ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 5, 2012

PICHA ZA AWALI ZA FIDELINE IRANGA ZAANZA KULIKI

Mara baada ya kimya kingi na na maswali mengi kutawala fikra na vinywa vya watu juu ya wapi alipojificha Super Model mwenye mvuto wa kipekee toka nchini Tanzania anayekwenda kwa jina la Fideline Iranga hatimaye picha zake za awali za 'modo' huyo zimeanza kuliki' kupitia mitandao ya marafiki zake tena akiwa katika muonekano mpya kabisa ambao umewashtua wengi akiwa 'kimodo' hata wakihoji kunani na wasipate majibu.

Picha hii na hiyo ya awali juu zimetoka hivi majuzi katika siku yake ya kuzaliwa kupitia Blogu ya U-turn
zikimuwishi na zikiwa na maneno 'Karudije kuwa mwembamba usupa model umerudi tutakomaje sasa kwenye runway.... chezea Fide'

Idadi ya watu waliokomenti juu ya picha hizo wameonekana wakijigawa katika pande mbili, kundi la kwanza likilaumu hatua aliyoichukuwa ya kujikondesha na kundila pili likisifia mpango huo.

Komenta mmoja kasema:- "Wabongo bwana yaani mtz akipungua hata kama alikuwa anafanya diet watauliza kaumwa nini? Kawaje? na wengine watampachika maradhi kuwa siyo diet, lakini akifanya mzungu/black mzungu kama Jernifer Hudson itawatoka wow na masifa kibao, kafanya diet kapendeza blah blah!"

Fide tha way back.....

Alitambulika sana kwa picha za vivazi nusu dizaini halikadhalika zenye mikao ya 'UTATA' swali ni jeh! SECOND SEASSON ya ujio wake Fide, atarejea na style zipi?

Si mara ya kwanza kwa watz kuhusika na projekti kama hizi za kupunguza mwili kwani hata mbunifu maarufu wa mavazi nchini Hassanali naye alipata kuhusika na sasa maisha yanasonga...

Any ways twakungoja sana siku utakapo jitokeza hadharani, Kila la kheri mdafada Fideline Iranga.

Tupe maoni yako

4 comments:

  1. ngoma nini?! huyu dada simfagiliii kabisa sura imekomaaa ka pimbi plus mashauzi ya kijinga!

    ReplyDelete
  2. Ah wapi, kwisha habari yake.

    ReplyDelete
  3. OMG mbona kawa kituko zaidi ya kituko alivyokuwa? tafadhali g tupia pix za full body tutathimini mengineyo you know mambo yetu yaleee.

    ReplyDelete
  4. Yaani huyu ndo mwenye mvuto baasi bwana

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.