ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 21, 2012

PINDA KUTOA TAMKO RASMI JUMATATU JUU YA TAARIFA ZA MAWAZIRI KUJIUZURU .

Waziri mkuu Mizengo Pinda akiteta na wabunge John Mnyika (kushoto), Zitto Kabwe na Hamad Rashid mjini Dodoma april 21. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
LIVE KUPITIA BONGO FLEVA NEW SEASSON NA ADAM MCHOMVU sauti ya ripota wa clouds fm kutoka mkoani Dodoma imewasilisha kuwa waziri mkuu Mh. Mizengo Pinda amkanusha taarifa zilizoripotiwa kupitia magazeti mbalimbali ya leo zikitaja mawaziri kadhaa kujiuzuru.

Mh. Waziri mkuu (akisikika live yeye mwenyewe) amesema kuwa hakuna barua yoyote aliyoipokea kutoka kwa mawaziri kujiuzuru na taarifa kamili huenda ataitoa jumatatu na kama kuna wanaotaka kujiuzuru basi watawasilisha kwake barua nae atatanabaisha kwa waandishi wa habari, lakini mpaka hivi sasa hakuna barua yoyote aliyoipokea kuhusu hilo na wala hana taarifa zozote kuhusu mawaziri waliojiuzuru..

Kabla ya habari hizo
Mawaziri nane wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete walitajwa kujiuzulu baada ya wabunge kumkalia kooni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusu ripoti chafu ya ubadhirifu wa fedha za umma zilizowasilishwa na wenyeviti wa kamati za tatu za Bunge.


Mawaziri waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu, Waziri wa Fedha, Mustapha Mkulo, Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), George Mkuchika, Waziri wa Maliasili na Utalii,Ezekiel Maige na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Haji Mponda.

Wengine waliotajwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu.

JIONEE SALIM ALI NEW COLLECTION,


BIOGRAPHY:
Salim ali worked as model for 2 years before establishing him self as fashion designer with his label Mtoko designs.
He has also worked as a stylist to different Tanzanian personalities for example Banana zorro and his band, EATV nirvana presenters.
He uses locally made materials like khanga, kitenge & and batiki to create original
african looks.
He showcased his designs in different fashion shows like lady in red fashion shows, swahili fashion week 2011, 2012. And also he was nominated in the category of the best menswear designer of the year 2011 by the swahili fashion week. And he has succeded to won the award of the best upcoming designer of the year in the lady in red fashion show.

Hii ni collection yangu ya tatu tangu niingie katika ulimwengu wa fashion. Na collection hii imekuwa inspired na rangi pamoja na dhima ya mimi kutaka kujitangaza zaidi, ndo maana nikaiita MNG'AO. Nimeizindua rasmi tarehe 18 april, alliance francaise nikiwa na model fromUS, Nyere Arinze. Pia katika kuonesha tofauti nimefanya piece moja ya nguo ya kike, hii ni kitu ambacho cjawai kukifanya kabla sababu yakuzoeleka kuwa ni base katika menswear. Na hii haimaanishi kama sas nimeamua kuingia katika kubuni mavazi ya kina dada, ilikuwa ni kuonesha tu tofauti kwa colletion hii.
THANX FOR YOUR SUPPORT.

Regards,
Salim Ali.
Tanzanian fashion designer.

