ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 22, 2011

FBG TOKA R-CHUGA KUDONDOSHA CODEMIXXING

FBG; wanahiphop toka chuga chuga wafungua mwaka na concious joint kuelezea hali halisi ya taifa le2 na maisha ya mtaa yanavotupelekesha huku viongozi wanafuja fedha ya mlipa kodi,Ngoma hi inakwenda kwa jina "inaniuma kwa roho" na imerekodiwa pande za noizmekah s2dio arachuga na harakati za kushoot video yake zilikwama kutokana na fujo kuzuka mjini arusha siku hiyo hiyo ilopangwa kushoot...FBG wanamalizia tape yao itayotolewa "FREE" na itakwenda kwa jina "codemixxing",collection hiyo itajumuisha pia wimbo huu na nyinginezo kibaona mwezi wa tatu mashabiki wategemee vibe za kumwaga

Friday, January 21, 2011

DIWANI STANISLAUS MABULA AANZA KUTEKELEZA AHADI ZAKE.

DIWANI wa Kata ya Mkolani ameanza utekelezaji wa Ilani ya CCM na ahadi zake kwa kutoa msaada wa mifuko 45 ya Saruji na kuchangia Shilingi 350,000/- za gharama ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, ofisi katika Sekondari ya Luchelele na shule ya msingi Mkolani Wilayani Nyamagana.Akikabidhi mifuko 25 ya saruji kwa Uongozi wa shule ya msingi Mkolani jana Diwani Stanislaus Mabula wa Kata hiyo(CCM),amesema kwamba tangu kumalizika kwa uchaguzi ameanza kutembelea Kata yake kufatilia kero ambazo ameanza kuzitafutia ufumbuzi wa haraka ikiwemo ya kutekeleza ahadi zake alizoahidi wakati wa kampeni za uchaguzi Mkuu uliopita.

Diwani Stanislaus Mabula (aliyenyoosha kidole) akipata maelezo ya mipaka ya eneo la chumba cha darasa na ofisi mpya za walimu toka kwa mkuu wa shule mwalimu Mbokela Sahani (mwenye shati-njano), mbele ya mtendaji wa kata Mtani Evarist (mwenye shati-pinki) na anayeandika ni afisa maendeleo kata Raphael mphulu.

Huku wengine wakijisomea ni Wakati wa mapumziko wanafunzi ndani ya moja ya madarasa ya shule hiyo.

Mheshimiwa akishiriki kuondoa nyasi zilizoota eneo la shule.

Hili ni Darasa kamili na madawati yake.

UHABA WA VYOO.
Kaimu Mkuu wa shule hiyo ambaye ni Msaidizi mwalimu Mbokela Sahani akipokea msaada huo wa Saruji amesema kwamba viongozi waliopo kwenye Kata hiyo kwa kushirikiana na wazazi waendelee kuisaidia shule hiyo kwakuwa bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo upungufu wa madarasa, Ofisi za walimu (Staff), maktaba na matundu ya vyoo ambayo hayatoshi na yamekwisha jaa.

Wataalam wetu wa kesho katika kamera yako.

PICHA YA PAMOJA.
Mabula amewataka walimu hao kutokubali kutumiwa na baadhi ya watu na wanasiasa kwa lengo la kudhoofisha utoaji wa taaluma na badala yake matatizo yao yapelekwe kwenye vyombo husika ili serikali iyatafutie ufumbuzi wa haraka huku wao wakihakikisha elimu na ufaulishaji wanafunzi katika shule zao ukiboreka kila mwaka na maadili ya watoto yakiwa mazuri.

Thursday, January 20, 2011

USIKU WA JANA STONE......

Wakazi wakijinafasi kwa raha zao.

Khadija Kopa akimwaga burudani ndani ya ming'aro ya usiku wa mwambao stone club.

Ma-VIP na kona yao, kushoto kabisa ni mshereheshaji wa usiku huo toka clouds TV, Sakina Lyoka wa kipindi cha muziki wa Taarab kiitwacho Ng'aring'ari, ambaye vilevile alikuwa akichukuwa baadhi ya matukio yatakayoonekana ndani ya kipindi chake.

Maneno 'kuntu'.

Sabaha Salum akiwatunukisha mashabiki wake burudani.

Usiku huo wa utofauti ambao sijapata kuona ulikuwa wanukia ile kisawasawa, nauliza: naambiwa ni mambo ya marashi ya udi uturi toka Ughaibuni.

