ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 22, 2012

NKABAaaaaa....!!! ..YONDANI ATUA YANGA

Awa kivutio mazoezini" "Gazeti moja laumbuka kwa propaganda za Simba"
"Kisa eti ametekwa na Simba"
Hatimaye aliyekuwa beki wa kutumainiwa wa klabu ya Simba katika msimu uliopita Kevin Yondan "Vidic" leo amekata mzizi wa fitina baada ya kuanza rasmi mazoezi katika uwanja wa Kaunda uliopo Makao Makuu ya klabu ya Yanga na kuwa kivutio katika mazoezi hayo.

Kipenzi hicho cha Yanga kiliwasili majira ya saa tatu kasoro dakika kumi asubuhi, ambapo mara baada ya kushuka katika gari mashabiki waliofurika katika mazoezi hayo walipomuona ghafla walimshangilia kwa vifijo na nderemo huku akielekea uwanjani akiwapungia mashabiki hao mikono.

Vidic ambaye ana mapenzi makubwa na klabu ya Yanga, leo ameripotiwa na chombo kimoja cha habari kuwa eti alitekwa hapo jana na klabu ya Simba na kudaiwa kushiriki katika mazoezi na timu yake hiyo ya zamani.

Kelvin Yondan

Mchezaji huyo ambaye kila kukicha timu yake hiyo ya zamani ikiendelea kumuota kwa mazuri aliyowafanyia amekuwa gumzo kwa kipindi hiki cha usajili ambapo timu yake mpya ya Yanga ikiendelea kufanya kufuru ya usajiri ambao unatarajiwa kumalizika Julai 15 Mwaka huu.

Yondan hivi karibuni aliwashukuru wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba kwa ushirikiano aliokuwa akiupata wakati akiitumikia timu hiyo,aliweka bayana mara baada ya kumwaga wino kuichezea Klabu ya Yanga kuwa Simba isihangaike na yeye kwakuwa hana mpango tena wa kuichezea klabu yake ya zamani.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanachama mmoja wa klabu ya Simba kwa jina maaraufu (Kobe) muda mfupi uliopita wakati www.youngaficans.co.tz ikiwa mitamboni aliwasili katika mazoezi ya timu ya Yanga yaliyokuwa yakifanyika katika uwanja wa Kaunda kwa ajili ya kutaka kuhakikisha juu ya uvumi wa beki Kevin Yondan kuwa yupo katika mazoezi.

Mara baada ya kumshuhudia mchezaji huyo akifanya mazoezi mwanachama huyo aliangua kilio uwanjani hapo huku mashabiki wa Yanga wakishangilia na kumnunulia maji ya matunda pamoja na uji.
Wachezaji wengine walioanza mazoezi leo ni pamoja na kiungo wa timu ya Taifa Frank Domayo aliyekuwa JKT Ruvu na mshambuliaji wa timu ya Taifa Saimon Msuva aliyekuwa Moro United.

Naye Kocha msaidizi wa Klabu ya Yanga Fredy Felix Minziro amesema kikosi chake chote kinatarajiwa kukamilika mara baada ya wachezaji Haruna Niyonzima aliyekuwa na timu ya Taifa lake(Rwanda) na Rashid Gumbo anayeumwa malaria watakapojiuunga na kikosi hicho.
Habari kwa hisani ya http://www.youngafricans.co.tz

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.