WAHESHIMIWA WABUNGE WALIOJITOA MHANGA

Mbunge wa Ludewa (CCM), Deo Filikunjombe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Kulia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe anayefanya zoezi la kukusanya sahihi za wabunge ili aweze kuwasilisha bungeni hoja kutokuwa na imani na waziri mkuu. Picha na Edwin Mjwahuzi
Saturday, April 21, 2012 5:46 AM
01. Mhe. Rashid Ali Abdallah – cuf
02. Mhe . Chiku Aflah Abwao- chadema
03. Mhe . Saluim Ali Mbarouk – cuf
04. Mhe . salum Khalfam Barwany – cuf
05. Mhe . Deo Haule Filikuchombe- ccm
06. Mhe.Pauline Philipo Gekul- chadema
07. Mhe. Asaa Othman Hamad-cuf
08. Mhe. Prof.Kuliyokela Kahigi- Chadema
09. Mhe.Naomi Mwakyoma Kaihula – chadema
10. Mhe . Sylvester Kasulumbayi- chadema
11. Mhe. Raya Ibrahim Khamis - chadema
12. Mhe. Mkiwa Hamad Kiwanga - cuf
13. Mhe. Susan Limbweni Kiwanga- chadema
14. Mhe. Grace Sindato Kiwelu –chadema
15. Mhe. Kombo Khamis Kombo – cuf
16. Mhe. Joshua Samwel Nassari – chadema
17. Mhe. Tundu Antiphas Lissu- chadema
18. Mhe Aphaxar Kangi Lugola- ccm
19. Mhe susan Anselim Lymo- chadema
20. Mhe. Moses Machali – NCCR Mageuzi
21. Mhe. John Shibuda Magalle – Chadema
22. Mhe. Faki Haji Makame- Cuf
23. Mhe . Esther Nicholas Matiko- chadema
24. Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi- Chadema
25. Mhe. Freman Aikaeli Mbowe- chadema
26. Mhe. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – chadema
27. Mhe. Halima James Mdee-chadema
28. John John Mnyika- Chadema
29. Mhe. Augustino Lyatonga Mrema- TLP
30. Mhe . Maryam Salum Msabaha- chadema
31. Mhe. Peter Msingwa-chadema
32. Mhe. Christowaja Gerson Mtinda- chadema
33. Mhe. Philipa Geofrey Mturano- chadema
34. Mhe. Christina Lissu Mughwai- chadema
35. Mhe. Joyce John Mukya – chadema
36. Mhe. Mchungaji Israel Yohane Natse – chadema
37. Mhe. Philemon Ndesamburo- chadema
38. Mhe. Ahmed Juma Ngwali- - cuf
39. Mhe. Vincent Josephat Nyerere- chadema
40. Mhe. Rashid Ali Omar- cuf
41. Meshack Jeremiah Opulukwa- chadema
42. Mhe. Lucy Philemon Owenya- chadema
43. Mhe. Rachel Mashishanga- Chadema
44. Mhe. Mhonga Said Ruhwanya – chadema
45. Mhe. Conchesta Rwamlaza – Chadema
46. Mhe. Moza Abedi Saidy- cuf
47. Mhe. Joseph Roman Selasini – Chadema
48. Mhe. David Ernest Silinde- chadema
49. Mhe Rose Kamili Sukum - chadema
50. Mhe. Cecilia Daniel Paresso- chadema
51. Mhe .Kabwe Zuberi Zitto- Kigoma Kaskazini
52. Mhe. Magdalena Sakaya – Cuf
53. Mhe Rebecca Mngodo- Cuf
54. Mhe. Sabreena Sungura -chadema
55. Mhe. Hamad Rashid Mohammed- CUF
56. Mhe. Rukia Kassim Ahmed (Cuf)
57. Mhe. Mustapha Boay Akoonay (Chadema)
58. Mhe. Abdalla Haji Ali (CUF)
59. Mhe. Khatibu Said Ali (CUF)
60. Mhe. Hamad Ali Hamad (CUF)
61. Mhe. Riziki Omar Juma (CUF)
62. Mhe Haji Khatibu Kai (CUF)
63. Mhe. Anna Marystella John Malack -Chadema
64. Mhe. Hamad Rashid Mohamed (CUF)
65. Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed (CUF)
66. Mhe. Thuwayba Idrissa Muhamed (CUF)
67. Mhe. Masoud Abdallah Salum (CUF)
68. Mhe. Muhamad Ibrahim Sanya (CUF)
69. Mhe. Ali Khamis Seif (CUF)
70. Mhe. Haroub Muhammed Shamis (CUF)
71. Mhe. Amina Amour Nassoro (CUF)

Friday, April 20, 2012

ZURURA YA KAMERA YAKO KUZISAKA TASWIRA

Je waweza otea picha hii imepigwa, mpigaji akiwa jengo gani barabara ya Kenyata Mwanza? .

Hadi matenga.. matumizi yasiyofaa kwa mapipa madogo ya taka ndani ya mji.

Mapipa mengi ya taka yanahitaji ukarabati. Jeh! nijukumu la mdhamini au Halmashauri ya jiji kukarabati vitendea kazi hivi?

Kitako kime goo..

Nyaya hewani toka kwenye mita za luku kama china vile...

Kiukweli mara baada ya wahindi kutufilisi hakuna juhudi za dhati zinazoonekana kuhusu usafiri wa kutumia njia hizi.

