ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, June 7, 2012

NASIBU RAMADHAN V/S FADHILI MAJIA ULINGONI 9/6/2012

FADHILI MAJIA(pichani) ANAMKABILI NASIBU RAMADHAN katika pambano la ubingwa wa WBO la raundi kumi azito wa fly weight, siku ya jumamosi 9/06/2012 katika ukumbi wa friends corner hotel-manzese.

Akilizungumzia pambano hilo katibu mkuu wa TPBO IBRAHIM KAMWE ”BigRight” ambao ndio wasimamizi wa pambano hilo amesema kuwa maandalizi yote yamekwisha kamilika na mabondia wote wapo katika hali nzuri kiafya na morali wa kulisubiria kwa hamu pambano hilo kubwa.

Amsema kuwa katika siku hiyo pia kutakuwepo na mapambano kadhaa ya utangulizi kama vile ABDALLAH MOHD’ Prince Naseem’ atakayemenyana na YOHANA MATHAYO, JUMA FUNDI v/s SHABAN MADILU, VENANCE MPONJI v/s JONAS GODFREY na mapambano mengineyo mengi.

Pia katibu huyo wa TPBO akaongeza kuwa jopo lake limejipanga vyema kwa kuwa na marefa pamoja na majaji wenye uzoefu na ngumi, "Siku zote huwa tunasimamia mchezo kwa haki na kufuata sheria na taratibu za ngumi hakuna upendeleo wa upande wowote hivyo tunawaomba mashabiki waje kwa wingi kutizama ngumi zenye ufundi wa hali ya juu na ushindani mkubwa" alisema

"Nimehakikishiwa na promota Kaike na akanionesha vielelezo vyote vya polisi kuwa ulinzi na usalama utakuwa wa hali ya juu na sehemu ya kuegeshea magari ipo ya usalama" aliongeza katibu huyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.