ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 10, 2011

LATEST UPDATES ZA KUZAMA KWA MELI YA SPICE ISLANDERS - ABIRIA 250 WAOKOLEWA

Picha kupitia TBC1.


Watu 250 wameokolewa wakiwa hai katika meli iliyozama ya Mv Spice Islanders iliyokuwa ikitokea Bandari ya Malindi Unguja kuelekea Bandari ya Wete Kisiwani Pemba.

Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema watu hao wameokolewa na vikosi vya uokoaji na wananchi mbalimbali wanaotoa msaada wa uokozi katika tukio la kuzama kwa meli hiyo Nungwi Mkoa wa Kaskazini unguja.

Waziri Aboud amesema watu hao wamesafirishwa kwa kutumia Boti zinazokwenda kwa kasi za zanzibar ambazo zilikwenda kutoa msaada katika eneo la tukio.

Amesema watu hao baada ya kufika Bandari ya Malindi Unguja watapelekwa Viwnja vya maisara kwa ajili ya kuungana na familia na jamaa zao.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali mohamed Shein yupo katika eneo la tukio huko Nungwi ili kujionea hali halisi ya tukio hilo na maendeleo yake.

IMETOLEWA NA:-
IDARA YA HABARI (MAELEZO) ZANZIBAR
10/09/2011

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.