Askwambie mtu, samaki wa Mwanza wanafaida.

MWANZA BEST OFFICERS AWARDS

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Saidi Mwema kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza, wametoa jumla ya shilingi milioni 3200000/= kwa askari 31 walioshiriki katika tukio la kupambana na majambazi lililotokea desemba 29 mwaka jana katika kijiji cha kanyama wilaya ya Magu mkoani hapa.Mkuu wa mkoa wa Mwanza Abbas Kandoro akikabidhi cheti na pesa taslimu kwa mmoja wa polisi walioshiriki zoezi la kupambana na majambazi wezi wa magari, mapambano yaliyotokea katika Kijiji cha Kanyama, Kata ya Kisesa wilayani Magu, mkoani Mwanza.

Sherehe fupi ya kuwapongeza Askari hao iliyokwenda sanjari na kuwakabidhi fedha na kuwatunuku vyeti imefanyika leo asubuhi katika uwanja wa polisi mabatini jijini Mwanza na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa ngazi za wilaya na mkoa.

"Jeshi la polisi ngazi ya mkoa tulipanga kutoa kiasi hicho cha fedha nilichokitaja lakini mkuu wetu wa kazi IGP Mwema kwa kutambua kazi nzuri waliyo ifanya vijana hawa akaongeza sh, 50,000/= kwa kila mmoja, vivyo leo tutawakabidhi shilingi lakimoja kila mmoja na kwa wale majeruhi wawili watakabidhiwa shilingi lakimoja na elfu hamsini kila mmoja" Kaimu kamanda wa pilisi mkoa wa Mwanza Nonosius Komba Akiongea wakati wa kumkaribisha mkuu wa Mkoa wa Mwanza.

Kamanda Komba amesema hali za majeruhi wote wawili zinaendelea vizuri ambapo PC Erasto aliyejeruhiwa kwa risasi katika paja na mkono wake wa kulia ameruhusiwa kutoka hospitalini wakati CPL jumanne aliyepigwa risasi mbili begani katika mkono wake wa kushoto anaendelea na matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Bugando
Gwaride la jeshi la polisi.

Wakati mgeni rasmi akihutubia, askari huyu aliyekuwa yummoja kati ya waliokuwa wamesimama wima ktk rigwaride wakisikiliza hotuba alianguka ghafla, Pichani akipelekwa eneo la huduma ya kwanza.

Aidha mkuu wa mkoa wa Mwanza amewataka wananchi kuheshimu utawala wa sheria kwa vile nchi inaongozwa kwa misingi ya kanuni na taratibu za utawala bora, wananchi waachane na dhana mbaya ya kuchukuwa sheria mkononi bali wanapomtuhumu au kumkamata mhalifu ni vyema wakamkabidhi mikononi mwa polisi ili sheria zichukuwe mkondo wake.

Picha ya pamoja askari waliotunukiwa na kaimu kamanda wa polisi.

Picha ya pamoja viongozi wa serikali pamoja na askari waliotunukiwa.

TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2011 ZAZINDULIWA RASMI.

Pichani kushoto ni mkurugenzi wa masoko wa TBL, David Minja pamoja na Katibu Mkuu wa BASATA, Gonche Materego wakizindua rasmi tuzo za kilimanjaro Tanzania music Award 2011 mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kushuhudia hafla hiyo. Wanaoshuhudia kulia ni Mratibu wa tuzo hizo kutoka BASATA, Angelo Luhala pamoja na Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro, George Kavishe.

HABARI ZAIDI TEMBELEA BLOGU YA JIACHIE

Wednesday, January 19, 2011

JEASHI LA CONGO 'LILIONGOZA UBAKAJI'

Kamanda wa jeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameshutumiwa kwa kuongoza ubakaji wa wanawake takriban 50 uliofanyika hivi karibuni.Kumekuwa na ripoti nyingi za ubakaji huko Congo lakini tukio hili linaaminiwa kuwa la kwanza kwa idadi kubwa ya wanawake kubakwa likihusishwa jeshi. Mmoja wa waliobakwa, pamoja na vyanzo vilivyonukuliwa katika ripoti ya umoja wa mataifa, wote wanamshutumu Lt Col Kibibi Mutware kwa kuhusika na ubakaji huo uliofanyika mwaka mpya mjini Fizi.

