ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, July 19, 2012

MH MKONO ATIMIZA AHADI YAKE YA KUPELEKA MADAWATI KATIKA SEKONDARI YA BUTUGURI

Gari kutoka Halmashauri ya Musoma likiwa linapakia madawati yaliyotengenezwa na TASAF tayari kurudishwa kwenye Halmashauri


Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondary Butuguri Godfrey Robert


Moja ya Madawati yaliyotengenezwa na Mh Mkono


Wadau wakiangalia baadhi ya Madawati yaliyotengenezwa na TASAF
MUSOMA
Na
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Nimroadi Mkono amekamilisha ahadi yake ya kupeleka Madawati mapya katika shule ya sekondari Butuguri baada ya kubainika kuwa madawati yaliyotengenezwa na mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika shule hiyo hayana ubora.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea awamu ya kwanza ya Madawati zaidi ya 50,diwani wa kata ya Butuguri Mwita Charles alimpongeza Mbunge huyo kwa kukamilisha ahadi hiyo huku akitoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano huo.

Diwani huyo alisema kuwa Madawati yaliyotengenezwa na TASAF hayana ubora na hivyo anaunga mkono kauli ya Mh Mbunge kuyarudisha Madawati hayo katika Halmashauri ya Musoma.

Kuhusu wale wote waliohusika katika ubadhilifu huo diwani huyo alisema kuwa wanatakiwa kuchukuliwa hatua za kisheria ili iwe fundisho kwa viongozi wengine ambao wapo kwa masilahi yao.

Naye Mwalimu mkuu Wa Shule hiyo Godfrey Robert alisemshukuru Mbunge huyo na kusema kuwa amesaidia kupunguza mzigo kwa wazazi katika kukabiliana na upungufu wa madawati uliokuwepo shuleni hapo.

Amesema Madawati yaliyokuwepo hayatoshi ikilinganishwa na idadi ya wanafunzi waliopo katika shule hiyo,na hivyo mwaka huu walikuwa na mpango wa kutengeneza madawati hayo.

Aidha madawati yote yaliyotengenezwa na mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF tayari yamerudishwa katika halmashauri ya Musoma Vijijini kutokana na kutokuwa na kiwango kinachokubalika

Hivi karibuni akifanya ziara shuleni hapo mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Nimrodi Mkono aliyakataa madawati zaidi ya 1000 yaliyotengenezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF kutokana na kutokuwa na kiwango chenye ubora

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.