ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 14, 2011

MIAKA 12 TANGU MWALIMU ATUTOKE

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka kifo kinamchukuwa ameacha vita ya wale maadui watatu ambao ni njaa, ujinga, umasikini. Ni miaka 12 sasa tangu alipotutoka nalo Taifa la Tanzania mwaka huu 2011 linakwenda sherehekea miaka yake 50 ya Uhuru likiwa na changamoto za kumwaga mpaka mchafuko wa kichefuchefu kwa kila siku tukibadili santuli za skendo.

Sasa kila mtu anavuna raslimali za taifa hili kadri anavyoweza, daraja kati ya masikini na tajiri linaongezeka urefu, huku masikini akiendelea kutwishwa mzigo wa ugumu ya maisha kila kukicha..... Nani kasema Tanzania ina amani? Watu wametulia tu, wananchi wana njaa, maisha magumu, bidhaa tunazozalisha wenyewe zinauzwa mara tano ya bei inayopaswa na pesa ya ongezeko inaenda kwa ‘mamasta plani’ wachache twawaita 'mafisadi', Amaniiiiii wakati Shida imekuwa wimbo wa taifa, halafu utasema huyo mtu ana amani kweli?

Nenda Mwalimu!, Nenda! Nasema Nenda kwani nahisi kuna jambo laja nami sitaki uweshuhuda ila sijajuwa litakuwa la faraja au huzuni …….

Inshahlah Mwenyezi Mungu ndiye ngome yetu.

Naomba kuwasilisha....!!!

POLISI WASAKA MADAKTARI WALIOTEKWA KENYA

Polisi wakitumia helikopta na magari wanawasaka watu watu wenye silaha waliowateka nyara madaktari wawili wa Uhispania wanaofanya kazi na shirika la misaada la Medicins Sans Frontiers (MSF) karibu na mpaka na Somalia nchini Kenya.

Wawili hao walitekwa katika kambi ya wakimbizi ya Daadab, ambayo inawahifadhi maelfu ya wakimbizi wanaokimbia njaa katika Pembe ya Afrika.

Taarifa zinazohusianasomalia, kenya, ulayaDereva wao, raia wa Kenya, alijeruhiwa na sasa amepelekwa hospitali, limesema shirika la MSF.


Katika wiki za hivi karibuni, wanawake wawili, mmoja raia wa Uingereza na mwingine Mfaransa walitekwa karibu na mpaka huo.

Mwandishi wa BBC Bashkash Jugsodaay akiwa kaskazini mwa Kenya anasema mikakati kabambe inafanywa kuwa saka watekaji nyara hao.

"Asubuhi ya leo wafanyakazi wa MSF walipatwa na tatizo huko Daadab"
MSF imethibitisha kupotea kwa madaktari wake raia wa Ulaya wawili, na wametoa taafifa fupi.


Chanzo: bbc swahili.

TANZANIA-2-DENMARK LIVE tour


About Mzungu Kichaa:
Mzungu Kichaa took East Africa by storm with his first music video Jitolee. After releasing his debut album in 2009 he won an African Achievement Award at a prestigious award ceremony organised by the African Diaspora in Scandinavia. Through his influence on the Tanzanian music scene Mzungu Kichaa was selected as a judge for the last edition of the televised talent show Bongo Star Search.

About Fid Q:
Fid Q is the most featured and respected rapper in Tanzania. With countless awards and prolific appearances on the live scene Fid Q is without a doubt the king of Tanzanian hip-hop. His flow and ability to relate to his audiences everywhere in the world has dubbed him the swagger don - the father of swagger. His sound is creative, both lyrically and musically, fusing sounds from jazz, taarab and neo soul. Fid Q hosts "free style friday", a new TV show broadcoast in Tanzania and online through www.cheusidawa.tv. He will be doing a feature piece about his DK tour, so keep an eye out for that.

