kuamua ugomvi wa jirani yake mnamo mwezi januari 2012.

NDOA YA MR&MRS E.KIMORI YAADHIMISHA MIAKA5

Ladies and Gentlemen Leo tarehe 26/04/2012 Mr&Mrs Emmanuel Kimori wa Mwanza Tanzania wanasherehekea miaka mitano ya ndoa yao yenye furaha, mapendo na amani tele.

 Ndoa hiyo Takatifu ilifungwa katika kanisa la ST ALBAN POSTA jijini Dar es salaam kisha Sherehe za kufana zikafanyika HURBERT KILATO hall kimara stop over.

Blogu hii ya jamii inawatakia kila la kheri wawili hawa katika maisha yao ya ndoa MWENYEZI MUNGU awabariki.

AIRTEL YATOA MSAADA WA VITABU SHULE ZA SEKONDARI WILAYA YA KONDOA - DODOMA

Airtel yatoa msaada wa vitabu shule za secondari wilaya ya Kondoa- Dodoma Chini ya mpango wake wa shule yetu kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imetoa vitabu vya ziada na kiada kwa shule 4 za sekondari zilizoko wilaya ya kondoa mkoani Dodoma ili kusaidia maendeleo ya elimu wilayani hapo na katika kutoa huduma kwa jamii. Makabithiano hayo yalifanyika katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali na shule ya sekondari zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na sekondari ya Goma, Gubali,Itaswi na Hurui, zote za wilayani humo ambapo wawakilishi wa shule hizo walikabidhiwa vitabu vyenye thamani ya shilling milioni moja kwa kila shule. Afisa mauzo wa Airtel kanda ya kati bw Hillary Tarimo akimkabithi vitabu vya taaluma bw Leonard Cyprian Ngotta Mwalimu wa taaluma shule ya sekondari Hurui katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu imegawa vitabu kwa shule za sekondari nne ziliziko wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma, shule zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma, Gubali,Itaswi na Hurui, akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu mkuu wa shule ya Sekendari Gubali
Akiongea katika hafla ya makabithiano Afisa uhusiano wa Airtel T Afisa mauzo kanda ya kati bw Hillary Tarimo alisema" Airtel kwa kupitia programme ya shule yetu imeweza kuwafikia wanafunzi wengi na shule nyingi nchini Tanzania na leo tunafurahi kuwa sehemu ya maendeleo ya shule za sekondari wilayani Kondoa na kuweza kuchangia vitabu zitakavyotumika katika kufundishia na kuwa nyenzo muhimu kwa walimu na wanafunzi wa shule zitakazokabithiwa. Tutaendelea kushirikiana na Serikali chini ya Wizara ya Elimu katika kuinuia na kuboresha kiwango cha elimu nchini kwani tunatambua elimu ndio ufunguo wa maisha na vijana ndio nguvukazi ya kesho. Aliongeza
Tarimo.

Afisa mauzo wa Airtel kanda ya kati bw Hillary Tarimo akimkabithi vitabu vya taaluma bwana Ibrahim Juma Mwesi Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari Itaswi katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya Sekondari Gubali ambapo Airtel kupitia programme ya shule yetu imegawa vitabu kwa shule za sekondari nne ziliziko wilaya ya kondoab mkoa wa Dodoma, shule zilizopatiwa vitabu ni pamoja na Goma,Hurui, Gubali na Itaswi, akishuhudia katika ni Kessy Musilenga Kessy Makamu mkuu wa shule ya Sekendari Gubali
Naye Makamu mkuu wa shule ya sekondari Galibu Bw Kessy Musilenga alisema" nachukua fulsa hii kuwashukuru Airtel kwa kutufikia na kutoa msaada wa vitabu kwa shule zetu na kupunguza changamoto zilizokuwepo katika shule hizi, tunayofuraha kwa shule yetu na wenzetu wa shule za jirani zilizopo wilayani kondoa kupata nyenzo muhimu ambazo zitainua kiwango cha elimu kwa wakazi na wanafunzi wa wilayani" Tunawaasa wanafunzi kuvitumia vizuri vitabu hivyo ili vilete matokeo vizuri kwa wanafunzi, Tunaamini jamii ikipata elimu bora maendeleo ya shughuli mbalimbali za uchumi yatafanyika kwa ufanisi zaidi na kuleta mafanikio makubwa kwa jamii. Aliongeza Kessy.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kama vile Vitabu vya shule ya sekondari, siku chache zilizopita Airtel ilitoa msaada wa computer 20 na vitabu vyenye thamani ya million 10 kwa chuo kikuu cha Dodoma - UDOM hii ni katika kurudisha faida inayoipata na kuchangia katika huduma kwa jamii.

