ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, August 13, 2011

TOTO AFRICANS YARAMBA DUME

Timu ya Toto Africans ya jijini Mwanza leo imeingia mkataba maalum wenye jumla ya thamani ya shilingi za kitanzania milioni 48 wenye nia ya kuboresha soka lake na Jarida maalum la kimichezo la 4:4:2 Jarida la Mabingwa ambalo litakuwa likitolewa mara moja kwa mwezi likiandika na kutangaza habari za michezo za ndani ya nchi na zile za kimataifa.

Timu ya Toto katika udhamini huo imepatiwa jezi mpya, track 40 na jaketi zake, bips 30 kwaajili ya mazoezi pia timu hiyo itanufaika kupewa kurasa mbili kutoka katika jarida la 4:4:2 zitakazokuwa na thamani ya Sh.32, 400,000 katika kipindi cha miezi 12, mipira 12 yenye thamani ya Sh.250,000 na Sh. 500,000 kwa ajili ya kuwawezesha waandishi wa habari.

Mkurugenzi msaidizi wa Jarida la 4,4,2 Mutanin Yangwe akitia saini mkataba huo wenye jumla ya thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 48 kwa timu ya Toto Africans.

Katibu mkuu wa timu ya Toto Africans Salum Kaguna akitia saini mkataba huo wenye jumla ya thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 48 kwa timu ya Toto Africans.

Mikataba ikidhihirishwa kwa Wandishi wa Habari.

Viongozi wa timu ya Toto Africans pamoja na wadau wa Jarida la 4:4:2 wakipitia kurasa moja baada ya nyingine kwa mfano wa chapisho la kwanza la gazeti hilo la Mabingwa lenye mikakati ya kuinua na kukuza soka la Toto, Mwanza na Nchi kwa ujumla.


Mambo mengine ambayo Toto itanufaika nayo kupitia mkataba huo ni pamoja na kupata ufadhili wa Sh. Milioni 7 zitakazoiwezesha kulipia kodi za nyumba kwa wachezaji wake, katika kipindi cha miezi 12 ambapo upangaji huo kwa mujibu wa Yangwe utakuwa ni wa kuanzia Agosti 15 mwaka huu.

4:4:2 CREW.
“Niwashukuru sana wenzetu hawa kutoka 4:4:2 magazine ambao kweli wameonyesha moyo wa upendo kuamua kuja kutusaidia, hii ni faraja kubwa kwetu, ikizingatiwa kuwa tulikuwa na hali mbaya, na sisi tutawahakikishia kuwa tutawapa ushirikiano ili kuhakikisha kuwa timu yetu inafanya vizuri katika mechi zinazokuja za ligi kuu na nitumie fursa hii kuwaomba wanamichezo na wafadhili wengine waige mfano huu wa wenzetu ili waisaidie timu yetu”,alisema katibu mkuu wa Toto Africans Salum Kaguna.

"NGOSHA THE SWAGA DON AUGUST 13' IS YA DAY"

Leo ni siku ya kumbukumbu kwenye familia ya Mzee Kubanda na familia ya wana Mwanza-Mwanza hali kadhalika familia ya wapenda Hip hop wanaharakati nchini kote hata nje ya mipaka pia, kwaaaanii.. Fid Q aka 'Ngosha' siku ya leo asherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Blogu ya G.SENGO yasemaaaa:- A birthday is just the first day of another 365-day journey around the sun. Enjoy the trip 'Hommie'...

JAWITAH i think you know warra i meen...

Friday, August 12, 2011

WIMBI LA MAJONZI LATANDA MAZISHI YA MWANDISHI WA HABARI RICHARD MASATU

Mke wa marehemu Richard Masatu ndani ya fikra nzito juu ya safari ya mwisho ya mumewe mara baada ya shughuli za mazishi kukamilika eneo la makaburi ya Mwisenge Msoma mjini.

Mwili wa marehemu Richard Masatu SINCE 1972-2011.

Mwenyekiti wa kamati ya maafa toka Chama cha waandishi wa habari mkoa wa Mwanza Bw. Fredrick Katulanda akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu.

Mwakilishi wa ITV mkoani Mara George Marato akitoa heshima zake za mwisho huku akiwa ameambatana na Peter Fabian toka MPC.

Mfanyabiashara maarufu jijini Mwanza Jack Fish akitoa heshima zake kwa mwili wa marehemu Richard Masatu.

Afisa utumishi wa Sahara Group Bwana Rafael Shilatu akitoa salamu za rambirambi kwa wafiwa.

Bibi wa marehemu akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu mjukuu wake.