Thursday, October 13, 2011

KESHO NI KUMBUKUMBU YA BABA WA TAIFA


This is The GREATEST MAN i have Ever KNOWN , May He Rest In PIECE

TAARIFA YA MAZISHI YA MAREHEMU MZEE SAIDI MUHAMMAD SIKAMKONO KUFANYIKA LEO

Rejea taarifa ya msiba wa Mzee Said Muhammad Sikamkono mazishi yatafanyika Leo tarehe 13/10/2011 katika makaburi ya Hainalt Garden of Peace saa nane mchana. Ila kabla ya makaburini tunaombwa wote tufike msikiti wa Sakina Walthamstaw (basi namba 179) saa sita na nusu mchana. Msiba uko nyumbani kwa marehemu Woolwich Dorkyard ambako wote tunakaribisha muda wowote kujumuika na familia ya marehemu wakati huu wa majonzi .Wakina mama pia wanaweza kufika msikitini au nyumbani kwa marehemu kwa ajili ya kutoa pole.

Address ya sehemu ya msiba ni;
Woolwich Ferry
405,Frances Street, London.
SE18 5JU.

Kwa maelezo zaidi tafadhali wasiliana na;
07813539025 - Haruna mbeyu.Katibu Jumuiya ya Watanzania -london
07766454596 - Abdallah Mdidi

MBUNGE WA MVOMERO AMOS MAKALLA ATEMBELEA ENEO LA MGOGORO WA ARDHI KINYENZE

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla (wenye suti) akiangalia uzio uliowekwa na mwekezaji katika Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro na kuziba njia inayokwenda katika mtaa wa Mwanga na katika mashamba.

Pia mwekezaji huyo raia wa kigeni amechukua sehemu ya mashamba ya wananchi hao bila ya taarifa
yeyote kwa Halamashauri ya Kijiji na wananchi.

Mbunge wa Jimbo la Mvomero, Amos Makalla (kulia) akiwa na kijana Hamis Maguo, alipotembelea hivi karibuni Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, kufuatilia mgogoro kati ya wananchi wa Kijiji hicho na mwekezaji.


Mnyetishaji: www.mrokim.blogspot.com

Wednesday, October 12, 2011

GARI LINAUZWA...

Kwa nje.

Kwa ndani..

Aina ya gari
Toyota surf(SSR)
Engine-2L
manual gear+4wd drive
Bei 10milioni
PIGA sasa 0714 198500

KESI YA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI WILAYA YA ILEMELA MWANZA KUUNGURUMA OCT 17.

Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi jimbo la Ilemela ambayo yalimpa ushindi mbunge Highness Samson (CHADEMA) dhidi ya Anthony Diallo (CCM), itaanza kuunguruma Oktoba 17 mwaka huu (2011).

Hadi kufikia Desemba 10, mwaka jana (ikiwa ni miezi miwili baada ya uchaguzi), kesi 43 zilikuwa zimefunguliwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda za Mbeya, Dar es Salaam, Sumbawanga, Dodoma, Moshi, Tabora, Mwanza, Bukoba, Iringa, Mtwara na Arusha.

Tukutane siku ya kesi wapendwa.

H.BABA&FLORA MVUNGI KUJA NA MUVI LA KISUKUMA

Ni Bush Star Search: Ndani ya kijiji cha Bujora kulikuwa na Mwanadada maarufu anayetikisa na kusumbua katika sanaa za aina zote iwe ni ngoma, maigizo, kuimba, sarakasi alikuwa juu sana hata wanakijiji walikuwa wakimwaminia. Ukaguzi wa Bush Star Search ulipotia timu kijijini Bujora kutafuta vipaji mwanadada huyo alionyesha kila aina ya kipaji alichokuwanacho lakini laaa!! Majaji wakamtosa!
-OOh Mie najuwa kuimba – Akaimba Hola huna kipaji!!
-Mie najuwa kucheza - Akacheza ngoma Hola huna kipaji!!!!!
-Akafanya Manjonjo yote ….Huna kipaji!!!!!
Mwisho wa siku majaji wakamwambia
“dada ungeondoka tu mahala hapa, huna kipaji cha sanaa aina yoyote ile na hata katika wale kumi tunaowahitaji HAUMO!”
Dada akauliza “sasa nyie mnataka nini kwani kama ni sanaaa uliza watu wote wananifahamu hapa kijijini?” na mshindi wa kwanza kiongozi yaani Chief alitenga ng’ombe 12 kama asili ya watu kabila la Sukuma hivyo washiriki wote wakajishughulisha kutwaa zawadi hiyo.