Wednesday, April 25, 2012

WAZIRI NAGU MGENI RASMI KONGAMANO LA MAKATIBU MUHTASI LITAKALOFANYIKA MALAIKA HOTEL MWANZA TRH 27 NA 28 APRIL 2012

Mwenyekiti wa TAPSEA Pilly Mpenda kulia akiongea leo na waandishi wa habari (hawapo pichani) anayefuata ni Mkuu wa Idara ya Uhazili TPSC Agatha Wanderage na Judith Nguli ambaye ni Mratibu wa Mafunzo ya Uhazili TPSC.
Chama cha Makatibu Muhtasi Nchini (Tanzania Personal Secretaries Association TAPSEA) kitaendesha kongamano la siku mbili katika Hotel ya Kimataifa ya Malaika, iliyo nje kidogo ya jiji la Mwanza tarehe 27 na 28 Aprili 2012.

Kongamano la jijini Mwanza ni la pili kuratibiwa na TAPSEA baada ya komngamano la Kwanza kufanyika Jijini Arusha, mwezi Mei, 2011, ambalo pia liliambatana na uzinduzi rasmi wa Chama.

Kongamano hilo linatarajia kuwakutanisha makatibu muhtasi zaidi ya 1,500 kutoka Wizara na Asasi za Serikali, Halmashauri na kampuni za kutoka sekta binafsi, kote nchini na linatarajiwa kufunguliwa Rasmi na Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji, Mhe. Dk. Mary Nagu (MB), ambaye ndiye ni muasisi wa wazo la kuunda chama hiki.

Lengo la kongamano hilo ni kuwakutanisha makatibu muhtasi kutoka kote nchini ili kuwapatia mafunzo ya kupanua uelewa wa masuala yanayohusu fani ya ukatibu muhtasi na namna fani hiyo inavyoweza kuboreshwa kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na mwingiliano ba maendeleo ya upashanaji habari yanayoletwa na utandawazi na teknolojia ya habari na mawasiliano.

Aidha, kongamano hilo linalenga kuwapatia makatibu muhtasi fursa ya kukumbushana kuhusu miiko na maadili ya fani ya uhazili na kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusiana na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Makatibu Muhtasi pia watawasilisha na kujadili ufumbuzi wa kero mbalimbali zinazowakabili katika utendaji kazi wao wa kila siku.

BAADHI YA MAFUNZO YATAKAYO TOLEWA
1. Katibu Muhtasi kama chachu ya mabadiliko katika utendaji wa utumishi wa Umma.
2. Ufahamu kuhusu ugonjwa wa Fistula, Athari zake na Matibabu yake.
3. Ufahamu kuhusu kansa za matiti na shingo ya kizazi.
4. Stadi za Mawasiliano na Mahusiano ya Umma kwa Makatibu muhtasi.
5. TAPSEA kama chombo cha Mabadiliko kwa Makatibu muhtasi.
6. Fursa Mbalimbali kwa Makatibu Muhtasi za kujiendeleza kitaaluma na kimaadili.

