ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, May 7, 2011

MWANZA, SHINYANGA WAANZA VYEMA KILI TAIFA CUP KITUO CHA MWANZA.

Timu ya mkoa wa Mwanza.
Wenyeji wa michuano ya Kili Taifa Cup kituo cha Mwanza Herous leo wametumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuibamiza timu ya mkoa wa Kagera Rweru Eagles 2-1 mchezo uliochezwa kwenye dimba la CCM Kirumba.

Mabao ya Mwanza Herous yalipatikana katika kipindi cha kwanza, goli likifungwa na Malegesi Mwangwa (36), dakika 3 baadae ikaandika bao la pili kupitia winga wake machachari Jerison Tegete aliyefunga kwa ufundi mara baada ya kuwapiga vyenga mabeki wa Kagera na hatimaye kuukwamisha mpira kimiani.mkuu wa mkoa wa mwanza Abass Kandoro akisalimiana nae Jerison Tegete kabla ya mchezo baina ya Mwanza Herous na timu ya mkoa wa Kagera.

Kipindi cha pili dakika ya 62 Kagera wakapata goli kupitia mpira wa penati iliyofungwa na Juma Nade. Hadi kipindi cha mwisho Mwanza Herous 2, Kagera 1.

Mchezo wa pili baina ya timu ya Shinyanga wana Igembesabo na timu ya mkoa wa Mara umemalizika kwa Igembesabo kuishushia kipigo cha nguvu Mara, magoli 3-0 Mabao yakipatikana dakika ya 73 mfungaji akiwa Kulwa Mobby, dakika ya 78 Fabian James anafunga Bao la pili mara baaada ya mpira wa adhabu toka kwake Jackob Same na kumkuta mfungaji.

Dakika mbili baadae Shinyanga wanaongeza bao la tatu mfungaji akiwa ni yule yule Fabian James, hadi mwisho Shinyanga walitoka kifua mbele kwabao 3-0

Kikosi cha Shinyanga (Igembesabo)

Timu ya mkoa wa Mara.

Timu ya mkoa wa Kagera.
Kesho kutwa katika kituo hiki mchezo wa kwanza saa nane ni baina ya Kagera v/s Shinyanga na mchezo wa pili ni baina ya Mara v/s Mwanza.

WIKIEND HIYOOOOoooo!!

Club yako izalishayo maraha kila kukicha 'STONE CLUB' ya jijini Mwanza bila hiyana WIKI HII inakupa nafasi wewe na yule kudhuru jumba lake la maraha ambapo humo utashangweka kuondoa ma-stresi na karibisha amani ya mwili na akili. Zuka basi pande zile yaaani-yani-yani haina Majotro ariff yaani-yani-yani ni fulu Eisii'

sms by
'MEMBA WAUKWELI STONE CLUB'

TUZO ZA WANAMICHEZO BORA 2011 ZAFANYIKA : MWANAIDI HASSAN AIBUKA MWANAMICHEZO BORA WA JUMLA.

Mwanamichezo bora wa jumla wa Mwaka wa tuzo hizo Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa netiboli katika timu ya JKT Mbweni akipokea tuzo yake kutoka kwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Gharib Bilal.

Mchezaji wa timu ya Yanga Shadrack Nsajigwa akipokea tuzo yake mwanamichezo bora wa mpira wa miguu toka kwa Mkurugenzi wa bodi Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Mark Bomani.

Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa akipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal.

Wadau waalikwa Sekta ya Habari.

Kutoka kushoto Salehe Ali (Global Publishers) Ronard Sherukindo (Multichoice) na Kutoka kulia ni Phares Magesa makamu mwenyekiti wa TBF pamoja na mama mzazi wa Hasheem Thabeet anayecheza ligi ya NBA nchini Marekani.

Meza kuu ya viongozi walio hudhuria utoaji tuzo za Mwanamichezo bora 2011 ambazo zimedhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti tukio lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hotel ya Movenpick jijini Dar es salaam..

Wanalibeneke mashuhuri ndani ya shughuli shughulini ukianzia kulia ni Michuzi Jr wa 'JIACHIE' naye Bukuku wa 'FULL SHANGWE'.

picha zote kwa hisani ya FULL SHANGWE

Friday, May 6, 2011

TBL YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KITUO CHA MWANZA KWA MAANDALIZI YA KILI TAIFA CUP 2011.

Picha ya pamoja katika makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa ligi ya Kili Taifa Cup 2011 ambapo Muhib Kanu meneja timu ya Shinyanga IGEMBESABO (shoto), akipokea vifaa hivyo toka kwa Mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mwanza Jackson Songora (kati) na Ofisa Msimamizi wa mashindano hayo George Wakuganda toka TBL.

