ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 3, 2011

MUBARAK WA MISRI AKANA MASHTAKA

Aliyekuwa Rais wa Misri Hosni Mubarak amekana mashtaka ya rushwa na kuamuru kuuliwa kwa waandamanaji, siku ya mwanzo ya kesi yake iliyofanyika mjini Cairo.Bw Hosni Mubarak

Waandishi walisema, alipelekwa akiwa kwenye kitanda cha hospitali na kuwekwa ndani ya kizimba mahakamani humo, jambo lililowashtusha wengi waliokuwa nje.

Bw Mubarak mwenye umri wa miaka 83 anashtakiwa na watoto wake wawili wa kiume, ambao pia walikana mashtaka yanayowakabili, na pia aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani Habib al-Adly na waliokuwa maafisa wengine sita.

Hukumu ya kuamuru mauaji ya waandamanaji ni adhabu ya kifo.

Takriban askari na polisi 3,000 wamezambazwa kuhakikisha kuna utulivu katika chuo cha mafunzo cha polisi ambapo kesi hiyo inasikilizwa.

Awali ilikuwa isikilizwe kwenye kituo cha mkutano cha Cairo lakini mamlaka husika zikahamisha eneo na kuunda mahakama ya muda ndani ya chuo hicho kutokana na suala la usalama.

Inakadiriwa watu 600 walitazama kesi hiyo ndani na nje ya mahakama, na mamilioni ya wengine wengi wakitazama kupitia televisheni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.