ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 3, 2011

MAGEREZA MABINGWA WA NDONDI TAIFA

Mara baada ya kuahirishwa mara kadhaa hatimaye mashindano ya wazi ya Ubingwa wa Taifa kwa mchezo wa ngumi yaliyoanza jumatatu jijini Mwanza yamemalizika jana nao timu ya Magereza Dar es salaam kuibuka washindi wa jumla.Kaimu rais wa BFT mstaafu Meja Changarawe akikabidhi kombe la Ubingwa wa jumla kwa timu ya ndondi ya Magereza.

Jofray Timoth wa Temeke akipeleka sumbwi kwa Osward Chaula wa Magereza, ambaye alishinda kwa pointi 3 kwa 0 michezo yote ikichezwa kwa round mbili kila mmoja.

Ndondi za uzito wa kilogramu 56 Wigoro Katuba toka Nyamagana (kushoto) alimtandika kwa pointi 2-1 Undule Langsoni wa Magereza


Ndondi za Uzito wa kilogramu 49, Yahya Maliki wa Temeke aliibuka mshindi dhidi ya Antony Idoa wa Magereza kwa kumkunyuga kwa pointi 3-0


Hili ndilo dimba la ndondi Taifa 2011 Uwanja wa Nyamagana jijini Mwanza.


Yona Segu v Nasser Mafuru

Ndondi za uzito wa kilogramu 60 kipute baina ya Nasser Mafuru wa Magereza na Yona Segu wa Temeke kiliisha kwa Yona kushinda kwa pointi.

Kaimu rais wa BFT mstaafu Meja Changarawe akikabidhi kombe la Ushindi nafasi ya pili kwa timu ya Nyamagana.

Kaimu rais wa BFT mstaafu Meja Changarawe akikabidhi kombe la ushindi ndondi nafasi ya tatu kwa Temeke.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.