ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 9, 2011

MIAKA 50 YA UHURU SHULE YA MSINGI NYAMAGANA YAZIDI KUSHUKA CHINI KIMAENDELEO

Ni moja kati ya shule kongwe jijini Mwanza iliyokuwa ikisifika kuwa na mazingira mazuri, vyumba vya madarasa, madawati, ufundishaji mzuri na vitabu vya kufundishia, wafanyabiashara watz wenye asili ya kiasia na wazawa wenye uwezo walikuwa wakileta watoto wao kusoma hapa....lakini leo ukiitembelea mmmmmmh...

Kwa uchunguzi wa haraka nilioufanya, baadhi ya madarasa shuleni hapa, hii leo hayana hata sakafu, hali ambayo inawalazimu wanafunzi kukaa kwenye vumbi na kusababisha usumbufu mkubwa kwa walimu katika ufundishaji wao.


Pamoja na kwamba ni shule ambayo iko katikati ya jiji la Mwanza baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wanakalia mawe na matofali, hali ambayo imekuwa ikichangia kuporomoka kwa kiwango cha elimu.

Vyoo ndiyo kabisaaaa 'chokesti' Pamoja na kwamba matatizo haya ni la muda mrefu, lakini viongozi hasa wanasiasa wanatoa ahadi tu wasizozitekelezeka, ni mfanyabiashara mmoja tu aitwaye Aritaf Mansoor aka Dogo kwa pesa zake ndiye aliye ameamua kujenga madarasa mengine shuleni hapo.

Mlio soma hapa enzi za Mwalimu mupooo? Jeh! mwayaona haya?

Tupe maoni yako

4 comments:

  1. Duh!Hali inatisha na kusikitisha..Kama Nyamagana ipo hivi vipi shule za Ibitabagumba au kome mchangani zitakuwaje?
    Hongera sana G sengo kwa kutuletea Taswira za jiji la mwanza sio kila siku watu wanaweka picha za majengo ya NSSF PPF.
    Nilibahati kusoma hapo darasa la sita la saba.Hakika hali inasikitisha sana sana..Something should be done..

    ReplyDelete
  2. Tunaomba utuwekee na picha za Nyanza.

    ReplyDelete
  3. Aisee Nyamagana ndio imekuwa hivi!!am shocked nilikuwa napicha nyingine kabisa kuhusu hii shule. Nimetoka Mza muda mrefu sana na hali ya shule hii imenishtua mnoo. Wakati mwingine nadhani sie wenyewe wana Mza tunatakiwa kulipa fadhila kwa kusaidia vitu kama hivi. Binafsi nafikiria kipi cha kusaidia Mungu akipenda soon nakuja Mza

    ReplyDelete
  4. Hata walimu huwa haangali usfi.mwalimu kwake
    anashindwa kupasafiha loe ijeiwe shule Loooo....
    panatisha kama hali ndiyo hii.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.