Dada alipokataliwa akaweka kinyongo na kwenda kushtaki kwa bibi yake ambaye alikuwa mtaalam wa kucheza na vibuyu. Bibi akamwambia omba mizimu utakalo, Dada akaiomba mizimu….

Siku wale Top Ten wanaondoka dada akawaambia majaji “Kama nyie ni wajanja basi tuone kama mjini mtafika….." HAPO NDIPO SHESHE NA BALAAA LINAPOANZA.... ISUBIRI MUVI INAITWA 'BUJORA'

NYERERE DAY 2011 IN Washington DC

Maadhimisho ya nne ya kuenzi maisha na kazi za Mwl Julius K. Nyerere yatafanyika Oktoba 15, 2011 hapa Washington DC. Mmoja wa waasisi wa Julius Nyerere Comemoration Bwn Rick Tingling akielezea maandalizi ya siku hiyo katika video hapa chini
NYOTE MNAKARIBISHWA
Itafanyika
Howard University Basement Auditorium
725, 2225 Georgia Ave, NW, Washington, DC 20059
FROM 3PM-6PM

MAELEKEZO KUELEKEA Howard University Hospital Basement Auditorium:
1.Ingilia mlango wa mbele wa Hospitali unaotazamana na Georgia Avenue.
2.Pita kwenye dawati la maelezo kwa utambulisho
3.Endelea mbele mpaka kwenye "lift" zilizo kama yadi 50 toka dawati la mapokezi.
4.Chukua "lift" / elevator kuelekea sakafu ya chini (basement).
5.Elekea upande wa kulia ukifuata alama zinazoelekeza ulipo ukumbi.
AMBATANISHO: MAELEZO KUHUSU MAADHIMISHO HAYO.
NOTE: Mabadiliko pekee niliyojulishwa ni kuwa Balozi Mwanaidi Maajar hataweza kuhudhuria kwa kuwa atakuwa nje ya mji.

BARAKA KWAKO NA ASANTE KWA USHIRIKIANO

http://www.changamotoyetu.blogspot.com
http://www.youtube.com/user/mutwiba

TAARIFA ; NAOMBA KUWASILISHA....


TAARIFA YA MABADILIKO YA MTANDAO WA MATUKIO NA WANAVYUO.
Sasa Blog hii imeungana na wanavyuo watanzania wanaosoma nje ya Tanzania Kwanza kabisa tunapenda kuwasalimu wadau wote popote Duniani,tunatumaini ya kwamba bado mnaendelea na ujenzi wa taifa letu.

Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapa taarifa kwamba mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo www.tzwanavyuo.blogspot.com sasa tumefanya mabadiliko makubwa ambapo tumewaunganisha wanavyuo watanzania wanaosoma Tanzania na walio Nje ya Tanzania, Tumefanya hivi kutokana na malalamiko na maombi ya Wanavyuo waliopo nje ya tanzania kutaka kuanza kutuma matukio yao ambayo yanajili huko waliko, Tumelipokea ombi hili na sasa mwanachuo yeyote ataweza kutuma habari zake ama habari zao hapa.

Pia kwa watumishi wa vyuo Hapa nchini Tanzania mnakaribishwa sana kuleta matangazo yenu ikiwa ni nafasi za masomo ama kama kuna habari ya haraka mnataka iwafikie wanafunzi basi mtutumie moja kwa moja nasi tutaiweka muda huo huo.

Mabadiliko mengine tuliyo yafanya kwa faida ya watu wote ni kwamba sasa tuna panel upande wa kulia ambapo tumeorodhesha tovuti za vyuo vyote vya Tanzania,pia tumeweka na mambo mengine mengi ya msingi ambayo yatapata kuwasaidia.

Mtandao wa wanafunzi ambao unafanya kazi kama Facebook (Social network)upo hewani mnakaribishwa kujiunga www.tzuniversitiesconnects.tk mnakaribishwa sana pia mtakutana na wanavyuo wengine.Tunatanguliza shukrani zetu za Dhati.