Ndani ya ardhi yenye rutuba taratiiib' kitaa kinakuwa..

'Anang'ataa....'

Hata mti ukichoka hung'oka wenyewe.

Chemichemi ya maji..

Mzigo huooo kuelekea kamanga then Sengerema.

News breaking: 25 MAANDAMANO YA KUDAI HAKI YA MUUNGANO KATIKA KATIBA MPYA ZANZIBAR

HABARI za muda huu, zilizo nifikia zinadai kwamba kikundi cha Wanaharakati huko Zanzibar kinaongoza maandamano ya amani kwa ajili ya kudai haki ya Mzanzibar.
Lengo ni kushinikiza Baraza la Wawakilishi kuiagiza serikali kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano ipigwe ili uamuzi wake uingizwe kwenye katiba mpya.

Naendelea kufuatilia.
By Mdau wa Ukweli.

PATA MAWASILIANO YA HUDUMA ZOTE ZA ROCK CITY NDANI YA JARIDA LA 'MWANZA REVIEW'

In this issue we have presented to you in a more simple manner the flight schedulles for for April, Taxis in Mwanza, Contacts of many businesses that we could find, available houses for rent, the map to make you cruise easily in town and many more.

For more information: CONTACT US
PUBLISHER
RAIDERS LTD
P.O.BOX 10378 MWZ
TEL +255 68482624/
0659826242
raiderslimited@yahoo.com

"HAPPY BIRTHDAY SHEMEJIIIIiiiiiiii"

Leo ni birthday ya shemeji yangu 'wa ukweli' JUDITH ELLY KIMORI aka Mama Nancy aka Mama mzaa chema. Blog hii inakutakia kila la kheri katika harakati zako njema za maisha yako na familia kwa ujumla, furaha iwe juu yako.
Mungu akujaze yaliyo kheri daima na milele.
Happy birthday shemejiiiiiii!

Thursday, April 19, 2012

WABUNGE KUMNG'OA WAZIRI MKUU KUFIKIA J3?

Deo Filikunjombe:- Ameliambia bunge kuwa Waziri wa Fedha Mkulo sio muaminifu anaitafuna nchi. Wabunge hawana imani na baadhi ya mawaziri wetu.
Awali alisema wengi wa mawaziri ni wezi na ushahidi anao atautoa ameongeza kuwa anashangazwa kwamba tangu jana hadi leo hakuna hata Waziri mmoja aliye jiuzuru na hii ni kutokana na malalamiko ya wabunge kuhusiana na kutokuwepo kwa usimamizi kutokuwepo kwa uwajibikaji mali za wananchi mali za umma zinapotea.

Vicent Nyerere:- Anashangazwa kwamba magari yananunuliwa na kufanyiwa ukaguzi kwa makampuni feki yanayotajwa kuwa ofisi zake ziko nje, kwa hali hii mawaziri wanaruka sarakasi na taulo watabaki uchi.







Baada ya hapo wakafuata Wenyeviti wa Kamati

John Cheyo:- Alichoguswa zaidi ni kwa jinsi gani wabunge wameungana pamoja bila kujali itikadi zao katika kusimamia matumizi ya pesa za serikali nakuhakikisha kuwa fedha hazipotei kama ilivyo sasa.

Agustino Mrema:- Kuna haja sasa kuhakikisha kwamba kesi hizi zinazo husiana na watu waliotumia vibaya madaraka yao kwa kutafuna fedha za wananchi zinaharakishwa badala ya kusikilizwa kwa muda mrefu kama ilivyo hivi sasa.

Msumari wa Mwisho:Zitto Kabwe:- Yeye akasema huko huko TBS kumekuwa na matatizo mengi lakini bado viongozi wake wamekuwa kimya kunakosekana uwajibikaji akagusia kwamba kama kuna marekebisho mapya yanayopaswa kuwekwa katika katiba hii mpya ni uwajibikaji kwa wale ambao wamefanya vibaya, ambao wamelitia hasara taifa waweze kuwajibika kwa hili sasa akasema wao kama wabunge kuanzia kesho watakusanya saini 70 za wabunge watakaounga mkono hoja itakayoletwa Bungeni ya bunge kutokuwa na imani kwa Waziri mkuu ili jumatatu iwasilishwe. Lengo ni kukomesha ubadhirifu na wizi unaopewa baraka na mawaziri.