Meneja wa timu ya mkoa wa Mara, Chiganga Pascal (shoto) akipokea vifaa toka kwa Mwenyekiti wa chama cha soka mkoani Mwanza Jackson Songora, tayari kwa kuianza ligi ya Kili Taifa Cup 2011, makabidhiano yaliyofanyika leo katika ofisi za uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Jackson Songora akizungumza wakati wa sherehe za kukabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya Mashindano ya Kili Taifa Cup yanayoanza kesho katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Jumla ya timu nne za kituo hiki chenye timu toka mkoa wa Kagera, Mara, Shinyanga na Mwanza zimekabidhiwa vifaa hivyo tayari kushiriki michuano hiyo inayotaraji kuanza kutimua vumbi kuanzia kesho katika vituo vyote nchini.


(Picha na Mohamed Mambo)

THE LAST KING OF SCOTLAND AND THE DISTINCTIVE LOOK OF EVIL

The first time I saw a photo of Osama bin Laden after 9/11, I was taken aback and just stared with my mouth agape.

“I know, ” Sean replied to my silence, “He doesn’t look like the kind of man who would do this.”

“No, he doesn’t,” I said. He really didn’t. He looked peaceful. He looked grandfatherly. He looked like Gandhi. He looked very much like the way I picture Jesus.


Last week, Sean and I took advantage of Free Popcorn Night at the Lyric (aka Monday). We saw The Last King of Scotland. The film is about Uganda’s Idi Amin whose bloody reign killed an estimated 300,000. We both really enjoyed the movie and I continue to find it thought-provoking.

I believe the film excelled in depicting the initial appeal and charisma of Amin. You see him as jolly and happy, with such a big shining smile. You hear him with hearty laughs and watch him exchange jokes. You see his generosity. You see him as he empathizes with the residents of the smallest villages and as he inspires large crowds with his vision for Uganda.


Idi Amin smiling and holding a child. Stalin smiling and holding a child.

Even as you start to get exposed to his darker sides and his paranoia, it’s just hard to look at him and think he is capable of such evil. How can a man with such good humour and who smiles so bright bring about so much death and destruction, so much hate and heartache?

So many people live their lives as if there is a magic formula to identifying evil. If Skin Color is X. If Religion is Y. If Sexual Preference is Z. If they smoke cigarettes. If, gawd forbid, they like heavy metal music. If they ride a skate board. If they wear veils in front of the faces, if they wear black trenchcoats, or even, if they wear a police uniform. But you can’t weigh the quality of a man’s heart by looking at his exterior. There is no distinctive look of evil. It can can be peaceful and harmless looking. It can be vivacious and smiling. Evil can look like just about anything.

I found “The Last King of Scotland” to serve as a good reminder of that.

OUATTARA WA IVORY COAST KUAPISHWA.

Alassane Ouattara anatarajiwa kuapishwa kuwa Rais wa Ivory Coast na mtu ambaye mwanzo alimkatalia ushindi wake katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Novemba.

Mwezi Desemba, kiongozi wa baraza la katiba alimwidhinisha Laurent Gbagbo kuwa mshindi, iliyosababisha nafasi hiyo kushikiliwa naye kwa muda wa miezi minne.

Bw Gbagbo pia anatarajiwa kuhojiwa juu ya madai ya kukiuka haki za binadamu wakati akiwa madarakani.


Bw Alassane Ouattara

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa mawakili wake kutoka Ufaransa wamenyimwa ruhusa ya kuingia Ivory Coast ambapo shirika la habari la AFP limesema walizuiwa kwenye uwanja wa ndege wa Abidjan na kutiwa kwenye ndege iliyofuata na kurejeshwa Paris.

Wakati huo huo, Umoja wa Ulaya unatarajiwa kuipa nchi hiyo msaada wa zaidi ya dola za kimarekani milioni 60. Kamishna wa maendeleo wa Ulaya, Andris Piebalgs, ambaye yupo Ivory Coast, amesema inabidi waende kwa kasi.

Aliiambia BBC kuwa hali ilivyo nchini humo bado ina utata na kama maisha ya watu hayakuimarishwa haraka, ghasia zinaweza kuanza upya.

Alisema raia wa nchi hiyo wanahisi wamepoteza miaka 25 ya maendeleo kutokana na mapigano ya kisiasa na kikabila ya hivi karibuni.

Takriban watu 3,000 wanaaminiwa kuuawa wakati wa ghasia zilizotokea kwenye nchi inayozalisha kakao zaidi duniani, ambapo awali ilikuwa nchi yenye utajiri mkubwa Afrika magharibi.


kwa hisani ya bbc.