Dr Faise Chacha, mkuu wa hospitali ya Fizi ameeleza, " Askari mmoja aliuawa hapa karibu kabisa na hospitali hii." "Hiyo ilisababisha wasiwasi na wagonjwa wetu wote wakakimbia. Tulirudi siku ya pili asubuhi na tukaanza kuwapokea watu waliokuwa wamepigwa kisu na wengine- wanawake- waliobakwa." Dr huyo na shirika la kitabibu la kutoa msaada Medecins Sans Frontieres wamewatibu waathirika 51 waliobakwa mpaka sasa.

Kama ilivyo kwa matukio ya awali huko Congo, wengi wanatarajiwa kuficha yaliyowasibu kuepuka kuachwa na waume na familia zao. Wawili miongoni mwa wanawake hao walikubali kuzungumza na BBC ilimradi tu wasitajwe majina yao.

Mmoja aliiambia BBC, " Nilibakwa mbele ya watoto wangu wanne." "Ninaona aibu, ninaona aibu sana. Nikikutana na watu wawili au watatu ambao wanajadili jambo, naanza kuhisi tu kuwa wananizungumzia mimi, hata kama si kuhusu mie."

Mwanamke huyo mwengine alifanikiwa kumtambua aliyembaka. "Ilikuwa jioni na walionibaka walikuwa wanajeshi," alisema kwa sauti ndogo, mwili wake ukiwa umefunikwa na khanga yenye rangi za kuvutia. nakuongeza kwa kusema " Walikuwa wanne- Kibibi na walinzi wake. Wameiba vitu vyetu vyote pamoja na pesa."


HISANI YA BBC SWAHILI.

CHANGAMKIA MZIGO UNAZWA BEI CHEE!!..

(a)

(b)Mambo vipi mdau? hope uko poa kabisa mashine hii inauzwa ni mpya imo kwenye box lake, Naiweka hewani kwa atakayekuwa tayari kununua tafadhali anaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi, 0756-162161 or 0762-854444 au kwa maelezo na details zote zaidi wanaweza kutembelea jojosssfashions.blogspot.com

Asante sana nakutakia kazi njema na kila la kheri.

HALO HALO MWANZA-MWANZA STONE CLUB JUMATANO YA LEO PATAKUWA PATAMU

DJ ELLY NA MC SAKINA LYOKA TOKA CLOUDS FM & TV WAKISHIRIKIANA NA MC KATUMBA WA STONE CLUB WATATUMIKA KISAWASAWA KUNAKSHI USIKU HUU WA TAARABU.
Waliosimama kutoka kushoto ni MC KATUMBA, DJ.ELLY BIG DADY 4BY4 (mzee wa Night Kali) na akiwa na Sakina Lyoka, walioketi ni waimbaji malkia wa taarab Khadija Omar Kopa na Sabaha Salum, hapa wakizungumza na wakazi wa Rock City kupitia mawimbi ya Radio Passion fm Mwanza mchana huu kuwapa menyu ya usiku wa leo ndani ya STONE CLUB Mwanza.

duh! Clouds Tv nao wamo!!..!!.

TAMKO LA WANA CCM TAWI LA KAMBARAGE SAUT KUHUSU KATIBA: WAMPONGEZA JAKAYA.

Halmashauri ya ccm tawi la kambarage ya chuo cha Mt. Agustino (SAUT) imempongeza Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Kikwete kwa uamuzi wake wa hekima na busara katika salamu zake za mwaka mpya alizozitoa tarehe 31dec2010 kwa kuunda tume ya kuratibu mchakato wa katiba mpya."Katika salamu za zake Mh.Rais aliridhia kuanzisha mchakato wa katiba mpya kwa mstakabali mwema na mapenzi ya dhati kwa watanzania kwaajili ya kulinda maslahi ya watanzania. Sisi tawi la ccm chuo kikuu cha mtakatifu Agustino Mwanza tunampongeza mheshimiwa Rais kwa hatua yake hiyo ya hekima na busara" kauli ya Mwenyekiti wa tawi hilo Silvester Yaredi.

SILVESTER YEREDI.Ushauri pia umetolewa kwa watanzania kuwa mchakato wa katiba mpya usije ukawa chanzo cha kuvunjika kwa umoja na amani yetu tuliyojiwekea kwa miaka mingi. Tuepushe hisia zetu za kisiasa, kikabila na kidini kwani katiba mpya ni kwa manufaa ya watanzania wote bila kujali itikadi ya dini, kabila wala rangi.

