ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, April 6, 2012

ALLIANCE WAIBUKA VINARA WA SOKA SHULE ZA MWANZA

Michuano ya soka yenye lengo la kukuza vipaji vichanga iliyoshirikisha shule za msingi 10 na sekondari 10 kwa jiji la Mwanza iliyoanza tangu machi 15 2012 imemalizika leo kwa mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na fainali ya kumsaka bingwa.

Timu za waandaaji wa michuano hiyo Alliance Sports Academy zimetoka kidedea kwa kuzitwaa nafasi zote za ubingwa kwa Shule ya Msingi na Sekondari michezo ikifanyika kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mchezo wa kwanza ulikuwa wa kutafuta mshindi wa tatu baina ya Igoma Secondary iliyopepetana na Mahina Sec mchezo uliolazimu kuingia katika hatua ya matuta mara baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90.

Kwenye mikwaju ya penati Igoma Sec imeitwaa nafasi ya tatu kwa kuifunga Mahina Secondary bao 4-2.

Mchezo wa pili ulikuwa ni fainali ambapo Alliance Sec iliichabanga Mtoni Secondary bao 1-0 na kutawazwa mabingwa, bao hilo la ushindi likifungwa na mshambuliaji Selemani Shadrack katika dakika za mwanzo tu za mchezo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.