ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 21, 2011

DC ILEMELA AOMBA MSAAADA WA CHAKULA NA MAHEMA KWA WALIOATHIRI NA KIMBUNGA MWANZA.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wilaya ya Ilemela na Kaimu Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Amanzi ameyaomba mashirika, watu binafsi na wasamaria wema kujitokeza kutoa msaada wa vyakula kwa watu walioathiriwa na kimbunga cha upepo katika Kata ya Bugogwa wilayani Ilemela. Said Amanzi.

Amanzi ameyasema hayo jana jijini Mwanza wakati akitoa tathimini ya uharibifu uliosababishwa na mvua hiyo kwa waandishi wa habari na kuleta athari kubwa miongoni mwa wakazi wa Kata hiyo.

Miongoni mwa sehemu zilizoharibiwa vibaya na mvua hiyo ni pamoja na vyumba vinne vya madarasa na Ofisi ya Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Igombe, Jengo la Ofisi ya CCM na lile la Kanisa la Roman Katholiki.

Katika tukio hilo lililotokea usiku wa Oktoba 18 mwaka huu lililosababishwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali jumla ya kaya 322 zimeathirika kutokana na athari hiyo ya mvua na kimbunga na Inakadiriwa pia kaya zipatazo 45 hazina chakula kabisa, zinahitaji msaada wa haraka ikiwa ni pamoja na mahema na chakula hii ni kutokana na vyakula vyao kuharibiwa na mvua.

Jumla ya watu 14 wamjeruhiwa na wote wamekwishatibiwa katika Hosipitali ya Rufaa ya Bugando na wamekwisharuhusiwa.

Tayari hatua mbalimbali zimekwishachukuliwa kuwanusuru wakazi hao ikiwa ni pamoja na kuundwa kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya tathimini ya kina ya athari hizo kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.