VIDEO SHOOTING

Kwaya ikitumia moja ya vivutio.
Rock City kuna vivutio vingi vya mazingira ya kitalii ambavyo bado havijatumika ipaswavyo hasa linapokuja suala la utengenezaji wa filamu za muziki.

Hata makazi yetu ni kivutio tosha.
Kwa wapiga picha wazuri fit kama hizi kwao ni thamani kubwa sana askwambie mtu.

Au pande hizi?.

Ama hapa kilimani karibu na fukwe za ziwa?
Waimbaji wengi jijini Mwanza wawe wa muziki wa Dini, Utamaduni au Dunia, wengi wamekuwa wakidiriki kujisumbua kubuni atifisho background ili tu kukamilisha picha zao tena wengine wakitumia gharama kubwa kutimiza hilo la kutengeneza ma-atifisho au kusafiri kwenda mikoa mingine. Sijui niseme kuwa hawaoni thamani ya walichonacho, au pengine kukariri shuting' za wasanii waliotoka au kuchukulia powa mazingira tuliyonayo? Yes! Zote hizi zaweza kuwa sababu.
"Tuwasaidieje...?"
Chunguza mjomba utabaini.

'UKISIKIA PAAaaa!!!'

Ukisikia paaa! ujue.....

Thursday, May 5, 2011

OBAMA : PICHA ZA OSAMA HAZICHAPISHWI

Wakati dunia ikiwa na usongo kuhakiki na kuipata sura kamili ya mwili wa jamaa aliyesakwa zaidi kuliko wote ulimwenguni (Osama Bin Laden), Rais Barack Obama ameamua kuwa picha za Osama Bin Laden, aliyeuwawa siku ya jumatatu, zisichapishwe.

Maafisa wa Marekani wamekuwa wakijadili iwapo wachapishe picha za mwili wa Bin Laden kukabili habari za uongo kuwa hakuuawa.

Lakini Bw Obama anaamini kuwa picha hizo huenda zikazua hisia kali akisema, '' sisi hatutaki kuonyesha picha hizi kama kikombe cha kujivunia cha kumwonyesha kila mtu."


Waandishi wa habari sambamba na wananchi wamekuwa wakifuatilia kwa saa 24 eneo yalipokuwa makazi ya Osama.

Kiongozi huyo wa al- Qaeda alipigwa risasi katika uvamizi jumatatu iliyopita na vikosi maalum vya Marekani, Kaskazini mwa Pakistan. Mwandishi wa BBC mjini Washington amesema kuwa rais Obama ameamua wazi kuwa kutoa picha hizo hazina thamani yeyote kwani huenda ikatishia maisha ya raia. Bw Obama amefichua uamuzi huo wakati wa mahojiano na kituo cha televisheni cha CBS.

Kutoka dirishani.
Uamuzi huo ulifikiwa wakati maafisa wa Marekani walianza kuchunguza habari kwenye kompyuta, simu za rununu na vifaa vingine vya kuhifadhi habari ambavyo vilipatikana wakati wa uvamizi huo katika eneo la Abbottabad, ambapo Bin Laden alikuwa amejificha.

Laini mbili za simu na euro 500 ($745; £450) zilipatikana zime shonelewa kwenye nguo ya Bin Laden, kana kwamba angehitajika kutoroka kwa haraka.

Mwanasheria mkuu wa Marekani Eric Holder amesema serikali hiyo inatarajia kuongeza majina mengine kwenye orodha ya magaidi wanaotakikana na Marekani, kufuatia habari walizopata katika nyumba ya Bin Laden.

Wakosoaji wameelezea wasiwasi wao kuhusu uhalali wa oparesheni hiyo, baada ya Marekani kubadilisha maelezo kuhusiana na kuuwawa wa Bin Laden akiwa ajajihami kwa silaha.


kwa hisani ya bbc swahili.

SAFARI YA MWISHO YA SOUND MAN WA ORIJINO KOMEDI ILIVYOKUWA

Mazishi ya Mtaalam wa sauti wa kundi maarufu la uchekeshaji nchini Mohamed Muya wa Orijino Komedi, aliyefariki hivi karibuni yamefanyika nyumbani kwao huko Korogwe mkoani Tanga na kuhudhuriwa na watu wengi wakiwemo ndugu jamaa na marafiki na wapenzi wa kipindi cha kundi hilo kinachorushwa TBC1.Wengi walihudhuria msiba huo kuhakiki habari zilizokuwa zimezagaa mtaani zikikanganya kwa wengi kupata habari kuwa mmoja wa wachekeshaji wa kundi hilo kaaga dunia huku wengine wakithubutu hata kutaja kwa majina.

