ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 22, 2012

AIRTEL YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA SHULE ZA MSINGI ZA GONGOLAMBOTO

 Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu wa Taaluma na michezo wa shule ya msingi ya Gongolamboto Jaika Mwl Almasi Shemdoe wakati Airtel ilipotembelea shule za msingi za Gongolamboto za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika na kugawa vifaa vya michezo hapo Jana

 Walimu wa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika wakiwa na jezi zao mara baada ya kukabithi vifaa vya michezo na Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel, makabithiano hayo yalifanyika katika shule ya msingi Maarifa Gongolamboto jijini Dar es Saalam. Pichani (Katikati) ni Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde

 Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Maarifa Mwl Marietha Mulyalya wakati Airtel ilipotembelea shule za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika Gongolamboto na kukabidhi vifaa vya michezo hapo Jana

 Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde akikabidhi jezi za mpira kwa Mwalimu wa Taaluma na michezo wa shule msingi ya Mwangaza Mwl Abdul Mwarami wakati Airtel ilipotembelea shule za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika Gongolamboto na kukabidhi vifaa vya michezo hapo Jana

Walimu wa shule za msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika wakiteja jambo mara baada ya kukabithiwa vifaa vya michezo na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.
 Kikundi cha kwaya cha shule ya msingi ya Maarifa kitumbuiza wakati wa hafla ya kukabithiwa vifaa vya michezo illiyofanywa na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel katika shule ya msingi Maarifa Gongolamboto jijini Dar esa saalam

Na Mwandishi wetu.
Shule za msingi zilizoko Gongolamboto Dar es saalam zimenufaika na vifaa vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel jana katika halfa fupi iliyofanyika katika shule ya msingi maarif. Airtel imetoa vifaa vya michezo lengo likiwa ni kuleta hamasa na kuwajenga wanafunzi katika mchezo wa soko wakiwa mashuleni na katika umri mdogo.
Vifaa hivyo vya michezo vimetolewa na Airtel kwa shule za Msingi za Mwangaza, Maarifa na Gongolamboto Jaika ambapo kila shule ilipata seti moja ya jezi na Mipira.

Akiongea mara baada ya kupokea vifaa hivyo mkuu wa shule ya maarifa Bi Marieta Mulyalya alisema “ Natoa shukurani zangu za dhati kwa Airtel kwa kutoa vifaa vya michezo kwa shule za Gongolamboto na kuahidi kuvitumia vizuri kwa manufaa ya shule na wanafunzi na washukuru Airtel kwa msaada wa madawati ambayo walituleate wiki chache zilizopita na tunawaomba Airtel
waendelee kutoa msaada si kwa shule yake tu bali na kwa shule za jirani pia ambazo pia zina mahitaji Mengi”.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa Uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde alisema” Airtel inatambua mchango wa michezo mashuleni na katika kuendeleza kuinua kiwango cha soka nchini ndio maana tunaendelea kuwawezesha wanafunzi hawa kuendeleza mchezo wa mpira kwa kuchangia vifaa hivi muhimu. Tunaamini jezi hizi zitatumika katika michuano mbalimbali shule ili kuwawezesha kukuza vipaji vyao ambapo matokeo yake ni kuzalisha kikosi kizuri cha timu ya taifa”

Mwenzi uliopita Airtel ilitoa madawati kwa shule ya Maarifa na kuwawezesha wanafunzi kupata madawati ya kukali ambayo ilikuwa changamoto kubwa shuleni hapa kwasababu shule hzo ni kati ya shule zilizoathiriwa na mlipuko wa mabomu uliotokea katika ghala la kuifadhia silaa la Gongolamboto.

“leo tunayofuraha kuwapatia vifaa vya michezo shule ya maarifa pamoja na shule za jirani za Mwangaza na Gongolamboto Jaika,. Airtel bado inaendelea kutoa vifaa vya michezo ambapo hivi karibuni inategemea kugawa vifaa vya michezo kwa Zaidi ya shule kumi zilizoko Nyanda za juu kusini ikiwemo mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, Songea na Rukwa” alimalizia kusema Bi Matinde.

Airtel imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika sekta ya michezo lengo likiwa ni kukuza maendeleo ya michezo hapa nchini, mwaka huu Airtel kwa mara nyingine iimeendelea kuendesha program yake ya kuinua vipaji vya vijana chini ya miaka 17 ijulikanayo kama Airtel Rising Stars ambapo vijana wengi wameweza kufaidika na program hiyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.