ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 20, 2012

VITUKO VYA SLAA KWENYE MAZISHI YA MTEMA;

VITUKO VYA SLAA KWENYE MAZISHI YA MTEMA...”Mchumba” wake AMZUIA ASISALIMIANE NA JK, KISA? ITALETA MANENO…!
Mazishi ya Mbunge wa Chadema, Mheshimiwa Regia Mtema yamethibitisha kuwa vituko na vioja vya Katibu Mkuu wa Chadema, Mheshimiwa Wilbroad Slaa na “mchumba wake,” Josephine Mushumbusi havijaisha hata kama sasa wanaishi pamoja.

Kwa namna ambayo sasa imethibisha nani hasa mwenye madaraka, mamlaka na kauli ndani ya nyumba yao, Josephine Mushumbusi amemzuia “mchumba/mume” kwenda kumpa mkono Kiongozi wa nchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.

Mara baada ya Rais Kikwete kuingia katika makaburi ya familia ya Mtema mjini Ifakara kiasi cha saa tisa unusu mchana, Mheshimiwa Slaa ambaye alikuwa amekaa peke yake na Josephine pamoja na Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema, alionyesha ishara ya kwenda kumsalimia Mheshimiwa Rais Kikwete ambaye alikuwa jukwaa kuu. Lakini Josephine Mushumbusi alimzuia mchumba wake asiende kumsalimia Rais Kikwete akimwambia, “usiende…italeta maneno ya bure.” Kwa namna inayothibitisha nani bosi ndani ya nyumba, Mheshimiwa Slaa alijikunja na kusalimu amri akisema, “haya bwana”.

Kila dalili za tukio hilo zimethibisha kuwa ubabe na ushujaa ambao Mheshimiwa Slaa huonyesha hadharani kwa kutukana, kukejeli na kuwashambulia wenzake katika siasa akiwamo Rais Kikwete ni nguvu za soda tu zisizotamba mbele ya Josephine ambaye alionyesha udhitibi na umwamba wake hadharani leo.

Lakini tukio la leo pia limethibitisha kwa mara nyingine kiwango cha kinyogo ambacho familia ya Slaa na mchumba wake wanayo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kikwete tokea Rais alipowabwaga na kumsambaratisha kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka juzi, 2010.

Tokea wakati huo, Mheshimiwa Slaa hajapata kumsema vizuri Rais Kikwete, hajapata hata kumtambua hadharani pamoja na kujua kuwa alishindwa kihalali, hajapata kumsalimia wala kumpa Kiongozi huyo wa nchi mkono hadharani hata fursa inapojitokeza kama leo.
Kwa ufupi, tukio la leo na mengine mengi yalimtangulia limethibitisha kuwa Mheshimiwa Slaa ni kiongozi mwenye kinyongo na asiyekuwa na heshima kabisa.

Kama ambavyo wamepata kusema wengine hana sifa za kuwa na kiongozi mkuu wa nchi yetu hii inayoongozwa kwa misingi ya maelewano na siyo kwa misingi ya chuki ambazo anazionyesha Mheshimiwa Slaa. Kwa hili Dr. Slaa Kachemsha, kadhihirisha wazi kuwa hana siyo tu ukomavu wa uongozi bali pia ukomavu wa kisiasa. Sasa naelewa pia kwa nini Slaa upadre ulimshinda.

Ni jambo la ajabu kuwa mfiwa kama alivyokuwa Slaa leo kwa sababu yeye amempoteza Mbunge anakataa vipi kwenda kumsalimia mwombolezaji ambaye amekwenda kumpa pole na kumjulia hali. Huu ni ubinadamu na uungwana kweli?

Mzee Slaa anashindwa na wadogo zake kama vile Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambao walipeana mikono na kukaa pamoja na Mheshimiwa Rais, kubadilishana mawazo na kuomboleza kwa pamoja.

Imetumwa na
Mtanzania mkweli
Naomba kuwasilisha.



Tupe maoni yako

10 comments:

  1. asante sana kijana umetupa ukweli na heshima yako ni kubwa katika fani ya siasa na upatikanaji wa haki.Endelea utupashe na ukweli utandike mtandaoni.