Ni kitu Live... leo leo tarehe 19/04/2012

MIFUKO YA AKIBA NCHINI YATAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA

Makamu wa Rais Dk. Ghali Bilal ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kuhakikisha kuwa inapanua huduma zake ili ziweze kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa wa maeneo ya vijijini na wale walio katika sekta zisizo rasmi.

Sehemu ya wadau wa Mkutano wa nne wa wanachama wa mfuko wa akiba ya wafanyakazi serikalini (GEPF) uliofanyika leo jijini Mwanza.

Pamoja na mchango mkubwa wa mifuko ya hifadhi ya jamii katika kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla, bado ni sehemu ndogo ya Watanzania wanapata kinga dhidi ya majanga mbalimbali kupitia mifuko hiyo.

Takwimu zinanaonyesha kuwa kati ya watanzania milioni 22 wenye uwezo wa kuzalisha kipato si zaidi ya asilimia 6 waliojiandikisha kwenye mifuko hiyo ya jamii.

Naye mkurugenzi mkuu wa Bodi ya mfuko wa akiba ya wafanyakazi serikalini (GEPF) Daud Msangi amesema kuwa mfuko wake umeanzisha mpango wa hiari wa kujiwekea akiba uzeeni ambao ni mahususi kwaajili ya watanzania wote bila kujali wanaishi kwa kutegemea mishahara ama vinginevyo.

Mfuko huo umeendelea kupata mafanikio ambapo kasi ya ongezeko la makusanyo kwa wanachama limekuwa likiongezeka mwezi hadi mwezi kuanzia shilingi milioni 2.62 mwezi Disemba mwaka 2009 hadi kufikia kiwango cha juu cha shilingi milioni 115 mwezi Septemba mwaka jana.

Ikafika muda wa kutoa tuzo hii ni tuzo ya kwanza... (jina laja)

Tuzo ya pili.. (jina laja)

Tuzo ya tatu... (jina laja)

Ndani ya maboresho ya mwaka huu mfuko wa mafao ya uzeeni kwa watumishi wa serikalini (GEPF) kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua huduma itayowawezesha wanachama wa mfuko wa GEPF walioko Tanzania nzima kurejesha na kulipa michango yao ya kila mwezi kwa kupitia huduma ya Airtel money.

BRIGEDIA JENERALI MWAKANJUKI AFARIKI DUNIA

Alipotembelewa na waziri Mkuu Mh. Pinda kujuliwa hali enzi zake za uhai wake Brigedia Jenerali mstaafu Mwakanjuki (kulia).
Waziri wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Brg. Gen. Mstaafu Mwakanjuki amefariki dunia mchana wa leo ktk hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es salaam.

HISTORIA yake inaonyesha kuwa miaka ya nyuma Jenerali huyo alikuwa askari polisi katika serikali ya Kibaraka wa Waingereza na Waarabu akiwa ndo kwanza kijana yaani PC katika kituo kikuu cha Malindi, Yeye pamoja na wananchi wengine hawakuufurahia uhuru feki wa Zanzibari kabla ya mapinduzi.

Amekuwa Waziri, Mbunge na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi wa muda mrefu anamwelezea marehemu kuwa.. Isingekuwa maamuzi mazuri ya Mwakanjuki katika siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, mapinduzi hayo yasingeweza kutokea au labda yangetokea kwa shida shida na huenda Wazinzibari wengi wangechinjwa vibaya sana siku hizo.

Jumbe alisema Mwakanjuki alikuwa zamu katika ghala la kutunzia silaha la polisi siku ya mapinduzi, na alipoona wananchi walioiasi serikali ya KiSultani wanakikaribia kituo chake ili wakiteke, badala ya kujihami kama ilivyo kwa askari yeyote mtiifu, lakini yeye akafungua ghala hilo na kuanza kugawia wananchi silaha na huo ndo ukawa mwanzo mpambano mkali kati ya jeshi la sultani na wananchi na hatimaye kupatikana kwa Mapinduzi hayo na Kukimbia kwa Sultani.

Hiyo ndiyo sababu watawala wengi huko Zanzibar kwa nyakati tofauti mpaka ule wa Amani Karume, hawakuweza kumsahau Mwakanjuki,bali walikuwa wakimpa titles tofauti tofauti, mara Mbunge wa kuteuliwa na Waziri, mara wa Kilimo, mara Uchukuzi etc almradi tu anakuwepo katika baraza la mawaziri akiwa Mkristo peke yake!.