Wadhamini wa kongamano hilo ni Sahara Communication, Nyanza Bottlers, Serengeti Breweries, Mamlaka ya Bandari, Clouds FM, PSPF, NSSF, EWURA, Tanzania Private Sector Foundation, METRO, Barmedas, Gold Crest Hotel, Isamilo Lodge, Mukesh Travel, Dar Lux, Malaika Beach Resort, TAI FIVE HOTEL, MAC PHOTO SPOT, 540 na Precision Air.

CHEKA AJIFUA KUMKABILI MAUGO JUMAMOSI HII


Kocha wa mchezo wa Masumbwi Abdalah Ilamba 'Komandoo' akimfanyisha mazoezi ya kukaza misuli ya tumbo bondia Francis Cheka Dar es salaam jana. Cheka anajiandaa na mpambano wake na Mada Maugo unaosubiriwa kwa hamu na wengi utakaofanyika jumamosi hii katika ukumbi wa PTA Sabasaba ambapo mshindi atakuwa bingwa wa Mkanda wa I.B.F na atanyakua Zawadi ya gari.
Picha na www.superdboxingoach.blogspot.com

CHELSEA YAIVUA RASMI UBINGWA BARCA

Katika mchezo uliokwisha kwa sare ya 2-2, walikuwa ni Chelsea ndiyo walipata ushindi ikiwa na jumla ya magoli 3-2. The Blues (Chelsea) ilielemewa baada ya Sergio Busquets na Andres Iniesta kuiwezesha Barca kuongoza katika mechi hiyo, Lakini Ramires kwa ustadi aliuinua mpira juu na kuandikisha bao safi la Chelsea katika mechi hiyo.


Barca walipata penalty, lakini Lionel Messi, licha ya maarifa yake na sifa nyingi katika ufundi wa penalty, aliishia kugonga mwamba.


Wakati wa muda wa majeruhi wa dakika tatu zilizoongezwa, Fernando Torres alionyesha utulivu wa hali ya juu sio tu kwa kushambulia ngome ya Barca ambayo kwa muda mrefu ilikuwa haiguswi, lakini vile vile kwa kumchenga hata kipa Valdes na kuutia mpira wavuni kwa makini. Mapema wiki hii, Torres alikuwa amenukuliwa akisema “sio siku zote timu bora hupata ushindi”, matamshi ambayo ni ndoto iliyotimia.


Klabu ya soka ya Chelsea ya Uingereza imefuzu kuingia fainali ya klabu bingwa barani Ulaya, licha ya nahodha John Terry kuonyeshwa kadi nyekundu dakika za mapema, ikisubiri kufahamu kama itacheza na timu ya kocha wao wa zamani, Jose Mourinho, akiwa mkufunzi wa Real Madrid, au pengine watakutana na Bayern Munich, ambao uwanja wao ndio utakaotumiwa kuandaa fainali ya ligi ya klabu bingwa. Real Madrid na Bayern zinapambana leo jioni, tarehe 25 Aprili 2012.

Tuesday, April 24, 2012

BARCELONA V/S CHELSEA USIKU PATACHIMBIKA


Chiss Lugoe (L) and Reuben Ndege (R)

Chelsea take a 1-0 lead into tonight's semi-final second leg at Barcelona, but know only winning the trophy might be enough for them to return next season.

Roberto Di Matteo's men currently sit four points behind fourth-placed Newcastle in the Premier League and Torres said: "It would be a catastrophe to miss out on the Champions League and we must be prepared to do anything to achieve this.

"It doesn't matter who plays, who scores, who gives the assists and who stays out. The important thing is that we are successful.

"This team has slightly changed the way I play, because of their style. For me the most important thing is to score goals – that's what I practice every day – but we all know this season has been tough and the team is the most important thing."



Fernando Torres.

Chelsea striker Fernando Torres has admitted it would be a "catastrophe" if the club failed to qualify for next season's Champions League. Meanwhile Torres has hailed the influence of interim manager Di Matteo, who has rescued Chelsea's season with 10 wins and just one defeat in 14 matches.