Ripota wa RFA na Star Tv mkoani Mara ambaye pia ni katibu wa siasa na uenezi (CCM) Mkoa wa Mara Bw. Maximilan Ngesi akitoa shukurani na wasifu wa marehemu Richard Masatu.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananzengo Mwanza Bwana Makongoro akitoa neno la shukurani na salamu za rambirambi toka watu wa chama chake waishio Mwanza.

Safari kuelekea nyumba ya milele.

Mapaparazi wote kanda ya ziwa walimiminika eneo hili.

Marehemu akiingia nyumba yake ya milele.

Marafiki wa dhati wa marehemu Richard Masatu toka Chama Cha Nzengo Mwanza.

Ni marafiki wawakilishi toka chama cha MPC kushoto Ntemi Nyanda, James George na Mheshimiwa diwani mtarajiwa.

SehEmu ya Ummati uliojitokeza katika mazishi ya Richard Masatu aliye zaliwa tarehe 8/Dec/1972 na kufariki dunia tarehe 10/Aug/2011.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Thursday, August 11, 2011

CHUO KIKUU CHAFUNGWA SWAZILAND

Chuo kikuu cha Swaziland hakijafunguliwa kwa mwaka mpya wa masomo baada ya serikali kushindwa kutoa fedha za ada za wanafunzi.Mfalme Mswati iii
Chuo hicho kimetangaza kuwa hatua ya kusajili imesimamishwa na masomo kuahirishwa. Kiongozi wa jumuiya ya wanafunzi Pasika Dlamini alisema wanafunzi wengi hawakuhudhuria masomo baada ya tangazo hilo.

Nchi hiyo ina upungufu mkubwa wa fedha kiasi ambacho wiki iliyopita Afrika Kusini iliamua kuwapa mkopo wa dharura wa dola za kimarekani milioni 355 na tayari chuo hicho kimethibitisha kuwa fedha bado hazijafika kuwalipia ada wengi wa wanafunzi hao, hakikuweza kufunguliwa. " Tuliambiwa kuwa chuo hakitafunguliwa siku ya Jumatatu, kwasababu hamna pesa, " alisema Bw Dlamini.

Mwaka huu serikali ilisema itawafadhili takriban wanafunzi 300, kiwango kilichopungua sana ukilinganisha na wanafunzi 1,200 mwaka jana. Mapato ya Swaziland ya mwaka jana kutoka ushuru wa forodha wa kusini mwa Afrika- chanzo kikuu cha fedha nchini humo- kilishuka kwa asilimia 60.

Baada ya kukubaliana na mkopo, Afrika Kusini ilisistiza jirani yake mdogo lazima ifanye mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa. Mfalme Mswati III, mfalme pekee barani Afrika mwenye mamlaka kamili, ameshutumiwa kwa kuishi kwa ufahari na wake zake 13, huku watu wake wengi wakibaki maskini.

Pia kumekuwa na ripoti kuwa nchi hiyo, ambayo ina waathiriwa wengi wa virusi vya ukimwi dunaini, imepungukiwa na dawa za kufubaza ukimwi za ARV.

MWANDISHI RICHARD MASATU AUAWA!

TANZIA
MAREHEMU RICHARD MASATU
Imenichukua muda kuamini (zaidi ya saa 24), pengine hii ndiyo sababu ya kuchelewa kuwafahamisha kuwa Tasnia ya Habari Mwanza imepata pigo kubwa baada ya Mwandishi wake mahiri Richard Masatu ambaye pia alikuwa Mkurugenzi wa Gazeti la KASI MPYA kufariki Dunia akiwa anapatiwa Matibabu katika Hospitali ya Mkoa ya Sekou Toure.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa Marehemu amekufa kutokana na majeraha ya kushambuliwa na watu wasiojulikana. Kwa sasa mwili wake upo Hospitali ya Rufaa ya Bugando mara baada ya uchinguzi uliofanyika jana kwa zaidi ya saa kadhaa kutokana na kukutwa na majeraha ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali, chini ya Kidevu, jicho la kulia ikiwa na kupigwa na kitu kizito usoni upande wa kushoto.

Baada ya kukamilika kwa uchunguzi, mwili wa marehemu utaagawa kesho Ijumaa saa 3 asubuhi nyumbani kwake Nyakato na kisha kusafirishwa kwenda Bunda mkoani Mara kwa mazishi.
EWE MWENYEZI MUNGU MSIMAMIE MJA WAKO
AMEN.

AIRTEL YAENDELEA KUPANUA MAWASILIANO NA HUDUMA MPYA MSIMU WA RAMADHANI

•YAFUNGUA HUDUMA ZA MAWASILIANO KANYEZI RUKWA
•OFA YA RAMADHANI BADO INAENDELEA TUMA NENO RAMADHANI KWENDA 15322 SASA...

AGOSTI 11, 2011 Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea kukekeleza azimio lake la kutoa huduma bora na bei nafuu nchini kwa kuzindua huduma ya mwasilaino kanyezi mkonia Rukwa wiki hii.