Tumumie matukio na habari zozote zihusuzo vyuo hapa: twanavyuo@live.com
Tembelea Mtandao wa Matukio na wanavyuo hapa: www.tzwanavyuo.blogspot.com

Kwa niaba ya wanavyuo wote,
Matukio na wanavyuo Crew.

Tuesday, October 11, 2011

TANZANIA BWANA KILA KONA FULL UTALII...!!!!

Katika pozi Masupa staa wa kesho.

Kwetu pazuri..

Kwetu pazuri bwana part two.

Hara ya kwetu 'mgeni kuchinjiwa kuku' na wakiwa wengi twaita 'vyuku'

Biashara ya kabeji eneo la Lamadi barabara ya kuelekea Musoma.

Mazingira na maji ya pembezoni mwa ziwa Victoria.

Kisiwa:- kitu ndani ya kitu.

Mv Misungwi ku-mayi.

DUKA LA KUUZA NA KUNUNUA HILI HAPA....


KARIBU DUKA LAKO (DUKA LA KUUZA NA KUNUNUA)
Habari za leo Mabibi na Mabwana... Ni matumaini yetu nyote mu wazima. Tunapenda kuchukua nafasi hii ya pekee kabisa kuwakaribisha sana katika mtandao huu wa kipekee,kisasa na waina yake ambapo mmiliki wa mtandao huu sio sisi lakini ni wewe ndio maana ukaitwa DUKA LA KUUZA NA KUNUNUA. www.dukalako.blogspot.com . Duka lako ni mtandao ambao umetengenezwa kwa nia na madhumuni ya kukurahisishia wewe mfanya biashara mtanzania popote pale Duniani, au wewe mtu binafsi kuweza kununua au kuuza bidhaa yako yoyote ile kupitia mtandao huu wa DUKA LA KUUZA NA KUNUNUA. Bidhaa hizo ni pamoja na Computers,Simu za mkononi,vifaa vya majumbani, Vifaa vinginevyo mbali mbali, Magari nyumba na kitu chochote ambacho unataka kukiuza kiwe ni kipya au chazamani utaweza kukiweka hapa na kitauzwa moja kwa moja. Kama ni Second hand mwenye mali atatakiwa kusema kabisa.

Yafuatayo ni maelezo ya jinsi ya kutumia mtandao huu:
1. Hii ni fursa ya mtu yoyote yule anaetaka kuweka bidhaa yake ipate kuuzwa na kununuliwa hapa,ndio maana ikaitwa Duka lako(Duka la kuuza na kununua). Utatakiwa utume bidhaa yako ukiambatanisha na bei zako pia mawasiliano ya barua pepe ama namba yako ya simu.

2. Ni muhimu unapo leta bidhaa yako iwe ni picha halisia kabisa ambayo umepiga wewe mwenyewe na sio ambayo umeitoa Google ili kuepusha usumbufu wakati unawasiliana na mteja wako anaetaka kununua bidhaa hizo.

3. Mtu anaetakiwa kuweka bidhaa hapa anatakiwa aweke specification ya bidhaa yake kama zipo mfano Kompyuta,simu na vitu ambavyo vitahitajika kuweka maelezo yake, atatakiwa kifanya hivyo ili kumrahisishia mteja wake kufanya maamuzi yaliyo sahihi na ikumbukwe kwamba duka hili ni lako wewe ambae utaweka bidhaa zako hapa.

4. Kwa wafanya biashara ambao wanamiliki tovuti za makampuni yao tunawaomba sana mtuwekee na link za tovuti zenu ili mtu akiingia apate kuona zadi kuna nini ndani ya duka lako.

5. Katika kuweka Bidhaa hizo katika duka Lako mteja atachangia kiasi kidogo cha fedha ili kuendeleza ufanisi wa kazi zetu,pia atatangaziwa bidhaa zake katika njia mbali mbali.

6. Tunaomba Baada ya mteja kupata mteja na bidhaa yake kuuzwa awasiliane nasi ili tuweze kuitoa bidhaa hiyo na kuwapisha wengine wanao weka bidhaa zaidi.