Lakini kwa msada wa wahusika na TBC1 na redio kadhaa nchini walishiriki kutoa habari sahihi zikimtaja Sound man wa kundi hilo Mohamed Muya kuwa ndiye aliyefariki dunia.

Mwili wa marehemu uliwasili mjini Korogwe marafiki na wakazi wake kupata fursa ya kutoa salamu za rambirambi.

Akiwa na majonzi mazito mtoto wa marehemu Mohamed Muya aitwae Ommy (mdogo kuliko wote) akishuhudia safari ya mwisho ya baba yake.

Hapa ndipo alipolala ndugu yetu Mohamed Muya.
"Ewe Mola mpumzishe kwa amani kiumbe wako"
Amina.


HABARI ZAIDI TEMBELEA www.mkandamizaji.blogspot.com

JE! UNATAFUTA CHUOoooo?

Kibonzo by Dennis wa gazeti la Msanii Afrika.
CHAUKOLA=Chaga Univasiti Koleji Ofu Laifu.

CHEO MZIGO: MADIWANI MKOA WA MWANZA WAOMBA WAPEWE MISHAHARA KAMA WABUNGE.

Madiwani wa halmashauri zote za wilaya mkoani Mwanza wametoa kilio cho kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza kwamba aende kuwatetea kwenye ngazi za juu za maamuzi ili nao waanze kulipwa mishahara kama ilivyo kwa wabunge.Udiwani ni moja ya nafasi zilizo sakwa kwa kila hali na wagombea kipindi cha uchaguzi na kila mshindi alishangilia kama kaiona pepo 'kumbe...'

Kilio kilitolewa juzi na Mwenyekiti wa jumuiya ya Serikali za Mitaa (ALAT), mkoa wa Mwanza Bw. Benard Polycarp kwenye kikao cha kawaida cha jumuiya hiyo kilichoketi katika ukumbi wa jiji la Mwanza.

Polycarp alisema shughuli nyingi za maendeleo za halmashauri zimeshindwa kutekelezeka ipasavyo kwa vile fedha za ruzuku hazijafika kwenye halmashauri hivyo kusababisha shughuli nyingi kulala kwa vile serikali haina fedha.

Alisema wanajitahidi kuendesha halmashauri zao kwa kutumia fedha za vyanzo vya mapato lakini hazitoshi, hivyo alimuomba mkuu wa mkoa kusaidia kupiga kelele ili mafungu ya ruzukuyalipwe haraka kuziokoa halmashauri kujendesha.

“Mheshimiwa mkuu wa mkoa tunaomba utufikishie kilio chetu kwenye ngazi za juu husika tungependa nasi tulipwe mishahara kwa mwezi angalau sh.350,000 na zitambulike kama mshahara” alisema Polycarp.

Bw. Polycarp ambaye ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi na diwani wa kata ya Igekelo, alisema wananchi wengi kwenye maeneo yao wana kasumba ya kumwona diwani kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kifedha hivyo anaposhindwa kutekeleza majukumu kwa kukosa uwezeshwaji wanamhesabu kama mtu asiyejuwa majukumu yake, hivyo hafai.

UPO HAPO!...

ASUBUHI YA LEO

Jijini Mwanza leo kumekucha na hali fulani ya baridi, jua likishindwa kabisa kuchomoza kwa mawingu mazito kutanda na hatimaye mvua kunyesha mpaka time hii saa 11:35, mvua hiyooo ikitokea pande za Igoma yarejea tena.

Tuesday, May 3, 2011

KUTOKA KWA KAMANDA SIRRO LEO.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro.

ACHOMWA KISU KISA WIVU WA MAPENZI
Mnamo Tarehe 1/5/2011 majira ya saa moja usiku huko katika kijiji cha Buhama kata ya Nyakasasa wilayani Sengerema, mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la Deus Kasimu (25) amepoteza maisha mara baada ya kuchomwa kisu kwenye bega la kushoto na mtu aliyetambulika kwa jina la Maulid Mustapha.

Kisa cha tukio hilo kinatajwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Mtuhumiwa alikimbia mara baada ya kufanya uhalifu huo.


OPARESHENI WAUAJI.
Nacho kikosi cha Udhibiti mauaji yanayo shirikisha imani za ushirikina kilichoundwa hivi karibuni kanda ya ziwa na kuanza rasmi kazi siku ya jana ya tarehe 2/5/2011 kinaendelea kufanya kazi zake na majibu ya oparesheni hiyo yasema kuwa tayari watu zaidi ya 25 wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani mwanza kwa mahojiano.

Wilaya zinazohusishwa na Oparesheni hiyo ni pamoja na Sengerema, Geita na Misungwi.