ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 1, 2011

WENGI TUNAJUWA UMUHIMU WA MATUNDA KIAFYA LAKINI..


Matunda mazuri ni yale yaliyoivia mtini na matunda ni vyema yakaliwa na kambakamba zake na siyo kuchujwa kama wengi tufanyavyo.
Matunda na mbogamboga ni muhimu sana kwa afya, haya-haya sasa tununue na tule!! KWANI TUNAJUA UMUHIMU WAKE. Kwani wewe hujui umuhimu wa matunda na mbogamboga kwa afya yako?

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. sawa tunatambua umuhimu wa matunda na mboga mboga, lakini mboga zinazolimwa na kuvunwa pembezoni mwa ziwa victoria hususan kata ya Kirumba kuanzia daraja la mto Mirongo hadi njia panda ya Mwaloni Kirumba, na eneo la Iloganzala kata ya Pasiansi ni hatari sana ! Mboga hizo zipo pembezoni mwa barabara ambapo magari na vyombo vya moto vinatoa moshi ikiwa ni mchakato wa kuunguza mafuta ambayo yana madini ya risasi (lead - Pb) ni hatari kwa afya za binadamu. Tunakufa pole pole kutokana na kula mboga zilizozalishwa katika maeneo ambayo si salama kimazingira. Aidha, wakati mwingine walzalishaji hao wa mboga hutumia madawa ya kuulia wadudu kwenye mimea hata siku chini ya 14 kabla ya kuvuna. Dawa hizi hubaki katika majani na hivyo kuwa sumu kwa mlaji.
    Ni ujasilia mali kwa anayelima na kuuza. Lakini kwa mlaji mboga mboga hizo hazifanyi kazi inayostahili kama wewe mtangazaji unavyojaribu kutushawishi kuwa twajua umuhimu wa matunda na mboga mboga. Badala yake wakulima wanawaua walaji pole pole. Ndiyo maana baada ya muda matatizo ya figo, maini, shinikizo la damu na magonjwa mengine mengi hatari yanajitokeza. Tabia yetu ya kutopima afya mara kwa mara husababisha mtu kugundua tatizo wakati limekwisha komaa. Aidha, elimu ndogo ya afya ya walaji wengi, matatizo ya namna hii yanapojitokeza, badala ya kwenda hospitali unawakuta kwa sangoma wakifikiri wamelogwa. Kumbe wachawi ni wakulima wa mboga mboga pembezoni mwa barabara.
    CHUKUENI TAHADHARI, ACHENI KUNUNUA MBOGA ZILIZOLIMWA PEMBEZONI MWA BARABARA MADHARA YAKE NI MAKUBWA MNO KWA WATUMIAJI WA MUDA MREFU WA MBOGA HIZO.Pia mnaponunua mnawahamasisha waendelee kuharibu mazingira ya ziwa ! kaombwe

    ReplyDelete
  2. Aaaaaa KAOMBWEeeee!!! umetisha kaka aksante kwa elimu.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.