ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 25, 2012

BREKING NEWS: POLISI WAWANASA WAUAJI WA KAMANDA BARLOW MWANZA

Manumba akitaja majina ya wahusika pembeni kushoto ni IGP Mwema.

Majina ya watu watano  wanaotuhumiwa kuhusika moja kwa moja na kifo cha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Leberatus Barlow yametajwa rasmi leo jijini Mwanza.


 Kabla ya hapo DCI Manumba alitoa taarifa juu ya uchunguzi uliofanyika na kikosi chake na kupelekea kunaswa wahusika hao... Msikilize kwa kubofya hapo juu kwenye play.

Akitaja majina hayo mbele ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema, MKURUGENZI wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba,  amesema kuwa simu iliyoporwa ya mwanamama ambaye alikuwa akisindikizwa nyumbani na marehemu ndiyo imesaidia kukamilisha upelelezi huo hatimaye wahusika kukamatwa...

Majina ya wahusika hao kuwa ni Muganyizi Michael Peter (36) ambaye inatajwa kuwa ndiye aliyemuua Barlow, Chacha Waitare Mwita (50), Magige Mwita Marwa (48),  Buganzi Edward Kusuta pamoja na Bhoke Marwa Mwita (42) ambao wote wamekatwa katika jiji la Dar es Saalm.

Damu ya aliyekuwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Barlow
Alisema Kikosi kazi cha upelelezi kilichokuwa chini yake  Manumba kilijigawa kwenye makundi matatu moja ni lile la Ukamataji, Mahojiano na lingine la interejensia huku wakitumia njia ya sanyansi kwa kufuatia mitandao ya simu.

Kukamatwa kwa watuhumiwa hao wa dar na wale wa Mwanza kunafanya jumla yao kuwa 10 na bado jeshi linasaka wengine.  Lakini hakuna sababu iliyotokana na mauaji hayo ambayo imeelezwa mpaka sasa na jeshi hilo.

Wengine watano wanaoshikiliwa kwa usalama ni pamoja na Doroth Alicia Lymo (42) kabila mchaga mwalimu wa shule ya msingi Nyamagana  mkazi wa Kitangili Minazi mitatu Mwanza ambaye alikuwa na marehemu siku ya tukio akisindikizwa,  Felix Felician Minde (50) kabila mhaya  mfanyabiashara mkazi wa Lumala na  Fumo Felician Minde (46) kabila mhaya mfanyabiashara mkazi wa kona ya Bwiru.

Wengine katika orodha hiyo ni  Bahati Agustino Lazaro kabila Muha Mfanyabiashara mkazi wa Nyakabungo na Amos Weibe Magoto (Bonge) ambaye ndiye aliyekutwa na simu ya mwalimu Doroth


Liberatus Barlow aliuawa Oktoba 13 mwaka huu, saa 8 usiku kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika eneo la Minazi mitatu huko Kitangiri wakati alipopita kumsindikiza Mwalimu Dorothy Moses nyumbani kwake kutoka katika kikao cha harusi kilichofanyika Mtaa wa Rufiji. moja  


Msikilize kwa kubofya hapa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania IGP Said Mwema akizungumzia juu ya source ya mauaji..
Baadhi ya Polisi wakifuatilia kinachojiri ndani ya ukumbi wa Halmashauri ya jiji la Mwanza jioni ya leo.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.