ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 30, 2012

POLE BROTHER EDGAR MAPANDE KWA KUFIWA NA BIBI MZAA BABA, MAZISHI KUFANYIKA JUMAPILI MAMBA WILAYA YA SAME MKOANI KILIMANJARO


Leo kuanzia majira ya saa 7:30 mchana hadi saa 8 mwili wa Bibi Eva E. Mapande umeagwa nyumbani kwa mwanae eneo la Nyakato jijini Mwanza ambapo pia ibada maalum kumwombea marehemu ilifanyika kabla ya kusafirishwa kuelekea Mamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro.

Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na Edgar Mapande ambaye ni mjukuu wa marehemu bibi Eva E. Mapande alizaliwa mnamo mwaka 1920 na kufariki dunia tarehe 28 nov 2012, katika zama za mwisho marehemu pamoja na uzee alikuwa akisumbuliwa na macho hali iliyomsababisha kushindwa kuona kabisa hadi mauti inamchukuwa.


Mchungaji wa kanisa la Sabato akiendesha ibada kabla ya heshima za mwisho kwa marehemu kutolewa.


Sehemu tu ya watoto wa marehemu kwenye ibada hiyo iliyofanyika nyumbani.


Mr. Hamza akiongoza hatua ya kutoa heshima za mwisho kwa marehemu.


Majonzi yametawala  katika kuuaga mwili wa marehemu bibi Eva E. Mapande.


Majirani, ndugu jamaa na marafiki wameshiriki ibada hii ya kuuaga mwili wa marehemu bibi Eva E. Mapande


Ibada hii ya kuuaga mwili wa marehemu bibi Eva E. Mapande imehudhuriwa pia na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Mwanza, Sixbeth Reuben.


Ibada ya kuuaga mwili wa marehemu ikiendelea.


Ndugu na marafiki wameshirikiana pamoja kupeana moyo.
Marafiki na ndugu eneo la tukio.


Jipe moyo.


Mara baada ya kukamilika kwa ibada maalum kumwombea marehemu ilifanyika Nyakato jijini Mwanza, safari ikawekwa sawa kuelekea Mamba wilayani Same mkoani Kilimanjaro kwaajili ya mazishi yatakayofanyika jumapili hii ya kesho kutwa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.