Vipengere vingine ndani ya salamu hizo za pongezi vinasema:- Tubishane kwa hoja kwa nia ya kujenga taifa letu na si kubomoa. Katiba mpya iwe chachu ya kuleta mabadiliko katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Bila kujali itikadi za vyama wanachuo wa chuo cha SAUT Mwanza kwa hivi sasa wanaendelea na mijadala na makongamano kuijadili katiba ya sasa, kung'amua mapungufu yaliyomo, kuorodhesha mapendekezo, hatimaye pindi itakapo fika wakati wapate kuyawasilisha kunakohusika.

Halmashauri hiyo ya ccm tawi la kambarage SAUT, kwa upande wake imekubali kuwa katiba ya sasa inamapungufu. "Upungufu uko kutokana na wakati" Aidha tawi hilo limeiomba tume itakayoundwa kuratibu mchakato huo wa katiba ifanye kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa ili nchi ipate katiba nzuri inayojali na kukidhi matakwa ya watanzania wote.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu ibariki Afrika.

Tuesday, January 18, 2011

JESHI LA POLISI MWANZA LANASA VIPUSA VYA FARU WA RAISI ALIYEUAWA.

Polisi mkoani Mwanza, imewakamata watu wawili akiwamo afisa wa wanyama pori, Allchraus Jacob (31),na Kasika John (44) ambaye ni mkuluma wa wilayani Bunda, wakijaribu kuuza pembe za kifaru maarufu kwa jina la George (12) akifahamika kama faru wa Rais Jakaya Kikwete, aliyeuawa na majangili, Desemba mwaka jana. Jeshi hilo limekamata Vipusa vya Faru vikitembezwa sokoni kutafuta Mteja, Inasemekana kuwa pembe hizi za faru (Vipusa) hutumika kutengenezea dawa ya kuongeza nguvu za Kiume huko katika nchi za Falme za Kiarabu, Japan, Korea na hata china ambako vinasoko kubwa sana.

#####WAKATI HUO HUO jeshi la polisi mkoani mwanza lanawashikilia watu wanne, wawili kati yao wakiwa na bunduki aina ya SMG na risasi 64 ambazo zilikuwa zimefichwa ndani ya begi la nguo zikisafirishwa kwenda wilayani Geita..Kaimu wa polisi amesema kuwa watuhumiwa ambao walikamatwa na begi hilo la silaha walijitambulisha kama mke na mume na kwamba walikuwa wakielekea katika kijiji cha Bukondo wilayani Geita.

Ndani ya begi hilo kulikuwa na viatu vya kike, panga moja na shoka ambavyo vilikuwa vimefungwa katika mfuko wa sandarusi pamoja na vikaratasi vidogovidogo vilivyokuwa vimefungwa dawa mbalimbali za mitishamba ambavyo walidai kuwa ni hirizi za dawa za kusaidia wakati wa matukio ya ujambazi.

Baada ya kuwakamata watu hao waliweza kuwataja wenzao ambao walikuwa bado hawajaondoka Mwanza kuungana nao katika shughuli zao za uharamia, ambao nao waliweza kukamatwa eneo la Nyegezi wakiwa na mkakati wa safari kuelekea ambako walipanga kufanya uhalifu mwingine..

Monday, January 17, 2011

"ITS MY BIRTHDAY!!" says BIZZO 4SHIZO

Ni mtangazaji wa The no One Radio Station in Southern Highland...87.8...88.2 & 94.7 EBONY fm.
Vwalaa! MARAFIKI WA UKWELI MTAFUTENI MDAU WENU WA UKWELI MKAMTUNUKISHE UVUMBA pia na MANEMANE.
Happy borzei braza.

HATIMAYE MH. PINDA AMALIZA UTATA UDOM.

Hatimaye waziri Mkuu wa Tanzania mh. Mizengo Pinda amesuluhisha mgogoro uliokuwepo baina ya uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na wahadhiri wa chuo hicho, kuhusu maslahi yao na wamekubali kuingia madarasani kuanzia leo Jumatatu, Januari 17, 2011.“Nimeongea na viongozi wa UDOMASA na kuwaahidi kuwa madai yenu ya posho yanaweza kukamilika mwezi wa Februari, nilitaka yaishe mwezi huu lakini kwa taratibu za HAZINA sasa hivi wameshaanza kushughulikia mishahara ya mwezi wa Januari kwa hiyo marekebisho yenu hayawezi kuwahi…wameniahidi mwezi ujao yatakamilika”, alisema huku akishangiliwa na wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA).

