ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 12, 2011

TAARIFA ; NAOMBA KUWASILISHA....


TAARIFA YA MABADILIKO YA MTANDAO WA MATUKIO NA WANAVYUO.
Sasa Blog hii imeungana na wanavyuo watanzania wanaosoma nje ya Tanzania Kwanza kabisa tunapenda kuwasalimu wadau wote popote Duniani,tunatumaini ya kwamba bado mnaendelea na ujenzi wa taifa letu.

Kwa heshima na Taadhima tunapenda kuchukua nafasi hii kuwapa taarifa kwamba mtandao wenu wa Matukio na wanavyuo www.tzwanavyuo.blogspot.com sasa tumefanya mabadiliko makubwa ambapo tumewaunganisha wanavyuo watanzania wanaosoma Tanzania na walio Nje ya Tanzania, Tumefanya hivi kutokana na malalamiko na maombi ya Wanavyuo waliopo nje ya tanzania kutaka kuanza kutuma matukio yao ambayo yanajili huko waliko, Tumelipokea ombi hili na sasa mwanachuo yeyote ataweza kutuma habari zake ama habari zao hapa.

Pia kwa watumishi wa vyuo Hapa nchini Tanzania mnakaribishwa sana kuleta matangazo yenu ikiwa ni nafasi za masomo ama kama kuna habari ya haraka mnataka iwafikie wanafunzi basi mtutumie moja kwa moja nasi tutaiweka muda huo huo.

Mabadiliko mengine tuliyo yafanya kwa faida ya watu wote ni kwamba sasa tuna panel upande wa kulia ambapo tumeorodhesha tovuti za vyuo vyote vya Tanzania,pia tumeweka na mambo mengine mengi ya msingi ambayo yatapata kuwasaidia.

Mtandao wa wanafunzi ambao unafanya kazi kama Facebook (Social network)upo hewani mnakaribishwa kujiunga www.tzuniversitiesconnects.tk mnakaribishwa sana pia mtakutana na wanavyuo wengine.Tunatanguliza shukrani zetu za Dhati.

Tumumie matukio na habari zozote zihusuzo vyuo hapa: twanavyuo@live.com
Tembelea Mtandao wa Matukio na wanavyuo hapa: www.tzwanavyuo.blogspot.com

Kwa niaba ya wanavyuo wote,
Matukio na wanavyuo Crew.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.