ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 19, 2012

MIFUKO YA AKIBA NCHINI YATAKIWA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIUNGA

Makamu wa Rais Dk. Ghali Bilal ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii nchini kuhakikisha kuwa inapanua huduma zake ili ziweze kuwafikia watanzania wengi zaidi hasa wa maeneo ya vijijini na wale walio katika sekta zisizo rasmi.

Sehemu ya wadau wa Mkutano wa nne wa wanachama wa mfuko wa akiba ya wafanyakazi serikalini (GEPF) uliofanyika leo jijini Mwanza.

Pamoja na mchango mkubwa wa mifuko ya hifadhi ya jamii katika kukuza uchumi na maendeleo kwa ujumla, bado ni sehemu ndogo ya Watanzania wanapata kinga dhidi ya majanga mbalimbali kupitia mifuko hiyo.

Takwimu zinanaonyesha kuwa kati ya watanzania milioni 22 wenye uwezo wa kuzalisha kipato si zaidi ya asilimia 6 waliojiandikisha kwenye mifuko hiyo ya jamii.

Naye mkurugenzi mkuu wa Bodi ya mfuko wa akiba ya wafanyakazi serikalini (GEPF) Daud Msangi amesema kuwa mfuko wake umeanzisha mpango wa hiari wa kujiwekea akiba uzeeni ambao ni mahususi kwaajili ya watanzania wote bila kujali wanaishi kwa kutegemea mishahara ama vinginevyo.

Mfuko huo umeendelea kupata mafanikio ambapo kasi ya ongezeko la makusanyo kwa wanachama limekuwa likiongezeka mwezi hadi mwezi kuanzia shilingi milioni 2.62 mwezi Disemba mwaka 2009 hadi kufikia kiwango cha juu cha shilingi milioni 115 mwezi Septemba mwaka jana.

Ikafika muda wa kutoa tuzo hii ni tuzo ya kwanza... (jina laja)

Tuzo ya pili.. (jina laja)

Tuzo ya tatu... (jina laja)

Ndani ya maboresho ya mwaka huu mfuko wa mafao ya uzeeni kwa watumishi wa serikalini (GEPF) kwa kushirikiana na Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imezindua huduma itayowawezesha wanachama wa mfuko wa GEPF walioko Tanzania nzima kurejesha na kulipa michango yao ya kila mwezi kwa kupitia huduma ya Airtel money.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.