Amesema amemwita Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua taarifa za mahesabu ya chuo hicho ili kubaini tuhuma zilizojitokeza za watu kulipwa hundi mbili za mishahara, walioacha kazi kuendelea kuwemo kwenye payroll ya mishahara, na wengine kukosekana kabisa kwenye payroll.

Kuhusu madai ya wanafunzi ya matatizo ya maji, Waziri Mkuu alisema amemwagiza Naibu Katibu Mkuu (Fedha) Bw. John Haule, afuatilie uhamisho wa ndani wa fedha katika Wizara ya Maji ili zipatikane sh. bilioni 1.66 zinazohitajiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Majitaka Dodoma (DUWASA) kuchimba visima maeneo ya Ng’ong’ona na Ihumwa ikiwa ni pamoja na kutandaza mabomba hadi chuoni ili kupunguza shida ya maji haraka iwezekanavyo.

Pia alisema katika mipango ya muda mrefu, DUWASA pia wanataraji kupata dola za Marekani milioni 26 ambazo zitatumika kuchimba visima vingine na kujenga matanki yenye uwezo wa kuhifadhi lita milioni 12 za maji na hivyo kuondoa kabisa tatizo la maji chuoni hapo. Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof. Idris Kikula alimweleza Bw Pinda, mahitaji halisi ya maji chuoni hapo ni lita milioni 3.5 kwa siku ambazo kati ya hizo, lita milioni 1.5 ni kwa matumizi ya wanafunzi peke yao na lita nyingine milioni mbili ni kwa matumizi ya ujenzi wa majengo unaoendelea chuoni hapo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa wanataaluma wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOMASA), Bw. Idd Mwerange alimwahidi Waziri Mkuu watarudi madarasani wakati wakisubiri madai yao yakamilishwe bali aliomba kuwe na uwakilishi wa UDOMASA katika timu ya watu watakaonana na CAG.


KWA HISANI YA BBC SWAHILI.

HAPA NA KULEee!...! ' KOSHA MACHO NDUGU'

Wanauzwa hawa! Maubunifu katika utafutaji ngawira.

Ukitaka swala, twiga, bata we mwenyewe tu! Ni kunakshi tu bustani na wanyama Feki.

Wabongo bwana OOOh oh pesa za sasa hivi hamna kitu' laini kama karatasi za kunyongea..., zinachafuka upesiii, ukiishika kwenye kiganja muda mrefu inapoteza uboraaaa.. Ziko kama feki feki hiviii..(Nimeshuhudia mwenyewe kwa baadhi ya watoa huduma hususani daladala wakizikataa fedha hizo). Je! wewe unazionaje, Je! Umezipendaaa?

Mzalendo akidadisi vihusishi vya noti mpya kutoka katika matangazo ya noti zetu mpya kwenye kuta za mitaa ya kituo cha stendi ya sahara.

Watoto hawa wa mitaani wanaonekana kila siku eneo hili lililo katikati ya jiji pembezoni mwa uzio wa benki moja, wakiombaomba kisha kucheza kamali baina ya wao kwa wao. Tunawatizama tu! biashara inaendelea..

Wajameni uchafu ni mazoea ama mauzembe?

MZEE MANDELA AVUMISHIWA KIFO...!

Habari zimetapakaa kutoka Johannesburg nchini Afrika kusini zikidokeza kuwa , uvumi umezagaa jijini humo kuwa Raisi wa zamani wa nchi hiyo Mzee Nelson Mandela yu taabani anaumwa na hali yake ni majaaliwa.Msemaji wa mfuko wa Nelson Mandela Sello Hatang amekanusha taarifa hizo siku ya jumamosi na kusema Mzee Mandela mwenye miaka 92 alikuwa katika mapumziko na mkewe Graca Machel na kwamba walikokwenda na wanachokifanya ni siri yao wawili na ni haki ya faragha kwa kila mwanadamu nayo inapaswa kuheshimiwa.

Hata hivyo kuna habari kuwa hali ya mzee huyo imezorota mno na wengine wamekuwa wakiwasiliana wakisema kuwa amekufa jambo ambalo limekanushwa vikali na watu wake wa karibu.

Hata hiyo vyanzo vya uhakika vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo vimeonyesha kuanza kukubaliana na uvumi huo.


Source wa habari: www.news24.com/SouthAfrica