Nakumbuka alipata ajali mwaka juzi vile akitokea Dodoma kwenye Halmashauri Kuu ya CCM na hali yake iliendelea kusuasua mpaka umauti ulipomfika.
MWENYEZI MUNGU TWAKUOMBA UILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN.

WANACHAMA WA GEPF KULIPA MICHANGO YAO KUPITIA AIRTEL MONEY

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mohamed Ghalib Bilal akizindua.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na Government Employees Pension Fund (GEPF),mfuko wa mafao ya uzeeni kwa watumishi wa serikalini, leo imezindua huduma itayowawezesha wanachama wa mfuko wa GEPF walioko Tanzania nzima kurejesha na kulipa michango yao ya kila mwenzi kwa kupitia huduma ya Airtel money ,

Kusanyiko.
Uzinduzi wa makubaliano haya yamefanyika leo katika hotel ya Golden crest mkoani mwanza na kuhudhuria na makamu wa Rais Dr Mohamed Ghalib Bilal ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi na kushiriki kuzindua huduma hii ya pekee itakayowawezesha wafanyakazi kulipia mafao yao bila usumbufu na kwa ufanisi zaidi.

Makamu wa rais.
Katika hotuba yake Mkamu wa Raisi Dr Mohamed Ghalib Bilal alichukua fulsa kuwashukuru Airtel kwa kutoa huduma zinazokithi mahitaji ya jamii na wateja kwa ujumla..aidha dr bilal amewapongeza GEPF kwa kupiga hatua na kutafuta njia mbadala za kuendesha shughuli zake kirahisi kwa ufanisi kwa hakika hatua ya kutafuta changamoyo zilizopo katika ukusanyaji wa malipo, ama kwa hakika hatua mliyoichukue niya kuigwa na vyombo vingine vya umma.

Asumpya Naligingwa.
Akizungumza kwa niaba ya Airtel Meneja wa kitengo cha Airtel money bw Asumpya Naligingwa alisema” Airtel leo tunajisikia furaha sana kugusa maisha ya watanzania kwa njia tofauti kupitia huduma hii ya Airtel money, kama mnavyofahamu kwa kupitia huduma ya Airtel money wateja wetu walioko nchi nzima wanaweza kufanya miamala mbalimbali ya fedha ikiwepo kulipa na kupokea pesa, kulipia Luku, USA visa, kulipia Maji DAWASCO, ada za shule , kununua petrol kwenye vituo kadhaa nchini na nyingine nyingi, leo kwa kushirikiana na wenzetu wa GEPF tunawezesha wafanyakazi na wanachama wote nchi nzima kuweza kurejesha michango yao kwa kupitia huduma ya Airtel money ambayo italeta na kuongeza ufanisi zaidi kwani sasa wateja wa Airtel wanaweza kulipia michango hii wakiwa mahali popote, siku yoyote, wakati wowote na bila usumbufu ”

Wadau wa Airtel Tanzania.
Tunaamini kabisa ushirikiano huu utaongeza na kuendelea kutunza idadi ya wanachama wa GEPF walioko sasa na kuleta ufanisi katika makusanyo ya michango kwa wanachama. Wenzetu wa GEPF wataweza kuona michango mara tu inapolipwa na pia itarahisisha njia ya malipo na kupunguza idadi ya watu wanaoenda ofisini au bank kulipia hivyo kuokoa muda unaotumika na wanachama kufanya malipo.

Jinsi ya kufanya malipo kupitia huduam ya Airtel money ni rahisi mteja anachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye menu ya Airtel money, lipa bill, ingiza jina la fumbo GEPF , ingiza reference namba ambayo ni namba ya uanachama, kisha bonyeza ndio, basi mojakwamoja akaunti ya GEPF itapokea mchango wako na kukutumia ujumbe utakaodhibitisha malipo yako aliongeza Naligingwa.