Katika kauli iliyotolewa na Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema, “Airtel imedhamiria kutoa huduma bora na nafuu na kuongeza mtandao wake kwenye maeneo mengi ya mikoani ili kuwapati wateja wake huduma bora za mawasiliano vijijini na maeneo ya miji nchiniTanzania .

“Tunaamini huu ndio wakati muwafaka kuendelea kupanua huduma za mawasiliano mkoani Rukwa pamoja na vjiji vingine, Kuwepo kwa mtando wa mawasiliano Rukwa kutainua shughuli za uchumi na kusaidia wakazi wa Kanyezi na jamii ya Tanzania kwa ujumla” Aliongeza kusema Mmbando

Mmbando alisema Airtel itaendelea kupanua mtandao wake nchini mwaka huu na mkazo utawekwa kwa maeneo ya Vijijini na hasa maeneo ya mikoa ya Pwani, kusini na Mashariki ya Kati.

“Kadri tunavyopanua mtandao wetu ndivyo tunavyo guza jamii na watu tunaowaunganisha kwa kuongeza na kuboresha hali ya maisha kwa kuwezesha na kufanikisha mawasiliano,” alisema Mmbando

“Tunazo timu za wataalum mikoani ambazo zinafanya thathimini ya mara kwa mara, na kila kunapokuwa na mahitaji ya mtandao, itatekeleza inavyotakiwa,” alimalizia kusema Mmbando

Zaidi ya kupanua huduma za mawasiliano Airtel inawakumbusha wateja kuna ofa ya Msimu wa Ramadhani. Wateja wa Airtel wanaweza kujiunga katika huduma hii kwa kutuma neno RAMADHAN kwenda 15322 nakupata ,Mistari ya Kuran, Saa za Ibada ,mida ya kufunga na kufungua, kila siku. Utatozwa sh 500 tu kwa wiki.

Sambamba na hili pia wateja wanazawadiwa muda wa maongezi,sms pamoja na internet Bure kwa kuongeza salio tu kuanzia shilingi 1000 na kuendelea kila siku kuanzia kuanzia saa 5 usiku hadi saa 12 asubuhi. ONGEA USIKU KUCHA

Wateja wetu wa Rukwa sasa nanyi mnaweza kujiunga na huduma hii na kufurahia ofa ya Ramadhani pamoja na wateja wetu wote nchi nzima.




Wednesday, August 10, 2011

BAROW AKABIDHIWA RASMI VIATU NA SIRRO JEH! VITAMTOSHA VITAMPWAYA AU VITAMBANA??

Kamanda Liberatus Barow akizungumza na wandishi wa habari Mwanza mara baada ya kutambulishwa na aliyekuwa kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Simon Sirro.

Kamanda Barow ameahidi kusimamia suala la maadili katika jeshi la polisi, kuhakikisha wale anaowaongoza wanafuata sheria bila kushurutishwa akisema: "Na Baada ya kutoa kibanzi nitakwenda kutoa boriti nje ya jeshi la polisi kwani siwezi kubaki na boriti kibanzi kiko nje nitapanmbana na kibanzi kuisafisha nchi"

Fredrick Katulanda nae akachangia "Tafadhali usafishaji wa jeshi la polisi uwe wa dhati kwani tunaposema nyumba yenu ni chafu huku uvunguni kunatakataka na panya waliokufa juzi ugomvi ndipo unapoanza na hapo ndipo ushirikiano kati ya jeshi la polisi na waandishi unapotoweka na kugeuka kuwa uadui.....baadhi ya maafisa wanapanda vyeo mara 3,3 wengine ambao ni watendaji kazi wazuri kwa miaka sasa hola..wako pale pale kunanini au tuseme kubebana?.."

"Mimi bado nina mashaka makubwa juu ya uelewa wa watendaji wa jeshi la polisi na hasa suala linalolalamikiwa kila kukicha suala la maadili, jeshi la polisi lina mikakati gani kwa watendaji wake?" akaongeza; "Bangi, madawa ya kulevya aina mbalimbali, pombe haramu vyote vinapenya mahabusu jeh! polisi hawahusiki na hili?"

Aliyekuwa kamanda wa Mkoa wa Mwanza mpiganaji, Simon Sirro (kushoto) sasa anakwenda makao makuu ya jeshi la Polisi nchini kushika nafasi ya Venance Tossi kuendesha kikosi cha Oparesheni Maalum.
"Nitahakikisha divai ya zamani haiendi kwenye viriba vipya maana vitapasuka bali nitahakikisha divai mpya inakaa kwenye viriba vipya na yazamani viriba vya zamani."By Kamanda Barow.