Wateja wetu kumi wa kwanza ambao tutapata barua pepe zao kupitia (dukalako@live.com) baada ya kumaliza kusoma hapa, watauza bidhaa zao hapa Bure kabisa kwa muda wa wiki moja kuanzia leo, kuwa wa kwanza sasa kuweka bidhaa yako hapa na kuuza na kupata wateja mapema iwezekanavyo. tunawahakikishia kuwa kwa njia hii mtaweza kuuza vitu vyenu kwa haraka na uhakika zaidi. kwa maelezo zaidi na kuona zaidi Tembelea Duka lako sasa. Tunatanguliza shukrani zetu pia ukiona hii mwambie na mwenzako pia asipitwe na Duka hili muhimu kabisa kwa watanzania wote popote Duniani.

Tuma Bidhaa zako kupitia Barua Pepe: dukalako@live.com
Wasiliana nasi kabla ya kutuma bidhaa au baada ya kutuma bidhaa kupitia namba ya simu hizo chini:
+255 762039028 au +255 714233895

Tembelea Duka hili hapa: www.dukalako.blogspot.com

CHEREKO LA SENDOFF YA NEEMA LAFANA..

Ni sendoff ya Bi.Neema iliyofanyika siku ya jumatano jijini Dar es salaam katika ukumbi wa New Sinza delux.

Bi.Neema akiwa na mtarajiwa wake Bw. Humphrey Simon.

Waalikwa wakikwaitika.

Hapa jeh!

Meza maalum.

Ngoma zetu shughulini...

Bwana Harusi mtarajiwa kulia akiwa na mpambe wake 'menyuni'.

Kamati ya Sendoff na binti yao.

Monday, October 10, 2011

EPIBAZDEI MTOTO FAITH.....

Keki ilivyokuwa.

'Happy birthday dear Faith ...... Happy Birthday 2U'

Kwasababu ni siku ya furaha Faith aliona vyema kujumuika na marafiki zake kusherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Faith akiwa na mama yake mzazi Jacky.

Blogu hii inakutakia kila la kheri mtoto Faith katika maisha yako, Mungu akutunze akulinde na pia ikamate elimu.

MOTO WA WOKOVU ULIPOWASHWA NA NEW LIFE BAND VIWANJA VYA FURAHISHA MWANZA

Chungulia VIDEO hii ujionee jinsi shangwe zilivyotawala kila kona.
Jana ilikuwa siku nzuri kwa wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake kwani walikusanyika katika viwanja vya Furahisha kuimba na kuabudu.
New Life Band kutoka Arusha wakishirikiana na Vijana waimbaji wa makanisa mbalimbali Mwanza walijumuika pamoja katika hili nakuzipaza sauti zao.
Mashuhuda toka pande mbalimbali walihudhuria tukio hili jema.
Moto usio zimika uliwashwa......
Ukashika kila pande nao vijana wakapaza sauti zao kumsifu mungu.

Kiongozi wa New life Band akitoa shukurani kwa viongozi wa Makanisa walioshiriki kufanikisha tukio hilo la kipekee.

UWT NYAMANORO MWANZA WAZINDUA MFUKO WA KUWEKA NA KUKOPA.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Bw. Clement Mabina akizindua katiba ya UWT mfuko wa kuweka na kukopa katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa PK jijini Mwanza.

Katiba tuliyoizindua ndiyo hii..

Mh. Mabina akisoma muhtasari wa baadhi ya vipengere vilivyomo kwenye katiba.

Katibu msaidizi wa UWT Mwanza akisoma taarifa fupi kuhusu azimio la mfuko huo.

Katibu wa CCM kata ya Nyamanoro Bw. Mtoro akikabidhisha mchango wake na wadau wa idara yake kuuboresha mfuko wa UWT Nyamanoro Mwanza.

Kupitia mfuko huo akinamama watakuwa na uwezo wa kukopa kwa riba nafuu hivyo kuweza kujikwamua na harakati za maendeleo na umasikini zinazowakabili.

Hongera akinamama kwani Kupitia vikundi kama hivi mtakuwa mnajitengenezea njia kupata unafuu wa mikopo toka kwa asasi nyingine za kifedha hivyo kuboresha mifuko yenu ya kukopeshana kwa maendeleo.