Wadau wa Airtel katika flash ya pamoja.
Makamu wa rais akisalimiana na wadau wa Airtel.
Naye Meneja masoko wa GEPF bwn Aloyce Ntukamazina alisema” namshukuru makamu wa Raisi Dr Bilal kwa khudhuria halfa hii na kuwa mgeni rasmi wa mkutano wa GEPF mwaka 2012. GEPF kwa kushirikiana na Airtel tumeanzisha mpango utakaotupa sisi GEPF njia ya kukusanya michango ya wanachama ya kila mwezi kwa asilimia kubwa sasa kulinganisha na hapo Awali. Tunawaomba wanachama wetu kutumia njia hii mbadala kufanya malipo yao wakati wowote bila usumbufu wala adha.”

CHELSEA 1 BARCELONA 0

Didier Drogba aliishangaza Barcelona alipofunga bao la Chelsea, na la pekee, katika mechi dhidi ya Barcelona, na kuiongezea timu yake matumaini ya kufika katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya.Drogba akipasia nyavu za Barcelona katika nusu fainali ya klabu bingwa mkondo wa kwanza.
Drogba alifunga katika kipindi cha kwanza, baada ya dakika mbili kuongezwa, huku vijana wa meneja wa Chelsea, Roberto di Matteo wakiimarisha ngome kali katika uwanja wao wa Stamford Bridge.

Barcelona waliumiliki mpira daima katika mechi hiyo, lakini walishindwa kumpita kipa wa Chelsea, Peter Cech.

Mara mbili Barcelona waligonga mwamba, lakini kweli bahati haikuwa yao. Hayo yalimpata Alexis Sanchez katika kipindi cha kwanza, na baadaye naye Pedro akitumaini kufunga bao la chini kwa chini, hakufanikiwa, na baadaye mkwaju wake pia ukigonga mwamba.

Kiungo cha kati wa zamani wa Arsenal, Cesc Fabregas, naye alielekea kufunga, lakini mpira ukaokolewa na Ashley Cole kabla tu ya kuingia wavuni.

Ingawa Chelsea imefanikiwa kuongoza mkondo wa kwanza wa nusu fainali baada ya timu hizo kukutana Jumatano jioni, bila shaka wachezaji hao wa timu ya England wanafahamu watakuwa na kibarua kigumu katika uwanja wa Nou Camp wiki ijayo katika mkondo wa pili.

CHANZO: bbc swahili.

Wednesday, April 18, 2012

TOTO YAENDELEA KUGAWA DOZI ZA JIONI YAMNYWESHA AFRICAN LYON DAWA 3 CHUNGU

Kikosi cha Toto Africans 2012.
Mara baada ya kutembeza kichapo cha 3-2 kwa Yanga mwishoni mwa wiki Toto Africans ya jijini Mwanza leo tena imeendeleza wimbi lake la kugawa dozi za jioni ikijitengenezea mazingira mazuri kuukwepa mstari wa hatari wa kushuka daraja mara baada ya kuizabua African Lyon ya jijini Dar es salaam bao 3-0 katika dimba lake la CCM Kirumba Mwanza.
Madaktari wa wakimpatia tiba beki wa Toto Africans aliyeumia kwenye paji la uso na kuvuja damu nyingi mara baada ya kugongana na mchezaji wa Lyon.
Wakiliandama lango la Lyon na kucheza kufa na kupona Toto walianza mbio zao za kuusaka ushindi kwa goli safi la dakika ya 12 mfungaji akiwa Mussa Said Mussa aliyepokea pande safi toka kwa winga aliyekuwa akihaha uwanja mzima Emma Swita.

Mara baada ya bao hilo African Lyon ilirejea kwenye mchezo lakini mashuti ya wachezaji wake Hassan Goboso na Benedict Jackob hayakuwa na macho kuziona nyavu za Wanakishamapanda.

Wakati wapenzi wa kandanda wakiamini kuwa kipindi cha kwanza kitayeyuka kwa matokeo yaleyale ilikuwa ni dakika ya 43 Iddy Moby aliyeitumia vyema pasi ya Mnaigeria Enyina Darlington kwa kuipatia Toto goli la pili. Hadi mapumziko Toto ilikuwa inaongoza goli 2 - 0.

Kasi ya mchezo ilirejea upya kipindi cha pili kwa pande zote mbili kushambuliana na kucheza kandanda salfi la kuonana. Hatimaye mwiba wa mwisho kwenye jeraha la Africa Lyon ukashindiliwa na Salum Kamana aliyefunga katika dakika ya 87 ya mchezo.

Hadi Mwisho wa game Toto 3 African Lyon 0.