ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 21, 2012

WANDISHI WA HABARI MWANZA WATEMBELEA TBL NAO MGAO WA UMEME CHANZO CHA KUPANDA BEI YA BIA

Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Edith Mushi akizungumza na waandishi wa habari kabla ya safari kuanza kutembelea eneo la kiwanda hicho lililopo Ilemela jijini Mwanza, ili kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji.

Mwishoni mwa wiki waandishi wa habari walipata fursa kutembelea kiwanda cha bia TBL mkoani Mwanza kujionea mapinduzi mapya yanayopangwa kufanyika ndani ya kampuni hiyo hasa katika sekta ya uzalishaji.

Meneja wa TBL Mwanza Richard Rymond akitoa maelezo katika kitengo cha mitungi ya kupika bia.

Mfanyakazi wa TBL kikazi zaidi.

Kwamujibu wa meneja wa kampuni hiyo amesema kuwa mgao wa umeme pamoja na kukatikakatika mara kwa mara kwa nishati hiyo ni miongoni mwa sababu zinazochangia kupanda bei kwa bia zinazotengenezwa na kampuni hiyo.

Meneja wa TBL mkoa wa Mwanza Richard Raymond amesema kuwa si lengo la TBL kupandisha bei ya bia kila wakati, lakini wanalazimika kufanya hivyo kutokana na mgawo wa umeme hivyo huamua kutumia majenereta ambayo huzifanya gharama za uzalishaji kuwa juu.

Sababu nyingine inayotajwa ni ongezeko la mara kwa mara la kodi na ushuru katika malighafi zinazotumika kuzalisha bia.

Kitengo cha uchujaji bia kimeboreshwa kwa kufungwa mitambo ya kisasa zaidi na hili ni moja kati ya machujio yaliyopo kwenye mashine hii.

Kidampa kikihamisha bia zilizozalishwa.

Ndipo ukawadia wakati wa SHINDANO LA 'WHO IS THE GREAT TEASTER' (muonjaji bora wa bia).

"Rilaxini' ni zoezi linalotumia ulimi, harufu, rangi ya kinywaji na kisha utulivu" sauti ya dada mdau toka TBL ilisikika.

Mwandishi Emanuel Chacha toka ITV ni mmoja kati ya watu wanne walioingia fainali na hapa zilitengwa glass tatu kwa kila mmoja.

Henry Kavirondo toka Chanel ten ndiye mshindi wa kwanza akigongana na ....

Jackline Wanna mwandishi wa habari wa gazeti la Mzawa na Kasi Mpya naye yu mshindi wa kwanza akigongana na Kavirondo.

Mshindi wa tatu

Emmanuel Chacha wa ITV mshindi wa nne na zawadi yake.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) tawi la Mwanza sambamba na kufanya upanuzi katika eneo lake la uzalishaji pia imeboresha vitengo vyake vya kuhifadhi malighafi lengo likiwa ni kwaajili ya kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. kaka hamjarudisha change kweli? maana huo mkanganyiko ni balaa

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.