ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 17, 2012

CITY NA UNITED WATAMBA LIGI YA EUROPA

Mchezaji wa zamu Sergio Aguero alipata bao dakika za mwisho na kuiwezesha Manchester City, baada ya kufungwa, hatimaye kuweza kujikakamua na kupata ushindi wa magoli 2-1 ilipocheza na Porto ya Ureno, usiku wa Alhamisi, ikiwa ni mechi ya mkondo wa kwanza wa mechi ya ligi ya Europa, kati ya timu 32 ambazo bado zimo katika mashindano.

Licha ya Porto kutangulia kufunga Man City waliibuka na ushindi Porto, ikicheza katika uwanja wa nyumbani, ilikuwa imetangulia kwa kupata bao kupitia Silvestre Varela.

Man City walipata nafasi ya kusawazisha wakati Alvaro Pereira alijifunga mwenyewe kwa kuuelekeza mpira kwa bega hadi wavuni, kufuatia mkwaju kutoka Yaya Toure, mpira ambao alitazamia utamfikia Balotelli.

Manchester United wamo katika hali bora zaidi baada ya kupata mabao ugenini Katika mechi ya awali, Ashley Young na Javier Hernandez walifanikiwa kufunga magoli katika kipindi cha pili, na kuishinda Ajax magoli 2-0, na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea katika mashindano ya ligi ya Europa.

Bao la pili Hernandez bila shaka litaisaidia sana United itakapoikaribisha Ajax katika uwanja wa Old Trafford kwa pambano la mkondo wa pili tarehe 23 mwezi huu wa Februari.

Licha ya kwamba vilabu mwamba vya Uingereza vimezoea zaidi ligi ya mabingwa na ambao inaheshimika zaidi kushinda Europa, meneja Ferguson ameelezea kwamba wao washatulia baada ya kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa, na sasa wanaonyesha ustadi wao kiufundi katika mashindano ya Europa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.