Sehemu C' ya Waandishi wa habari toka vyombo mbalimbali nchini walio hudhuria utambulisho huo uliofanyika kwenye chumba cha mikutano ofisi za makao makuu ya jeshi la polisi mkoani Mwanza.

HAYA HAYA KWA WATEMBEAO... KAMA MIMI

Shimo hili lililo tengenezwa na wazee wa vyuma chakavu na kuwa shimo la hatari, lisilo kuwa na vielelezo vya tahadhari liko sehemu ya biashara lenye mapito kwa watu waaina mbalimbali katikati ya jiji la Mwanza eneo la salma cone. Kazi kwetu tutembeao kwa kukariri mazingira tukisoma magazeti na wavijimeseji vya fesi buku hala hala shimo na mguu...!! Dah huruma sipati picha kwa ndugu zangu wasioonana wenye uono hafifu..
AaaaaH! wahusika TAHADHALI .

HAPPY BIRTHDAY MUBELWA BANDIO

Salaam kwako ndugu yangu.
Natumai kuwa u-mzima na unaendelea vema na harakati za mapambano ya maisha.. Nami pia.
Sababu pekee ya wewe kupokea UJUMBE HUU BINAFSI siku hii ya leo ni kwa kuwa umekuwa sehemu ya maisha yangu ndani miezi 12 iliyopita ama zaidi. Hivyo ninapo sherehekea siku yangu ya kuzaliwa (Aug 10), napenda kuleta ujumbe huu mfupi wa SHUKRANI ZANGU ZA DHATI kwa namna ulivyoendelea kuwa mmoja wa wale wanaoyafanya maisha yangu kuwa yalivyo sasa. Iwe ni kwa MANENO, MATENDO ama MAWAZO yako.
Nathamini sana uwepo wako na nakuombea mafanikio katika kila lililo jema utendalo ila maisha yako yawe mfano mwema kwa wengine wengi.
Nikumbushe tu kwamba, katika maisha yetu na katika kila jambo tutendalo, "kuna anayetuona kwa mara ya kwanza na / ama mara ya mwisho" na swali ni kuwa TUNAMUACHA NA TASWIRA GANI KUHUSU SISI NA MAISHA YETU?
Unapendwa, Unakumbukwa na UNAOMBEWA MEMA
ASANTE KWA KUWA ULIVYO

http://www.changamotoyetu.blogspot.com/
http://www.youtube.com/user/mutwiba

ANATAFUTWA NA MWAJIRI WAKE

Jamaa anaye tambulika kwa jina la Juma Hemed Hamisi (pichani)anatafutwa na Jeshi la polisi mara baada ya kutoweka na kiasi cha pesa shilingi za kenya 115,000/= (lakimoja kumi na tano elfu) sawa na shilingi za Tanzania 2,127,500/= (milioni mbili lakimoja na ishirini na saba elfu na miatano), pamoja na pesa taslimu za kitanzania shilingi laki tatu alizokabidhiwa kwaajili ya kufanya malipo mbalimbali.

Dreva Juma Hemed Hamisi inatajwa kuwa alipofika mpakani aliliitelekeza gari hilo lenye namba za usajili T106 ABQ roli aina ya Scania mali ya Lakairo Investiment likiwa na mizigo yake, akitokea nchini Kenya kuingia Tanzania.


Taarifa za tukio la kutoweka kusiko julikana kwa dreva huyo huku akiwa na mafungu ya watu yaani jumla ya fedha ikiwa ni shilingi milioni mbili laki nne ishirini na saba na mia tano, akimwacha mwajiri wake mdomo wazi asijuwe kisa na mkasa tayari zimeripotiwa kwa jeshi la polisi kupitia RB no MZN/RB/5347/11.

Roli lililotelekezwa tayari limekwisha fikishwa kwa mwenye mali mara baada ya dereva mwingine kuagizwa kulifuata mpakani. pichani likiwa kwenye karakana ya Lakairo Investiment, Mwaloni Kirumba jijini Mwanza

Tuesday, August 9, 2011

NYAMHONGOLO 8/8 MAMALIZIO HAYA FUNGA TWENDE

Kama kawa huteka umma ni kona ya biashara sampuli ya machinga dizaini.

Wakusoma.com mupooo!!!

Kona ya misonsomolo.com Mbuzi achomwa hadi moyo.

'Kwato ya ng'ombe ndani ya spoku za baiskeli yaingiaje?!!'

Hatimaye mwananchi huyo alimzaba kibao mnyama huyo hukumaneno yakimtoka "Li-Ng'ombe we!" Tehe'

Banda la Airtel maonyeshoni.

Hivi miwani tununuazo toka kwa wamachinga zinaubora kwa afya ya macho yetu?

Hizi Baiskeli sikuelewa ni mitumba au paking..?

Banda la Startimes maonyeshoni.