    ReplyDelete
    Replies
    1. pole sana, nadhani nawe pia hufanyi utafiti kabla ya kuongea, no research no right to speak

      Delete
  2. Nikiwa msomaji mzuri wa BLOG hii, katu sijapendezewa na habari hii iliyojaa unafiki na kusheheni itikadi ya siasa.Sengo nakushauri siyo kila habari inayotumwa kwako ni budi ui-post habari kama hii haijengi bali inabomoa.
    huyu mtoa habari hii anauthibitisho gani wa hayo aliyosema kuhusu Slaa na mke wake?

    ReplyDelete
  3. jamani mbona slaa amejibu kwenye gazeti la mwananchi la elo, you would be so logical kama utaiweka na hiyo post ili watu wasome waone ukweli... unless otherwise nithisi either wewe G ama mtuma mada anatumiwa na watu fulani

    mimi pia i was among of the people who were so anxious kujua kwa nini Slaa amkimbie JK but alipotoa majibu nimemuelewa

    tuweke siasa pembeni tutafute ukweli

    ReplyDelete
  4. Sikutegemea kama ningekutana na habari ya namna hii katika blog yako kaka, mimi ni msomaji wako na nilivutiwa na habari za kanda ya ziwa nyumbani amabako mimi sipo kwa muda.
    lakini unapotoa habari za kishabiki na kidaku kwa kiwango hiki unahudhunisha wasomaji.

    Chukua hatua juu ya hili, na utuombe radhi kwa kutukera.

    ReplyDelete
  5. Marafiki aka wadau, Taarifa hii nimetumiwa hivyo mwandishi si mimi kajitambulisha mwishoni mwa taarifa, by the way sisimami kwaajili ya chama fulani 'kulia au kushoto' bali naisimamia haki na burudani iliyo kweli.... Wadau eeeeh ukweli hata mimi ninautafuta....na nikiupata nitawatonya.

    Wasalaam.

    ReplyDelete
  6. hii ni blog yako na wewe ndo last editor..mambo ya kinafiki na kiuwendawazimu kama haya unaweza kuyachuja kabla ujapost hapa...huu ni uendawazimu ambao hata mtoto mdogo ataushangaa..simply..uchochezi na uchizi

    ReplyDelete
  7. YAANI KATIKA MAMBO YOTE PALE MSIBANI ULICHOONA NI SLAA KUTOMPA MKONO KIKWETE. NAHISI WAKATI WATU WANALIA ULIKUA UNAWATAZAMA USONI KAMA WANA MACHOZI. HII INAONYESHA UVIVU WA FIKRA NA MAADILI. YAANI MFIWA AMFATE ALIYEKUJA KUMPA POLE MKONO? TUAMBIE UTAMADUNI WA WAPI HUO.

    ReplyDelete
  8. Yaani watu wanauchadema hadi humu!! Yaani kosa kusemwa slaa tu eti aombe msamaha kwa kumchana slaa, mbona wafupi wa fikra jamanii, hawa wanasiasa ni wafanyabiashara na wanajua saana hawana lolote wengine huku mnabakia washabiki maandazi, sasa nshajua sababu ya chadema kuwa na katabia ka kuzilazila kila kitu, imesababishwa na mashabiki kama hawa wanaodai waombwe msamaha na kuona mwenye blog ni mnafiki, wee kama habari haijakuvutia potezea, mnamshambulia kaka wa watu hata hamsomi hadi mwisho muone muandishi ni nani,, inaonesha hata darasani mlikuwa mkifeli kwa kutofata instruction….gsengo hata usiache kutupa habari wee toa za kila dizaini kwani huwezi kuwafurahisha wote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani mwandishi wa habari hiyo ndiye aliyeipost katika page ya blog hii???

      kwani habari inapofika mezani kwa editor wa blog haifanyiwi editing ili iwe na maana?

      kwani blog hii haina Theme yake kama chombo cha habari???

      kwani G sengo ana ruhusu kuonekana chochote kile eti kwakuwa hakukitengeneza yeye???

      kwani Slaa alisalimiana na wote pale msibani isipokuwa rais peke yake??

      kwani haikurepotiwa na blog hii mwanzo kabla haijarudiwa tena kinafiki na kidaku???

      hebu nijibu msomi wewe unayeweza kufurahia hata picha ya uchi katika blog hii na usimlaumu bloger husika ili tu uonekane MSOMI na ULIFAURU vizuri sana mitihani yako katika hiyo shule ya kata uliyosomea.

      Delete

Note: Only a member of this blog may post a comment.