ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, May 18, 2012

MWILI WA MAFISANGO WAAGWA NA WATANZANIA

Wachezaji wa timu ya Taifa la Tanzania iliyoteuliwa hivi karibuni, mbele ni Juma Nyoso (L) na John Boko (R) wakiwa wamebeba jeneza la mwili wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya Simba marehemu Patrick Mafisango, kwaajili ya kuagwa katika viwanja vya  TTC Chang'ombe jijini Dar es salaam nchini Tanzania.

Mwili wa marehemu ukiwasili viwanjani hapo kwaajili ya wadau mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho, mbele wanaonekana Juma Nyoso na John Boko na kwa nyuma ni Shahbani Nditi.
Kombe la Ubingwa Tanzania Bara likiwa limewekwa juu ya jeneza la marehemu Patrick Mutesa Mafisango aliyezaliwa mwezi March mnamo mwaka 1980 na kufariki dunia tarehe 17 May 2012.
Sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania wakiwa na majonzi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mchezaji wa Simba aliyefariki dunia Patrick mafisango.

Golikipa wa Simba na Taifa Stars Juma Kaseja alishindwa kujizuia kulia hali iliyosababisha kupatiwa msaada toka kwa marafiki waliojitokeza kuuaga mwili wa marehemu Patrick Mafisango.

Mafisango, alikuwa amechaguliwa kuchezea kikosi cha kitakachowania kufuzu kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 dhidi ya Algeria alifariki katika ajali ya barabarani asubuhi ya kuamkia jana mjini Dar es Salaam Tanzania katika ajali iliyohusisha pikipiki na gari wakati gari alilokuwa akiliendesha lilipoteza mwelekeo na kuanguka kwenye mtaro..

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.