ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 14, 2012

BREAKING NEWS: AJALI YAPOTEZA MAISHA YA MBUNGE WA CHADEMA REGINA MTEMA

REGINA MTEMA ENZI ZA UHAI WAKE.
Habari tunazozipata hivi sasa kutoka vyanzo vya ndani ya CHADEMA zinamtaja aliyekuwa Mwanaharakati shupavu Mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA jimbo la Morogoro Regina Mtema kuwa amefariki dunia kupitia ajali mbaya ya gari iliyotokea leo katika eneo la daraja la Ruvu akiwa safarini kutokea jijini Dar es salaam kuelekea mkoani Morogoro. Bi. Mtema alikuwa na familia yake akiwemo mama yake mzazi. Majeruhi wote wamepelekwa kwenye Hospitali ya Tumbi, kibaha-Pwani.Habari hizi zinatukuta tukiwa kikaoni.
Katika kumuenzi mbunge huyo Wanachama wa chama cha wandishi wahabari mkoa wa Mwanza (MPC) walisimama kwa muda wa dakika moja.

BLOGU HII INAUNGANA NA WALE WOTE WAZALENDO WALIOGUSWA.
MWENYEZI MUNGU ILAZE ROHO YA MAREHEMU REGINA MTEMA MAHALI PEMA PEPONI AMEN.
Habari zaidi tutaendelea kupashana.

Tupe maoni yako

3 comments:

  1. Mungu ailaze mahali pema peponi...na tunatoa pole kwa Chama Cha CHADEMA na wanachama wake wote pamoja na watanzania wote kwa ujumla. JAMES LS URASA

    ReplyDelete
  2. Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi...na tunatoa pole kwa Chama Cha CHADEMA na wanachama wake wote pamoja na watanzania wote kwa ujumla.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.